Saturday, October 22, 2016

Bonyeza link uisome riwaya hii ya taharuki

Riwaya: The world hates me{dunia ina nichukia)
hali ya mawingu ilitawala katika anga ikiambatana na manyunyu yalio sababishwa na mvua kubwa ilionyesha kwa saa zima iliyopipta, mvua ilionekana kumshtukiza kila mkazi wa mji wa dar es salaam hakuna mtu alieitarajia , mvua hii ilionekana kuwa kero kubwa kwa wakazi wa mtaa wa tandika kwa maana barara nyingi za mataa huo zilijaa mtope yakiambatana namaji. wakazi wachache wa mtaa huo walipitapita wakiwa na miavuli ya o wakielekea madukani na sehemu nyinginezo. maderava wa bodaboda nao waliendelea kupita wakibeba abiria wenye haraka.
Hari ndani ya mtaa watandika haikuonekana kuwa nzuri hata kidogo maana maana polisi walioneka kana kila barabara ya mtaa huo watandika, kila aliye kuwa mkazi waeneo lile alione kushangazwa na uwepo wa polisi hao kwani walionekana kuwa na msako usio kuwa wa kawaida na kila polisi aliku amelowa chepechepe huku bunduki zao zikiwa makini katika mikono yao! Wakazi watandika walizidi kuwa na hofu pale walipo ona gari nne zilizo jaza mapolisi ambao waliruka mmojammoja kutoka kwenye gari na kuigia ndani ya vichochoro vya mtaa huo wa tandika, halikuwa gari moja peke yake bali magari mengi ya police yalindelea kupita kila kona ya mtaa huo wa tandika huku yakiendelea na zoezi hilo la kumwaga police katika vichochoro vya mtaa huo,
hofu ilitanda wakazi wa mtaa huo wa tandika hawa kujua nini kilichokuwa kinaendelea japo baadhi ya watu walibahatisha kwa kusema itakuwa ni oparation ya kusafisha wauza bangi na wauzaji wa madawa ya kulevya, lakin kila mtu alisema la kwake wengiwao waliongea wakiwa kwe vibanda vya chips na wengine wakiwa majumbani mwao wakiwa wamesimama mlangoni na baadhi yao wakiwa vibalazani ,
wakiwa wanaendelea kujiuliza maswali yasiyo kuwa na majibu mara ghafla walishuhudia gari mbili za police zikipita mbele yao zikiwa mwendo mkali zikiwa zimejaza watu waliova nguo za police lakini nguo zao zilikuwa tofauti kidogo, kwa muonekano tu watu waliweza kugundua kwamba ni FFU.!
hofu ikaongezaka !
kabla hawaja tanabahi waliona magari hayo yakiwa mwisho kabisa mwa barara yakifunga brek na kupunguza mwendo na kuanza kukata kona kwa kwa muundo wa kuangaliana kisha madereva wa magari hayao wakakutanisha gari hizo zikawa zime funga barara hiyo, na askali wagari la upande kushoto walionekana kushuka huku wakiwa wameshika vitu kama minyororo, na mmojamoja walianza kushuka huku wakiwa wame tanguliza mbwa wakubwa mbele yao!
kufikia hapo amani ilitoeka kwa wa kazi wa eneo hilo walio kuwa milagoni walifunga milango na kuenda madirashani kuchungulia wakisubiri kuona nini kingetokea, na waliokuwa vibarazani walitafuta nyumba za kuji hifadhi kwa wakati huo ,kuna baadhi walikosa pakwenda wakaamua kutulia walipokuwa wakisubiri tukio ambalo kwa hakika hawakujua ni tukio gani lingetokea kutoka kwa askari wale!
wale askali walioshuka na mbwa walikoki bundiki zao nakuondoka kwa mwendo wa mchamchaka mbwa wao wakiwatangulia kuelekea ndani yamtaa, na askari walibakia kwenye gari la pili wao walishuka nakwenda upande mwingine wa magari hayo kisha wakawa wameangalia upande waliko elekea wanzao wenye mbwa!
mudawote bunduki zao zilikuwa zimekaa makini mikononi mwao.****
kufikia muda huo wa saa 7 police walionekana kila kona ya eneo hilo liliopo karibu kabisa na stend i, kila barabara iliokuwa ina tumika kuingia na kutoka ndani ya stand ya tandika ilifungwa kwa magari ya police na hakuna gari hata moja lilo ruhusiwa kutoka ndani ya stendi hiyo ya tandika!, na watu walipo taka kwenye daradara ili watoke ndani ya stend hyo watembee kwa mguu hawakuruhusiwa na polisi waliokuwa wametanda eneo hilo!
hakuna aliejua kuna nini mpaka kufikia hatua ile!
na wingu yalitanda anga yote ikawa giza na mvua kubwa ikaanza kunyesha.
watu walitawanyika kujikinga na mvua ile, lakini hakuna polisi hata mmoja alie ondoka sehemu alio kuwepo. ****
Mtaani polisi walijaa wakipita huku na huku mvua ikiendelea kuwa nyeshea , polisi wengine waliendelea kusimama sehemu moja ina onekana walia ambiwa wakae sehemu hiyo,
gari moja aina ya rava4 lenye namba za usajili za serekali liingia kwa kasi ya ajabu na kusimama pale kwenye gari ya FFU ilioshusha askali wenye mbwa muda mchache ulio pita, katika gari la rava4 alishuka mwanaume wamakamu alie kuwa amevaa nadhifu nguo za kiraia za heshima, na bila kujali mvua kubwa iliokuwa ikiendelea kunyesha alianza kuelekea kwenye zile gari za FFU na kabla haja zifikia kwenye zile gari askari mmoja alie kuwa hana bunduki lakini alikuwa na bastola kiunoni alionekana kuwa na cheo flani alimkalibia kabla ya fika mtu huyo wa makamu na kumpa heshima kwa kupiga saluti,
"nipe taarifa" alisema mtu wamakamu bila hata salamu!kana kwamba aliona salaamu hiyo haina ummuhimu wakati huo!
" tumefanikiwa kufunga barabara zote zinazo toka na kuingia ndani ya stendi na askari wameenea ndani ya stendi hii.." alijibu askari aliekuwa na bastora kiunoni. mtu wamakamu hakusema kitu ila aliendelea kumuangalia kwa macho yaliyo hitaji taarifa zaidi, na yule askari aliendelea kutoa taarifa....
" ...na ndani ya mtaa tumefanikiwa kufunga barabara si chini ya 12, na askari wame tapakaa karibu robo tatu ya mtaa." askari huyo akawa amesha maliza kutoa taarifa yake, na mtu yule wa makamu aliyevaa nguo za kiraia aliingiza mkono mfukoni na kutoa RADIOCALL, na akabonyeza kitufe flan ,na akaisogeza kalibu ya kinywa chake.
"i.s.p robert naongea" aliongea mtu yule wa makamu.
"report please" sauti upande wapili uliongea.
"tumesha dhibiti upande wa stendi hakuna mtu wala gari litakalo toka nje bila idhini,kwa upande mtaani tumidhibiti karibu robo tatu ya mtaa, nita hitaji kuonana wenyeketi wa mtaa ili watulekeze nyumba za kulala wageni pamoja na vichochoro wanavyo vijua , nita hitaji askali zaidi ili oparesheni ianze" ali maliza i.s.p robert.
"sasa mimi nisha fanya mpago baada ya dakika kumi natano vyombo vyote vya habari vitatangaza juu ya oparesheni ilikuwapa taarifa wakazi watandika ili wawe watulivu wakati opareshen ina endelea, baada ya dakika kumi na nane oparesheni ianze" sauti ya upande wapili uli maliza maelezo.
"ok nime kupata and out" robert aliongea kikakamavu, na akashu mkono wenye radio call na kumgeuka yule askari mwenye bastora kiunoni.
" tuna hitaji mwenyekiti wa eneo hili" alisema robert huku akifuta maji kwenye macho yake alikuwa ameshalowa chapachapa
"hamna tatizo mda mchache uliopita alikuja kuuliza nini kinaendelea, tulimwambia asiondoke ofsin kwake kwa muda huu na alitu onesha ofisi yake ilipo"
"vizuri afande tuma askari wamfuete haraka" alisema na kurudi kwenye gari lake na kuliegemea, dakika kumi badae mwenyeketi wa mtaa aliwasili eneo alilokuwepo robert ****
TAARIFA YA HABIRI YA DHARURA! JAMBAZI ALIYE KUWA AKITAFUTWA MKOANI MWANZA KWA KOSA LA KUUWA POLISI, HUKU AKIHUSISHWA NA MAUJI YA MZAZI WAKE, IMESADIKIKA JAMBA zi HUYO AMEFANIKIWA KUINGIA DAR ES SALAM MTAA WA TANDIKA, TAARIFA ZA HABARI ZINA SEMA YAMETOKEA MAUJI YA WATU WASIO NA HATIA NDANI YA TANDIKA AMBAYO YANASEMEKANA YAME SABISWA NA JAMBAZI HUYO NA KUTOKOMEA NDANI YA YA MTAA WA TANDIKA! POLISI WANA WAOMBA WAKAZI WA ENEO HILO WAWE WATULIVU KIPINDI OPARESHEN IKIENDELEA YA KUMTAFUTA JAMBAZI NDANI YA MTAA HUO MPAKA SASA ASKARI WAMESHAFIKA ENEO LA TUKIO .
radio na tv vyote nchini vili tangaza habari hii ya ghafla kwa upande wa wakazi watandika ni wachache walio isikia maana wakati huo hofu ili tawala mtaa mtaa huo watandika wengi hawa kuwasha vyombo vya habari. ***
mwenyekiti aliwapigia simu wanyekiti wenzake na muda mchache badae walikuwa wamekutana na robert eneo la tukiokila mwenyekiti alieleza mtaa wake ulivyo na nyumba za wageni alizozifahamu katika eneo lake, katika kufuatilia maelezo ya wenyekiti hao, robert na yule askari waliweza kugundua kwamba upande wa magharibi wa mtaa ule ndio eneo pekee ambalo polisi hawa kuwepo kabisa, na upande huo ulionekana kuwa na vichochoro vingi,..
akili na hisia za robert ziliona upande huo wa magharibi huwenda akawa amejihifadhi jambazi waliemtafuta ambae kwa hakika alikuwa tishio, robert alitoa radio call kisha akaisogeza karibu kabisa na kinywa chake
"OPARESHENI IANZE KWA UPANDE WA STENDI KAGUENI KILA GARI FUNGUENI HATA BUTI ZA GARI , NA UPANDE WA MTAANI INGIINE KILA NYUMBA BAR NA GUEST, MSAKO UWENDE KWA KASI KUELEKEA UPANDE WA MAGHARIBI NINA MASHAKA NAPO OVER" alisema robert. "nimekupata sir".
oparesheni ilianza ya kumtafuta jambazi huyo.
baada ya robert kutoa maelekezo taarifa zilisambaa kwa maaskari wote waliokuwa eneo la tukio, namsako ulianza kwa kasi na vurugU kiasi ambacho haikuwahi kutokea, upande wa stend askari waliingia kwenye kila gari lili kuwepo eneo hilo walifungua kila kilicho funguka katika magari hayo , askari wakiwa na picha waliendelea kumuangali kwa makini kila mtu alie kuwa eneo hilo, kuna baadhi ya watu waliwekwa chini ya ulizi walio onekana wamefanana na mtu aliekuwa akitafutwa lakini baada ya kuchunguzwa na kufananishwa ni picha ya mtu huyo waliachiwa, askari waliendelea kutafuta bila kuchoka japokuwa walikuwa wame lowanishwa na mvua iliokuwa ikiendelea kunyesha lakini miili ilikuwa imechemka kwa kuKIMbia huku na kule, stend yote ilikuwa kimya kilicho sikika kwa muda huo ni sauti ya mvua ikiambatana na ngurumo, watu waliokuwepo eneo la stendi walibaki wamesimama pembezoni mwa maduka yaliokuwepo eneo hilo wengine walikuwa wakipigwa mvua wao walikosa pakujikinga na mvua hiyo , polisi baada ya kutafuta sana ndani ya magari waliamua kujigawa wengine waliingia kwenye maduka ya eneo hilo la stendi na watu waliokuwa wame jikinga kwenye maduka wali tolewa nakujiunga na wenzao waliokuwa waki nyeshewa mvua!
*****
robert baada ya kuona msako umeanza yeye alichukuwa askari wanne pamoja na mwenyekiti kwajili ya kumuelekeza eneo la upande wa magharibi, ambapo robert alihisi kuwepo na uwezekano wa mtu aliye kuwa akitafutwa kukimbilia eneo hilo, baada askari wanne pamoja na mwenyekiti kuingia ndani ya gari la robert, gari liliondolewa kwa mwendo usio wakawaida hata kidogo gari liliendeshwa na robert , gari ilikatiza mtaani kwamwendo kasi,
ndani ya gari robert alionekana kuwa na hasira iliyo pitiliza mawazo yake yote yalikuwa ni kumkamata mtu huyo aliekuwa anaanza kuwa tishio nchini, akiwa kama umbali wa hatua stini mbele yake aliona gari lililokuwa katikati ya barabara huku likizungukwa na askari kama wanane ,hapo moyo wake ulilipuka na kuhisi ndani ya gari hilo kutakuwa namtu aliye tafutwa, lakini aliwaona wale polisi hawakuwa na tahadhari hata kidogo maana baadhi yao bunduki zilikuwa zimevaliwa migongoni badala ya kuwa nazo mikononi , hakupunguza mwendo alindelea na speed yake na kuwasogelea askali wale , .
askari walishitushwa na muungurumo wagari na wote wali geuka kwa wakati mmoja walishanga kuiona gari yenye namba za usajili wa serekali, wote walihisi ndani yagari hilo kulikuwa na mkubwa wakazi, wote kijasho kili watoka! na muda huo huo gari ilipiga breki kama hatua tatu mbele kutoka kwa wale askari. na milango yote ilifunguka kwa wakati mmoja na robert alishuka na kutoa bastora yake kiunoni mwake, maaskari alikuwa nao robert ndani ya gari wali weka sawa bunduki zao tayari kwa kuachia risasi, robert alielekeza bastola yake usawa wa gari lile na askari alio kuwa nao ndani yagari walilizunguka gari hilo huku wakielekeza siraha za kwenye gari hilo " NANI YUMO NDANI YA GARI ?" robert ali wauliza wale askari alio wakuta eneo hilo.
* * * *
moses akiwa nyumbani kwake alishangazwa na taarifa ya habari alio kuwa akiendelea kuangalia, macho yake haya kutaka kuamini kwamba jambazi aliekuwa akitafutwa mkoani mwanza sasa yummo ndani ya jiji la dar es salaam. mawazo yake yalikatishwa na mlio wa simu iliyo kuwa mfukoni mwake , aliitoa na kuangalia nani aliekuwa akipiga mara ghafla alikunja uso! kwa sekunde kadhaa alikuwa amesha mtambua mpigaji! alipokea kwa unyonge . " habari afande!" moses aliongea baada ya kupokea.
"uko wapi na sitaki uniambie kwamba uja sikia juu ya tukio linalo endelea tandika" sauti ya upande wapili ilifoka na kumnyong'onyeza moses!
"hapana afande taarifa ndo nimeipata muda sio mrefu" moses aliongea kwa unyonge na hofu,
" baada ya kupata taarifa ukasubiri nikupigiesimu"
"hapana afande"
"sasa sikia mauji yamesha tokea mauaji tangu ABDUL awasili jijini, nenda haraka tandika katika eneo yapotokea mauji kafanye utalatibu wa maiti kupelekwa hospitali? taarifa zote unipe mimi na so mtu mwingine," na simu ikakatwa.
moses alinuka haraka haraka na kuingi chumbani mwake akachukua koti lake jeusi na kulivaa akachukua grove na bastora yake, na kutoka nje bila kuzima tv yake akatoka nje akapanda juu ya pikipiki yenye namba za usajili wa serekari na safari ikaanza.
****
"ndio afande..." alijibu mmoja wa wale askari walioulizwa na robert,
"It's ABDUL!?" robert alimkatisha kabla aja malizia yule askari,
" hapana ila tuna mtilia shaka " askari alijibu kwa kigugumizi!
"kivipi hemu mtoe mlete haraka nje" alisema robert huku akishangazwa na kigugumizi cha yule askari ,
askari mmoja alifungua mlango wagari na kumtoa mzee mweupe mnene, robert alishangaa na hapo aligundua kwamba wale askari walikuwa wanataka rushwa kutoka kwa mzee yule na ndomaana walikuwa wana wasisi mwingi,,ali wageukia wale askari akiwa amekunja uso wake,
"mnamtilia mashaka yapi babu kama huyu mlikuwa mnataka atoe rushwa sio?" aliuliza robert huku aki waangalia mmoja baada ya mwingine.
"hapana afande tusamehe...."alisema yule askari .
"nyie yaani mnaacha kazi muhimu mnaanza kuomba rushwa, au mna ona hii kazi haina umuhimu?" kimya!
"nasema hivi katika hii oparashen nitafukuzisha kazi askari wengi!" alisema huku akirudi ndani ya gari lake na askari wake aliokuwa nao na na mwenyekiti aliekuwa pembeni kidogo walimfuata wakaingia ,
"toeni hilo gari haraka " alisema na baada ya gari kutolewa ali washa gari na kuendelea na safari..
***
kundi la askari kumi na moja wakiwa na gari lao , katika kuulizia ulizia walikutana na kijana aliekuwa na mfuko uliojaa makopo, ni kijana huyu baada ya kudadisiwa na polisi alisema dakika kama kumi zilizopita alikutana na mtu alie onekana kuwa na wasiwasi , polisi mmoja alitoa picha na kumuonesha kijana huyo , kijana alisema ni yeye alie muona aliedakika chache zilizo pita
"...ndio yeye afande lakini ye amevaa miwani ya macho na suti nyeusi, piteni huu uchochoro niliotokea mimi barabara ya tano ndo nilipo kutana nae"alisema kijana huyo muogota makopo huku akielekeza kwa ishara.
askari wali jigawa wanne waliingie kwenye gari hiyo ya polisi, na sita walifuata huo uchochoro, na gari ilindolewa kwa kasi ikizunguka upande wa pili alipokuwepo mtu walie mtafuta.
****
kijana mrefu kiasi mweupe aliekuwa amevaa miwani ya macho mikono yake ikiwa ndani ya mifuko ya koti la suti aliyokuwa ameivaa, na alikuwa amelowa chepechepe, kijana huyo alitembe kwa mwendo wa kasi ajabu, macho yake haya kutilia yale angaza huku na kule alitembea kwa kuchechemea alionekana ku choka sana , alipita kwenye matope bila kujali na ni huyu ndie alie kutana na yule muokota makopo muda mchache uliopita!
****
polisi walio fuata uchochoroni walitembea kwa kasi ya ajabu na kwa umakini wa hari ya juu, ndani ya dakika kumi walikuwa walikuwa wamefikia barabara ya nane ,na kama hatua tisini mbele yao walimuona mtu alikuwa akitembea kwa kasi akisunta mguu mmoja,alikuwa amevaa suti nyeusi waliendelea kumkalibia kwa kasi kubwa huku wakiwa makini asi waone.
****
gari lilo ondoka na askari watano akiwemo dreva lili zunguka mtaa kwa kasi na kuufuata upande walioelekezwa , gari lipopita kama barabara kumi na moja dreva alikata kona na kushika barabara ya kumi na mbili, dreva alikuwa na lengo la dreva ilikuwa kusimamisha gari ili apige simu na kutoa taarifa ili askari waongezwe katika eneo hilo., akiwa mwendo wa kasi mara ghafla mbele yake hatua kama arobaini aliona mtu alievaa suti akiwa anataka kuvuka barara!
****
yule mtu aliekuwa akifuatwa nyuma na askari bila yeye mwenyewe kujua alitembea kwa haraka akisunta ili aivuke barabara alioiona mbele yake, kutokana na waswasi na mawazo pamoja na kelele ya mvua iliyo piga kwenye bati za nyumba za mitaa hiyo, huyo kijana hakusikia kabisa muungurumo wa gari la polisi lilokuwa likija katika barabara aliyokuwa akiiwahi ili avuke,
alipoingia tu barabarani mikono yake ikiwa bado kwenye mifuko wakoti ndipo kwa kihorokikubwa macho yake yaliishuhudia gari ya polisi ikija kwa kasi alipo simama!
haya mtu alie onekana na muogota makopo yupo katikati ya barabara na gari la polisi inakuja kwa kasi alipo simama na polisi wa sita wapo nyuma yake bila yeye kujua je? nini kitatokea?
jina ABDULI TUMEWEZA KULISIKIA MARA MBILI LIKITAJWA JE? ABDUL NI NANI ?
tukutane kesho tupate kugundua mengi zaidi.
Itaendelea...... like na kushare kesho iendelee
MAONI YAKO NIMUHIMU

No comments:

Post a Comment

Iblame my body

RIWAYA   : I'BLAME MY BODY ( NAULAUMU MWILI WANGU ) Imezaminiwa na   Simulizimahiri.blogspot.com Mahakama kubwa ya kesi za jina...