Friday, October 21, 2016

Sophia

mtunzi: iddi siraji
SOPHIA
Bugando mwanza .
Asilimia kubwa ya wagonjwa walikuwa wamisha pitiwa na usingizi huku wengine wakiwa wamejituliza vitandani mwao kana kwamba wamelala lakini walikuwa macho wakiungulia maumivu ya maradhi yao yalio endelea kuwa sumbua  na kuwaweka kwenye hosptali ile ya bugando.
kwa ufupi usiku ule hosptal ilikuwa kimya, pirika za hapa na pale za wahudumu na manesi zikiendelea kwa utulivu mkubwa na ukimya wa hali yajuu..
wodi nambari H 109 ilikuwa ni wodi ya private huku ndani yake akiwemo mgonjwa aliefahamika kwa jina la Sophia .
muda wote usiku ule sophia alikuwa amekaa katika kitanda chake huku mbele yake kukiwa na meza ndogo ikiwa imebeba barua ilio kuwa ikamalizikia kuandikwa na sophia..
sophia aliendelea kuandika ile barua huku machozi yakimtiririka kwa hudhuni kubwa na simanzi ilio kuwa imewaka makazi ndani ya moyo wake.
tayari alikuwa amesha andika ukrasa wa kwanza na sasa alikuwa anamalizia ukrasa wapili na chini kabisa ya barua aliandika kwa maandishi makubwa (GIKA NISAMEHE SANA KWA MAAMUZI NILIYO YACHUKUA) kisha akailaza karamu yake juu ya barua yake  na kwa mkono wake wa kulia akaichumoa sindano ya dripu alio tundikiwa na kufanya damu itiririke kwenye mkono wake kutokea kwenye mshipa aliochomoa ile sindano ,hakuwa na muda wa kuitazama ile damu kwani wakati wake wa kuishi hapa duniani ulikuwa umefikia mwisho kwani sophia alikuwa na maamuzi ya kujiua usiku ule..
"haina maana ya kuendelea kuishi mabaya nilio wahi kumfanyia Gika lakini leo ndio kawa msaada mkubwa katika maisha yangu .. wako wapi? wafanya biashara wenzangu wapo marafiki zangu wa karibu niliokuwa nao katika starehe zote za huu mji wa mwanza  yupo wapi mpenzi wangu nilivuma nae kwenye magazeti kwa skendo za kwa sophia natoka na msanii chipkizi wa mziki wa bongo fleva.. yeye si ndie nilie muona anafaa na kumtelekeza gika nakuamua kumfuata yeye alie nifanya nitambulike kwenye media na magazeti.." aliongea kwa sauti ndogo ilio ambatana na kilio cha chini chini huku nafsi yake ikimsuta kwa mabaya alio mfanyia gika
"ok yote yamepita nikisha pona itanilazimu nikaishi kwa gika kwenye nyumba yake ambayo nilisha wahi kuitukana na kuita ni banda la njiwa huku nikijivunia jumba langu ambalo mpaka sasa imeshapigwa mnanda..
nitamtazama vipi gika nikiwa katika nyumba yake?
na vipi waandishi  wa habari wakini tafuta kwa mahojiano?
hapana siwezi kuishi siwezi kuishi tena"  alisema sophia kupiga hatua emegency door akiwa na lengo la kutoka nje ili ajitupe chini kutoka ghorofha namba 9 aliyo kuwepo .. lakini kabla hajafungua alisikia mlio kutoka kwenye simu yake aliyo iacha kitandani moyo ukamsukuma kuiangalia ile simu na alipo rudi kuiangalia alikuta jina gika kwenye kioo cha simu yake,
gika alikuwa anampigia!
ndoge zito lika mkaba kooni akashindwa hata kuipokea simu  kilio cha sauti kikataka kumtoka akijikaza na kuya ruhusu machozi yatiririke..
simu ikakata na hapo sophia akapiga hatua kwenda kwenye ule mlango aufungue atoke nje kufanya maamuzi ambayo aliyaona ni sahihi kwake ...
simu ilianza kuita lakini safari hii sophia hakurudi nyuma  alikwenda kuufungua ule mlango wadharula akajitupe ......
hii ni simulizi fupi tukutane wakati mwingine tupate kujua hatima ya sophia...

No comments:

Post a Comment

Iblame my body

RIWAYA   : I'BLAME MY BODY ( NAULAUMU MWILI WANGU ) Imezaminiwa na   Simulizimahiri.blogspot.com Mahakama kubwa ya kesi za jina...