Wednesday, November 9, 2016

Abdul

RIWAYA : DUNIA INANICHUKIA
simu      : 0746206428

           4

ILIPOISHIA....
Yule mtu aliekuwa akifuatwa nyuma na askari bila yeye mwenyewe kujua alitembea kwa haraka akisunta ili aivuke barabara alioiona mbele yake, kutokana na waswasi na mawazo pamoja na kelele ya mvua iliyo piga kwenye bati za nyumba za mitaa hiyo, huyo kijana hakusikia kabisa muungurumo wa gari la polisi lilokuwa likija katika barabara aliyokuwa akiiwahi ili avuke,
alipoingia tu barabarani mikono yake ikiwa bado kwenye mifuko wa koti ndipo kwa kihoro kikubwa macho yake yaliishuhudia gari ya polisi ikija kwa kasi alipo simama!
ENDELEA.....
"ni abdul"
dereva wa gari alibabaika kumuona abdul akiwa katikati ya barabara na kabla haja fanya lolote, kwa wepesi ambao haukutalajiwa abdul alijitupa pembeni huku akitoa mkono wake wakulia kwenye koti!
, pah pah !, miliyo ya risasi ili sikika huku abdul akijitupa pembezoni mwa barabara,
<*muda wote abdul alipo kuwa anatembea mkono wa kulia ulikuwa umeshika bastola ndani ya koti na kipindi anajitupa pembeni   alichomoa mkono wake kwenye koti na kufyatua risasi mbili akiwa hewani kuilekea ile gari ya polisi ,
abdul baada ya kujitupa chini akiwa anataka ainuke aangalie sehemu ya kujificha hapo hapo akasikia milipuko mikubwa ya risasi na muda huo akashuhudia baadhi ya risasi zikichimba kuta za nyumba za eneo hilo, abdul akabaki pale chini akiwa hana cha kufanya kwani risasi zilikuja kwa wingi eneo alili kuwepo maji yakiwa yamemfika shingoni.
****
robert akiwa anaendesha gari kwa kasi mara alisikia ile milipuko ya risasi ikitokea upande aliokua akielekea moyo wa robert ukaripuka kwa furaha akijua abdul kaonekana"yah hisia zangu zilikwa sahihi upande wa magharibi ndipo alipo kimbilia abdul" alijisemea robert huku akijisifu kwa uhodari wa kuhisia , mara ghafla akasikia milipuko mingine mfululizo ikitokea upande wake wa kulia, robert alipigwa butwaa kwani alisikia milipuko ya risasi pande mbili tofauti hakutaka kuamini kule aliposikia risasi mara ya kwanza ndiko aliko sikia mara ya pili ilikuwa ni sehemu mbili tofauti , robert akiwa anaendelea kujiuliza hapohapo radio call yake ikatoa mlio wa mkoromo,
"inspector robert naongea" alisema robert baada ya kusogeza radio call kinywani mwake,
" ehh afande tumevamiwa huku na wenzetu wa nne wamesha uliwa ndani ya guest walio enda kukagua" sauti iliongea ya upande wa pili ,"unafikiri atakuwa ni abdul" aliuliza robert,
"nafikiri maana wenzetu waliingia kukagua kwenye guest hiyo na mara wakashambuliwa ndani ya guest, na walio shambulia wapo zaidi ya mmoja kwa kifupi tunaomba msaada msaada" taarifa hii ilimchanganya robert robert alijiuliza ina maana abdul alikuwa na kundi lake huko tandika 'yah inaweza ikawa ndomaana aliamua kukimbilia huku' alijijibu robert,
"hemu muulize guest ina itwaje" sauti ya mwenye kiti iliuliza kutokea nyuma ya robert,
"ah wazo zuri.... eti we hiyo guest inaitwaje" robert aliongea na watu wawili kwa wakati mmoja,
"ah eh ni coconut guest"
"washa gari twende na pajua"alisema mwenye kiti,
"sawa lakini acha ni wape kwanza taarifa askari wote" alijibu robert,
robert akawaalifu askari wote waliokuwa kwenye oparesheni waelekee coconut guest kwani huko ndiko waliko shambuliwa wenzao.
robert alipo maliza akawasha gari na kuanza kuondoka .
<<<*****
askari waliokuwa mtaani baada ya kufanya msako bila kufanikiwa waliamua waanze kusogea upande wa upande wa magharibi kama walivyo ambiwa na robert, gari lenye askari kumi na moja lilianza kuondoka kuelekea magharibi na ni hili gari ambalo askari wake walikutana na yule muogota kopo alie waelekeza alipo muona abdul. na gari la pili lili ondoka na askari kumi na mbili gari hili lilipita barabara nyingene, baada ya mwendo wa kasi dreva wa gari lenye askari kumi na mbili alisimamasha gari baada ya kuona bar moja na guest moja pamoja na grocery moja ndani ya mtaa alio kuepo akaona ni vyema washuke na wakague ile guest na bar pamoja na grocery. "oya shukeni tukague eneo hili fasta tuondoke.... wanne muende kwenye ile guest na wanne wengine waende kukagua kwenye ile bar na watatu mnifuate tukakague ile ile grocery", alisema dreva alie onekana kuwa kiongozi wa askari wale. kulitokea ubishi kidogo kwani kuna askari nane wali gombea kwenda kwenye guest kukagua , hii ilitokana na askari hawa kila walipo enda kukagua guest wali vunja milango ya vyumba ambamo wali kuta baadi ya watu wakiwa wakifanya mapenzi na wali wakuta wakiwa kama walivyo zaliwa kitendo hiki kikapelekea askari kupenda kukagua guest kuliko sehemu nyingine , yule askari alie kuwa anaongoza askari hao ali wakemea baada ya kuona wana leta masihara kwenye kazi,
"haya bwana nendeni mkawachungulie vizuri" alisema askari mmoja katika wale wanane huku akijitoa kwenye kundi lile na wenzake watatu wakafuate,
"bwana sasahivi sio zamu yenu tuachieni tukajionee vibwanga" alisema askari mmoja kati ya wale wanne walio baki.
msako ukaanza na wale askari waliokuwa wamepangwa kukagua guest walitembea haraka na kuingi ndani ya guest hiyo iliyo itwa coconut guest, askari wale wakatoa taarifa juu ya msako wao ndani ya guest na wakaanza kukagua,
walivyo fika kwenye korido ya vyumba vya guest wakajigawa wawili wawili ili waanze kukagua vyumba vile,
askari wawili wakagonga chumba kimoja wakafunguliwa wakaingia waanze kukagua, na askari wawili wengine waka gonga chumba kilichofuata ... kimya! hakuna aliitika wala kufungua chumba kile.
askari hawa wawili askari wawili wakaangaliana wakajua mule ndani kilicho kuwa kinaendelea ni mapenzi , askari hao wakapeana ishara kuwa wavunje mlango ili wakajionee mambo, askari mmoja akarudi nyuma na kuurukia teke mlango ukafunguka na ghafla askari alie bomoa mlango akatupwa kwenye ukuta na kuanguka chini kama mzigo! na mlio wa risasi ukasikika! askari wapili alipigwa butwaa hakujua mwenzake katupwa na nini, askari akainua bunduki yake kuelekea kwenye kile chumba lakini alichewa kwani hapohapo risasi mbili zili toboa kifua chake zikitokea kwenye chumba walicho bomoa mlango! askari wawili wakawa chini huku mmoja akiwa na tundu likivuja damu kwenye paji la uso wake. wale askari wengine walioingia kwenye chumba cha kwanza walisikia ile milipuko ya risasi iliyo tokea chumba cha pili wakatoka haraka ili wawa saidie wenzao lakini walikua na bahati mbaya kwani walivyo tokeza tu kwenye korido walipokelewa na risasi mfululizo zilizo toka kwa watu wawili walio simama kwenye maiti za wenzao. watu hao wawili baada ya kuona askari wanne wamesha kufa, watu hawa wawili wakaingia kwenye chumba walicho kuwemo wakachukua mabegi yao mawili yaliojaa wakaanza kukimbia wakitoka nje ya guest askari .
*** wale askari wanane walio kuwa wanafanya msako kwenye bar na grocery walisikia ile milipuko ya risasi kutokea kwenye guest walio ingia wenzao ndipo wakaanza kukimbia kwenda kuwa saidia wenzao,
"itakua ni abdul kashambulia tuwahi tuka wasaidie wenzetu" alisema yule kiongozi huku akitimka mbio.
walivyokua wanaiingia ndani ya guest ile ndipo wakaona wale vijana wawili wenye mabegi wakiwa na bastola mikononi mwao wakitokea kwenye korido walikua kama umbali wa hatua thelasini askari hawa kusita walianza kuwatupia risasi wale watu ambao nao kwa wepesi walijitupa chini waka biringita kuridi kwenye korido ambapo walipata cover na kuanza kuwatupia risasi askari bila kuwa pata kwani askari nao walikuwa wame jikinga kwenye ukuta wa counter, asakari na wale watu wawili wakaendele kutupiana bila kupatana.
yule kiongozi wa askri wale alivyo iona hari ile ndipo alipo amua kumpa taarifa robert juu ya tatizo hilo la coconut guest.
*****>>>
taarifa alietoa robert ilizagaa kwa askari wote ndani ya oparesheni ile askari wakaanza kumiminika kuelekea coconut guest,
robert nae kwa kuelekezwa na mwenye kiti akafanikiwa kufika coconut guest na magari mengine ya polisi yakafika eneo hilo na askari wakazunguka guest hiyo bundiki zao zikiwa makini mikononi mwao, askari wakaanza kujiandaa wavamie ndani ya guest hiyo........
je? hawa watu wawili walio ua polisi wanne ni kina nani? kwani wame ua polisi?
je?nini kitawakuta maana wamezungukwa na asakari.
upande wa pili abdul alijitupa chini na kuachia risasi mbili, lakini kipindi anataka kuamka ana shuhudia risasi zikitua eneo alipo na risasi nyingine zina chimba kuta za eneo hilo je? abdul atapona hapo?
tukutane kesho saa tisa upate kujua mengi zaidi.

No comments:

Post a Comment

Iblame my body

RIWAYA   : I'BLAME MY BODY ( NAULAUMU MWILI WANGU ) Imezaminiwa na   Simulizimahiri.blogspot.com Mahakama kubwa ya kesi za jina...