Saturday, October 29, 2016

kisasi

RIWAYA : KISASI
0746206428 whatsapp
imezazaminiwa na simulizimahiri.blogspot.com
Baada ya lile sekeseke zito  lilio sababisha mvutano mkubwa baina ya vyama viwili vya siasa vilivyo minyana vikali vikiwania uongozi wa taifa la tanzania huku kila chama kikipigana kufa kupona ilihali tu kimsimamishe kiongozi kwenye kiti uraisi..
vijembe vya kisiasa pamoja na kukashifiana kwa viongozi walio wania  kiti kile vilichukua  nafasi  kubwa katika sera za kampeni zao, ama hakika uchaguzi huo ulio lindima mwaka 2015 ulikuwa na changa moto kubwa kuliko chaguzi zote zilizopita kwani chama tawala kili pambana na upinzani mkubwa kutoka kwa chama pinzani mpaka kufikia hatua ya kutabiriwa machafuko ya amani katika uchaguzi huo nchini tanzania.
Lakini hakuna mwazo lisilo na mwisho, chama tawala kilishinda kwakishindo na kumsimamisha mgombea wao Mh raisi nakuanza kuiendesha nchi kwa amani na utulivu.
na kama ilivyo kuwa kawaida kila raisi mpya akiapishwa basi hufanya msamaa kwa wafungwa ndivyo hivyo alivyo fanya Mh rais mpya kwa baadhi .
UKONGA ni moja ya magereza yaliyo bahatika kupitiwa na msamaa huo ambao uli wasamehe wafungwa wenye miaka zaidi ya stini na wenye magonjwa makubwa
na siku ya leo ndio walikuwa wakiachiwa..
ndani ya ofisi ya bwana jela asubuhi ya saa tano kulikuwa na wafugwa sita walio kuwa wametawaliwa na furaha kubwa ya kubahatika kupata msamaha wa raisi na muda huu walikuea kwenye usahiri wa kusaini ili waondoke gerezani lile wakaishi maisha yao.wafungwa watano walikuwa ni wanaume ambao kwa haki walikuwa ni mababu kasoro mmoja wao tu ndio hakuonekana kuwa na furaha nae alukuwa ni mwana dada ambaye nywere zake tu zilionesha wazi hakuwa raia harisi wa tanzania japo alikuwa amekonda na kufifia rangi lakini kama ungemuona lazima ungekili kuwa kabla ya hapa huyu dada alikuwa ni mrembo hatari! dada yule hakuwa na shauku kama waliokuwa nayo wale wafungwa wazee yeye alikuwa katulia kabisa nyuma yao akiwa kaegemea ukuta wa ofisi ile..
"haya ni zamu yako dada" aliongea mtu aliekuwa nyuma ya meza ile ya kiofisi na huyu mtu alikuwa ni bwana jela mpya...
yule dada akapiga hatua na kuisogelea ile meza akachukua karamu iliyo kuwa juu ya file lake husika.
"tia sahihi hapa na hapa" yule bwana jela alimuelekeza yule dada
na dada yule akainama kutia sahihi sehemu alizo elekezwa, wakati akitia sahihi ghafla nywere zake alizo zibana kwa nyuma zilifunguka na kuangukia mbele zikilanda usoni kwake mpaka kwenye file alilo kuwa akitia sahihi , yeye akaendelea kutia sahihi kana kwamba hakuziona nywere zake kwamba zimefunguka .
aliachia kwa utulivu ile karamu na kuilaza juu ya file na kuinuka akarudi nyuma hatua huku baadhi ya nywere zikiwa zime landa usoni.
bwana jela alimtazama kwa makini yule dada na kwakuwa bwana jela huyu aliekuwa mpya alimshangaa sana mfungwa yule kwanza  aliona yule dada hakuwa raia halisi wa tanzania asili yake ni Asia pili muonekano wa mwanamke yule alikuwa kama alishawahi kumukona
"wewe unaitwa nani "mkuu wa magereza alimuuliza kwa kumkalipia huku akimtazama kwa makini..
"Mariamu mustapha"  yule mwanamke alijibu kwa sauti iliyo kwaruza ...
"What? ni yule mariamu uliefanya maua.."  mkuu yule mpya wa mageleza alishindwa kumalizia sentesi yake kwa mshangao haraka akachukua file la mariamu lilikuwa na maelezo pamoja na vigezo vilivyo pelekea msamaha wa raisi, akasoma maelezo yale kwa ufasaha.
alishusha pumzi kubwa baada ya kumaliza kusoma kwani maelezo yalikuwa yakidai kumuachia mariamu baada yakutumikia jela miaka sita kwani ndani ya miaka minne mariamu amekuwa akisumbuliwa na kansa ya ini na kupata shinda sana gerezani hivyo mamlaka imependekezwa mariamu aaichiwe huru kwa msamaha wa raisi .
"askari watoe nje ukawakabidhi kwa mtu wa mahakama" mkuu wa magereza hakuwa na la ziada juu ya mariamu cha zaidi alishangaa sana maamuzi ya uongozi kwa kumuachia mariamu alie wahi kufanya mauaji miaka saba iliopita.
wafungwa sita akiwemo mariamu ambao kwa hakika walikuwa huru waliongozwa na askari mpaka nje gereza ambapo kuna gari liliwasubiri ili wapelekwe mahakamani wakapewe hati zao ili warudi uraiani.
Davidi alifurahi sana baada ya kumuona mariamu akitoka katika lango kubwa la jela . kwa furaha isio kifani davidi alupiga ngumi gurudumu la gari alio liegemea
"asante mungu juhudi zangu zimefanikiwa!!!!!" alisema kimoyo moyo davidi!
wakati wakiendelea kusonga kuelekea ilipokuwa imeegesha gari mariamu aligeuka na kulitazama lile jengo la gerezalililo zungukwa na ukuta mkubwa .alilitaza gereza lile huku kumbu kumbu za mateso na shida alizozipata ndani gereza lile zikijirudia kichwani mwake na picha za sura mbali mbali zikipita kichwani mwake ...
machozi yakawa yanamtoka
"Where is my son" aliongea kwa sauti ya kukwaruza  huku kumbu kumbu za siku aliyo nyan'ganywa na kutenganishwa na mwanae mdogo wa kiume ikimrudia  .
"we songa mbele" askari mmoja alimuamuru mariamu huku akimgusa na kirungu begani..
lakini alikuwa kimya
david alipoona hivyo alipiga hatua mpaka alipo kuwa mariamu na kumgusa begani
"upo huru mariamu tuondoke" alisema davidi
"siwezi... kuondoka bila mwanangu wanirudishie mwanangu" mariamu aliongea huku machozi yakimtoka....
HII NI SIMULIZI ITAYO KUJA KWA JINA LA KISASI NI SEHEMU YA PILI YA I BLAME  MY BODY ....0746206428
unaweza kututembelea simulizimahiri.blogspot.com kupata sumulizi nyingine nyingi

No comments:

Post a Comment

Iblame my body

RIWAYA   : I'BLAME MY BODY ( NAULAUMU MWILI WANGU ) Imezaminiwa na   Simulizimahiri.blogspot.com Mahakama kubwa ya kesi za jina...