Wednesday, August 2, 2017

Iblame my body

RIWAYA  : I'BLAME MY BODY (NAULAUMU MWILI WANGU)

Imezaminiwa na  Simulizimahiri.blogspot.com

Mahakama kubwa ya kesi za jinai
jijini dar es salaam ilikuwa imefuruka
watu walio kuwa wamekaa kwenye
viti vya mahakama huku kila mmoja
macho yake yakiwa yameangalia
mbele palipo kuwa na hakimu
pamoja na mawakiri na polisi
aliekuwa pembeni kidogo ya kizimba
alicho kuwa amesimama msichana
alie tawaliwa na majozi huku
machozi yakizidi kutiririka kutoka
kwenye macho ya msichana huyu .
ndani ya mahakama hii watu wengi
waliokuwa humo walimtizama
msichana aliekuwa kizimbani kwa
macho yaliyo onesha dhahiri kuwa
walimchukia msichana huyo!.
***
nje ya mahakama polisi walikuwa na
kazi nzito ya kuzuia raia wengi
waliokuwa na mabango yaliyo
andikwa maandishi yaliyo andikwa
"MARIAMU HUKUMU YA KIFUNGO
CHA MAISHA HAIMTOSHI
AHUKUMIWE KIFO MARIAMU
ANYONGWE!", watu walikuwa niwengi
huku wakilalamika kuwa msichana
anaitwa mariamu kesi yake ina
cheleweshwa ,
ndani ya kundi hili la watu waliokuwa
na mabango kuna baadhi ya watu
walikuwa wamepanga kama mariamu
asipo hukumiwa siku hiyo, wakati
akitolewa wamvamie na kumponda
mawe ikiwezekana wamuue! kwani
waliona kama mahakama
ilimchelewesha mtu ambae kwa
asilimia kubwa alichukiwa na watu
wengi katika jiji la dar es salaam.
ndani ya mahakama hii kuna watu
wawili bibi na bwana wenye asili ya
kiarabu waliokuwa wamekaa kwenye
benchi la mbele kabisa kwenye
mahakama hiyo.
watu hawa walikuwa kwenye simanzi
kubwa huku mwanamke akiwa
anashindwa kabisa kuya zuia
machozi yalio ambatana na kilio cha
kwikwi!
msichana mariamu mwenye nywele
zenye asili ya kiarabu, huku ngozi ya
mwili wake ikionekana kupaushwa na
matatizo aliyo kuwa nayo muda ule,
sura ya msichana huyu wazi
ilionekana kuwa ya urembo ila
kwasasa urembo ulikuwa umeanza
kujivua kwa msichana huyu
mariamu,
sura ya msicha huyu ili shabihiana
kabisa na hawa watu wawili wa
makamu wenye asili ya kiarabu, ni
wazi mariamu na watu hawa wiwili
walikuwa na uhusiano mkubwa!
Mariamu alikuwa katika majonzi
makubwa yaliyo mfanya ashindwe
kabisa kuzuia machozi kwenye macho
yake pamoja na kilio cha masikitiko
ambacho kilihuzunisha watu
wachache wasio fikaka kumi ,huku
umati uliojaa ukimuona kama ana
waektia!
uso wamaliamu ulikuwa unawekundu
ulio sababishwa na kulia sana ,
mariamu alitembeza macho
mahakama nzima huku akikutana na
macho mengi yaliyo mtizama kwa
hasira , mariamu akajikaza na
kulazimisha macho yake kutazama
walipokuwa wale bibi na bwana
wenye asili ya kiarabu ambao ni
wazazi wake!
na ndipo hapo akashuhudia jinsi
mama yake akilia na hapo mariamu
akashindwa kabisa kujuzuia,kilio cha
sauti ya kukwaruza kikamtoka
maraiamu huku akiwa na majuto
mengi.
mariamu aliendelea kulia huku
akijifuta machozi kwa gauni lake aina
ya dela na , mara mariamu
alipunguza kulia huku akijitahidi
anyamaze kabisa kwani alikuwa
amesha ona harakati za mawakili
wakipita na mafaili huku wengine
wakienda kumkabidhi baadhi ya
mafaili .
harakati za mawakili kupita pita
ziliendelea kwa muda na mara
zilikoma na ukimya na utulivu
vikatawala mahakama ile huku na
watu wote wakawa makini kusikiliza
kesi ile.
kesi ilikuwa imeanzwa kusomwa!
hakimu alimsomea mashtaka mazito
yalio muhusu mariamu ,
baada ya hakimu kumaliza kusoma
mashtaka yale ikafuatia majibizano
ya mawakili wa pande mbili tofauti.
david mwakyema yeye alikuwa ni
wakiri pekee alie kuwa amebaki
akimtetea mteja wake mariamu,
wakiri huyu alikuwa ni mmoja wa
mawakiri watatu walio ahidiwa
kulipwa pesa watakayo ihitaji kutoka
kwa baba yake mariamu, ili mradi
mariamu asikutwe na hukumu
mbaya.
lakini mpaka muda huu alikuwa
amebakia wakiri david na wale
mawakiri wengine wawili walikuwa
wamejivua kwenye kesi ya kumtetea
mariamu, mawakiri hawa walikuwa
wameamua kujivua kwenye kesi
baada ya kugundua ile kesi ilikuwa ni
ngumu na kamwe wasinge weza
kumsaidia mariamu kutoka kwenye
hukumu ya kifungo cha maisha kama
sio kifo .
ni wakiri david pekee aliebakia
kwenye kesi hii ambayo
iliwaogopesha mawakiri wengi
kumtetea mariamu,
mawakiri wenzake na david
walimshangaa sana david kujiingiza
kwenye kesi ambayo ilionekana wazi
ni kesi ya kushindwa, lakini yeye
david alikuwa king'ang'anizi kwenye
kesi hii yenye hujuma nzito juu ya
mariamu.
kwa upande wake david alijua kabisa
kuwa kesi aliyokuwa anaisimamia
ilikuwa ngumu, na tena kulikuwa
kuna asilimia kbwa ya vielelezo
vinayo onesha kua mariamu lazima
apate hukumu kubwa.
wakiri david kuna kitu kilimsukuma
mpaka kukubali kuwa kwenye kesi hii
nzito!
...
Majibishano yaliendelea kwa muda
kati ya wakiri david na mawakiri wa
upande wa mlalamikaji , huku dalili
zote zikionesha kuwa kesi ile ilikuwa
ngumu kwa mariamu.
hata david alilijua lile lakini alikuwa
hana jinsi,
mashahidi wa upande wa
mlalamikaji walipandishwa kizimbani
na kushuhudia tuhuma za mariamu
huku wakitoa ushahidi wao ambao
ulizidi kumkandamiza mariamu
ambae hakuwa na shahidi hata
mmoja wa kumtetea zaidi ya wakiri
dav,
kama haitoshi timu ya makachero
(wapelelezi) ilifika na kutoa ushahidi
wao na vielelezo vingi vilivyo
thibitisha kuwa mariamu ni
mtuhumiwa tena aliefanya kosa kwa
kukusudia.
ama hakika kesi. ilikuwa ngumu kwa
mariamu!
"mariamu una cha kuithibitishia
mahakama na kupinga hizi tuhuma
juu yako" swali kutoka kwa wakiri wa
upande wa ulalamikaji alimuuliza
mariamu.
mwili wa mariamu ukaingiwa ganzi
mariamu akahisi kupigwa shoti, papi
za midomo yake zikamtetemeka,
akahisi donge likimkaba kooni.
mariamu akashindwa ajibu jibu gani
kwani ushahidi mwingi wa
kumkandamiza ulikuwa mbele yake .
mariamu akainua uso wake na
kutembeza macho yake , mariamu
akamtazama wakiri david alie kuwa
akimtetea, na mara macho ya
mariamu yakatua kwenye timu ya
wapelelezi walio kuwa wameleta
ushahidi mzito wa kumkandamiza,
mariamu akamwangalia mpelelezi
mmoja kwa macho ya kutoamini
anacho kiona, mariamu alionekana
kumfahamu mmoja wa makachero
wale.
mariamu akatazama watu wote walio
kuwa wakimtazama kwa mtazamo wa
ubaya,akawatazama mashahindi
walio kuja kumkandamiza kwenye
kesi hii, mariamu akajua wazi ile kesi
ilikuwa imemuangukia na kamwe
asinge jinasua kwenye wimbi lile.
"unaona muheshimiwa mariamu
amekaa kimya inamaanisha hana cha
kujitetea.. Hakimu mtuhumiwa hana
cha kujibu inasubiriwa hukumu yako"
alizungumza wakiri,
Kufikia hapo mariamu alikuwa
amejithibitishia hukumu yake,
Moyo wa mariamu ulikuwa kwenye
majuto makubwa mno, na kichwa
chake kilizingilwa na kumbu kumbu
za mambo aliyo yafanya mpaka
kufika hapo kwenye wimbi la
majanga,......

2


2
mariamu alikuwa mtoto peke wa
familia ya mzee rakhimu, familia
ambayo ilikuwa na uwezo mkubwa
wa kifedha. mzee rakhimu na mke
wake walikuwa na asili ya kiarabu
huku ngozi za miili yao zikiwa zina
kauesi ka mbali. na hata mtoto wao
mariamu nae alikuwa mtoto mzuri
mwenye nywere za kiarabu na uesi
wa mbali uliofanya mtoto huyu
kusifiwa kwa uzuri tangu akiwa
mtoto. rakhimu na mama mariamu
walimpenda sana kwani ndo alikuwa
mtoto wao wa pekee, wazazi wa
mariamu walimpeleka mtoto wao
kwenye shule za kulipia ili aweze
kupata elimu bora itakayo kuwa
nguzo yake maishani mwake,
kadri mariamu alivyo zidi kukua
ndivyo uzuri wake ulivyo zidi
kuonekana huku baadhi ya watu
wengi wakitabari kuwa msichana
huyo atakuja kuwa tishio na kiboko
ya wavulana,
mariamu tangu akiwa shule ya msingi
alikuwa na maadili hakuwa na
maringo, vitu hivi vikazidi kumfanya
mariamu azidi kupendwa na kila
mwalimu shuleni na hata wanafunzi
wenzake huku sifa zakuwa yeye
nimzuri zikimuandama kila kukicha,
mariamu alipoingia darasa la saba
akiwa ameanza kukua ndipo umbo
zuri lilianza kuonekana dhahiri
kwenye mwili wa mschana huyu, kwa
mara ya kwanza akaanza kuwatia
watu tamaa ya kumtamani mpaka
baadhi ya walimu waliokuwa na akiri
za uasherati wakawa wakimtamani
huku wengi wao wakijifanya kuweka
ukaribu nae kwa kisingizio cha
kumpa vijikazi vidogo vidogo kama
kusaidia kusahisha mitihani n.k
mariamu akijikuta akianza kupata
usumbufu mkubwa kutoka kwa
wanafunzi wenzake wakimtaka
kimwili huku wengi wakiwa wanatoka
kwenye familia zenye uwezo kama
yeye.
kutokana na maadili aliyokuwa nayo
mariamu hakusita kwenda kushtaki
kwa mwalimu mkuu kuwa
alisumbuliwa na vijana. kitu
ambacho kilipelekea vijana hao
kupata adhabu kutoka kwa walimu
ambao baadhi yao walikuwemo walio
mtamani mariamu .
**robbin na david walikuwa ni vijana
marafiki ambao urafiki wao ulitokea
nyumbani mpaka shuleni , vijana
hawa walisoma shule moja na darasa
moja alilo somea mariamu.
robbin na david na wao walikuwa
nimiongoni mwa vijana walio tamani
sana kumpata mariamu huku kila
pakicha vijana hawa wakitambiana
kila mmoja akidai yeye ndie
atampata mariamu.
vijana hawa wao kidogo walifanikiwa
kuwa na ukaribu na mariamu kupita
vijana wengine, hii ili sababishwa na
mazingira yaliyo kuwepo kati ya
vijana hawa na mariamu, mtaa
alioishi mariamu nyumbani kwao
hapakuwa mbali sana na walipo ishi
marafiki hawa wawili waliokuwa
wanaishi kwenye nyumba za kota!
basi ya shule kila siku ilikuja
kuwachukua na kuwapeleka shule na
kuwa rudisha . sehemu
waliposhushiwa vijana hawa ndipo
alipokuwa anashukia msichana
mariamu na hata njia ya kurudia
nyumbani ilikuwa moja na vijana
hawa . vijana hawa walijitahidi kila
siku wakati wakurudi nyumbani na
kweli walifanikiwa! mara nyingi
walishuka pamoja na kuongozana na
mariamu .
robbin ndo alikuwa wa kwanza
kuvunja ukimya kwa mariamu
kumuuliza vimaswali visivyo kuwa na
kichwa wala miguu huku david akiwa
kama msindikizaji na mwitikiaji huku
dalili zote za kuzidiwa ucheshi na
robbin zikidhihirika .
robbin yeye alikuwa nimcheshi
kupita kiasi na hakuwa na aibu usoni
kitu ambacho kilamsaidia kumkabili
mariamu, na hata mariamu akawa
amependa sana ucheshi wa robbin
na kuzidi kuwa karibu nae kuliko
david! david yeye alikuwa na aibu
pamoja na uoga wa kuhimili kuongea
na mariamu kitu ambacho kilimfanya
asiwe na ukaribu na mariamu kama
kama ilivyo kwa robbin. kuna wakati
david alijaribu kwenda kuongea na
mariamu akiwa peke yake lakini
hakupata ushirikiano kutoka kwa
mariamu kama ilivyo kwa robbin.
tayari robbin alishafanikisha kuwa na
ukaribu na mariamu japo alikuwa
bado hajatamka kuwa anampenda,
ukaribu wa mariamu na robbin
ukaanza kujenga picha tofauti kwa
wanafunzi wenzao,na robbin akizidi
kujitamba kwa rafiki zake kuwa yeye
na mariamu wana uhusiano ya
kimapenzi, hakuna alie bisha kwani
ukaribu wa mariamu na robbin
ulileta maana hiyo,
kwa mara ya kwanza david aliingiwa
na wivu wa kimapenzi na chuki
kubwa juu ya rafiki yake mpendwa
robbin, david alijua fika hakuwa na
chake kwa mariamu kwani david
mara kadhaa alimfuata mariamu
akiwa peke yake na kujaribu
kumwambia anampenda lakini
mariamu alifoka na kumuambia dav
kuwa akiendelea kumsumbua
ataenda kusema kwa mwalimu mkuu,
mpaka hapo david akajua tayari
mariamu mahusiano na robbin na
ndomaana mariamu anakuwa mkali.
kitu ambacho david hakujua ni
kwamba robbin alikuwa rafiki wa
kawaida tu kwa mariamu na sio
mpenzi.
taratibu urafiki wa vijana hawa
robbin na david ambao waliishi
kwenye kota za serekari na baba zao
walikuwa ni polisi waliotofautiana
vyeo ukaanza kuzoroteshwa na wivu
wa kimapenzi uliojengwa na david.
**** baada ya kufanya mtihani wa
darasa la saba na matokeo kutoka
ilikuwa ni wakati wa wazazi wenye
uwezo kuwatafutia watoto wao shule
zenye maadili na elimu na elimu
bora, wazazi wa mariamu
walimtafutie shule mariamu ya
kulipia ili apate elimu bora , shule
ilikuwa ina mabweni lakini wazazi wa
mariamu waliamua mtoto wao awe
anaenda shule na kurudi nyumbani
kwani waliamini mabweni
yanachangia mmomonyoko wa
maadili hasa pale shule inapokuwa
haina ulinzi wa kutosha.
robbin nae alibahatika kupelekwa
shule aliyo pelekwa mariamu! hii
ikazidi kumpa faraja robbin kuwa
lazima angempata mariamu ambae
kwa muda huu walikuwa na urafiki
wa hari ya juu!
bahati mbaya ilikuwa imemuangukia
david! maskini ya mungu david
alikuwa amepelekwa shule tofauti na
aliyo pelekwa mariamu na robbin ,
na kibaya wazazi wake walimpeleka
shule ya boarding yaani david akawa
amehamia shuleni na anarudi
nyumbana kwa msimu.
moyo david ulimuuma sana
kupelekwa shule tofauti na mariamu,
japo alikuwa ameshakataliwa alikuwa
hajakata tamaa lakini kwa pigo hili
lilimkatisha tamaa kijana huyu na
kibaya zaidi robbin alikuwa
amepelekwa shule moja na mariamu!
david akabaki ma simanzi yake .
shuleni urafiki wa robbin na
mariamu ulizidi kushamali huku wote
wakiwa wanaenda shule na kurudi
nyumbani pamoja. robbin akaona
ule ndo ulikuwa muda sahihi wa yeye
kufanya maamuzi yaliyokuwa sahihi,
robbin alikuwa amepanga
kumwambia mariamu 'bora ni
mwambie mapema ,shule yenye
imejaa mabraza men wakiarabu
wengi, asije kuchukuliwa na waarabu
wenzake' alijisemea robbin, na siku
hiyo robbin jioni akiwa anarudi
nyumbani na mariamu aliamua
afunguke kwa mariamu!
tofauti kabisa na matarajio ya robbin
kutoka kwa mariamu! mariamu
alikuwa amemkataa robbin. robbin
alifikiri urafiki wa yeye na mariamu
ungemsaidia kumpata mariamu
kirahisi lakini haikuwa hivyo "sikia
robbin mi staki kabisa huo upuuzi
kama ni urafiki ni bora ufe"maneno
makali kutoka kwa mariamu yali
uralua moyo wa robbin, ni akheri
mariamu angesema atamfikiria
robbin lakini haikuwa hivyo, robbin
alijitahidi alivyoweza lakini ikawa
kana kwamba ana uweka hatarini
urafiki wake na mariamu , robbin
akajikuta amefeli kwa mtu ambae
alimpenda kwa dhati tangu wakiwa
wadogo, robbin akaona ni bora
asitishe mikakati yake kwani alihisi
kama ataendelea kumng'ang'aniza
mariamu kulikuwa kuna hatari ya
urafiki waliokuwa nao kupotea.
maisha ya shule yakaendelea huku
urafiki wa mariamu na robbin ukiwa
unazorota kwa kiasi , robbin alikuwa
ameupoteza urafiki wa yeye na david
na sasa kulikuwa kuna hatari ya
urafiki wake na marianu kupotea.
**** mariamu akiwa kidato cha tatu
akawa mdada anaejitambua urembo
ulio kithiri ukadhirika kwa mariamu
huku kero kubwa ya kutongozwa na
wanafunzi wenzake ikipita kiasi,
waalimu wakiume hawakuwa nyuma
kumfuata mariamu kwa gharama
yoyote, mariamu alikataa kabisa
huku akitoa vitisho vikali kwa walimu
walio mtongoza kuwaambia
angeenda kumuambia baba yake na
baba yake angeenda kwenye ngazi za
elimu na kuwafukuzisha kazi!
sifa kemu kemu alizopata mariamu
na kwa jinsi alivyo fuatwa sana na
wanafunzi wenzake pamoja na
baadhi ya walimu, vitu hivi
vilimtosha kumjulisha mariamu kuwa
yeye ni mzuri na hakukuwa na mzuri
mwingine shulen zaidi yake yeye!
mariamu akatazama baadhi ya rafiki
zake wa kike mariamu akagundua
tofauti kubwa iliyo kuwepo baina
yake na rafiki zake ambao wote
hawakuwa wazuri kama yeye ambao
wengi walikuwa wameanzisha
mazoea nae, mawazo ya mariamu
yakamwambia kuwa wale hawa kuwa
type yake na walikuwa
wanajipendekeza sababu yeye ni
mzuri , "najizalilisha kuwa na watu
kama hawa..inafaa niwe na watu
matawi ya juu sio kuwa na walu walu
kama hawa" haya ndo mawazo yaliyo
muingia mariamu na yeye bila
kujiuliza aliyaruhusu na kuyapa kipa
umbele. maskini mariamu hakujua
mbaya na mzuri wote wameubwa.
rebeca, enjoy na amina walikuwa ni
waschana waliosoma kwenye shule
hii aliyo kuwa anasoma mariamu .
waschana hawa walikuwa ni wazuri
wote kana kwamba walijichagua,
hawa kuwa na mazoea mazoea sana
na wanafunzi wenzao , mara zote
walikuwa wakitembea pamoja na
hata kujisomea , walikuwa na
maringo yaliyo kithiri kitu ambacho
kilicho sababisha wanafunzi wasi
wazoee , Ni wavulana wachache sana
walio kuwa na ukaribu na waschana
tena wavulana hawa walionekana ni
vijana wenye pesa .
mariamu aliwafahamu waschana
hawa na sasa aliwaona kama wale
kidogo ingekuwa ni aina yake kwani
walikuwa warembo na kwa mtazamo
wa haraka walikuwa ni masista du,
mariamu akaamua aweke urafiki na
kundi la waschana hawa .
ghafla sana mariamu alibadiri
muelekeo wake na kupunguza
uhusiano wa urafiki na rafiki wote
ambao alisema sio type yake, hata
kwa robbin pia urafiki ulishuka
ikabakia salamu pekee kitu ambacho
kilimshangaza robbin, mariamu
akawa na urafiki mkubwa na hili
kundi la waschana watatu.
kitu ambacho mariamu hakujua
nikwamba hawa waschana hawa
kuwa wazuri hata kidogo.. waschana
hawa walikuwa na sifa zote za kuitwa
maraya walitumia uzuri wao
kutembea na wavulana wenye pesa
na hata watu wenye umri mkubwa
walio lingana na baba zao. umaraya
waliufanyia maeneo ya mbali .
nyumbani kwao na shuleni
hawakujulikana hiyo tabia yao,
maramu alikuwa ni kama kondoo alie
jiingiza kwenye kundi la mbwa
mwitu!
..

  3

maisha ya shule yaliendelea huku
mariamu akiwa bado yupo kwenye
giza kubwa la kuto kujua tabia za
rafiki zake.
yeye mariamu alijua ustarabu na
maadili aliyokuwa nayo yeye ndivyo
walivyo kuwa kina rebeca, mara kwa
mara mariamu alifuatwa na baadhi
ya rafiki wa kina rebeca wakimtaka
kwa mahusiano lakini mariamu
aliendelea na msimamo wake wa
kukataa kujiingiza kwenye
mahusiano kitu ambacho kina rebeca
kiliwaudhi wakaamua waanze
kumshawishi mariamu,
"mariamu ujue wewe ni mzuri tena
kutupita sisi?.." ilikuwa ni sauti ya
rebeca akimwambia mariamu wakiwa
wamekaa peke yao na ulikuwa muda
wa mapumziko
"why unasema hivyo best" mariamu
aliuliza kwa kustaajabu
"ni kweli we ni mzuri zaidi yetu bt
tunashangaa huutendei haki uzuri
wako" rebeca aliongea kwa kusisitiza
"kivipi mbona sikuelewi" mariamu
aliuliza safari hii akiwa na taharuki
"sisi ndo hatukuelewi wewe
mwenzetu ...mungu amekupa kila
kitu kwenye mwili wako but unakaa
kujibana bana wewe ni shule na
nyumbani tu, hauna sehemu hata
moja unayo kwendaga kuenjoy sio
siri hauji tendei haki, wewe
umeshakua bado unajibanabana
jiachie mtoto usije ukaitwa mama
majuba" rebeca aliongea kana
kwamba alikuwa anatoa somo kwa
mariamu ,
"wewe muda huu ulitakiwa uwe na
boy friend ,achilia bali boy friend
unatakiwa uwe una enjoy, kwanza
leo ijumaa keshekutwa inatakiwa
tutoke ukauone mji!" rebeca alizidi
kumlaghai mariamu.
mariamu alikataa kabisa ushauri wa
rafiki zake wale hasa ukizingatia
mama yake kila siku alimuhusia na
kumkataza asijihusishe na
mahusiano katika umri huu.
Siku zote maneno huwa ni suma
maneno yanaua zaidi ya upanga!
Kina rebeca walifanikiwa
kumshawishi mariamu, mariamu
akawa amewakubalia kina rebeca juu
ya swala la kuwa wanatoka siku ya
weekend lakini mariamu alisema
hata jihusisha na swala la uhusiano!
Siku ya juma mosi ilifika na mariamu
akawa ame muaga mama yake kuwa
juma pili ataenda kujisomea shuleni
kwao na wanafunzi wa boarding na
wazazi wake wakamkubalia bila
wasiwasi.
Juma pili iyo mariamu kwa mara ya
kwanza alienda kutembezwa bichi na
kina rebeca,
Usafiri walio tumia ilikuwa ni gari
aina ya noah iliyo endeshwa na
kijana aliekuwa mpenzi wa rebeca ,
na walipo fika bichi walikutana na
vijana wawili waliokuwa gari moja
vijana hawa walikuwa ni wapenzi wa
enjoy na amina , vijana hawa wote
walionekana kuwa na pesa zilizo
wapa kiburi akina rebeca,
Ni mariamu peke yake ambae
hakuwa na mpenzi siku ile kitu
ambacho kilimfanya awe mpweke
japo wali enjoy vy kutosha!
Mtu ukionja asali kamwe huwezi
acha!
mariamu alijikuta akienjoy sana na
wale rafiki zake japo yeye hakuwa na
mpenzi kama wenzake,
haya ndo yakawa mazoea ya
mariamu kila jumapili aliaga
myumbani kwao anaenda kujisomea
na wanafunzi wa bweni badala yake
aliwapitia rafiki zake na kwenda kula
nao maisha na hii ndo ikawa desturi
ya mariamu.
***
ilikuwa ni juma pili tulivu kijana
aliejulikana kwa jina la moody
alikuwa amekaa ufukweni mwa
beach yenye hadhi,siku hii mood
alikuwa anaisubiria kwa hamu na
sasa aliwasubiri kina rebeca ili
ajihakikishie yale waliyo mwambia
kuwa kuna msichana mzuri
wamemuandalia.
moody alikuwa ni kijana alie ishi
maisha ya kitajiri na alitumia pesa za
wazazi wake kwa kuzifuja katika
starehe jijini dar es salaam,
mbali na kuwa wazazi wake wana
uwezo wa kipesa baba yake moody
alikuwa mbunge huko mkoani arusha
na hata mama yake alikuwa mfanya
kazi wa serekalini.
moody alikuwa na urafiki mkubwa na
mpenzi wake rebeca kitu kilicho
pelekea awatambue vizuri kina
rebeca enjoy na amina na leo
alikuwa ameahidiwa na kina rebeca
kuwa kulikuwa kuna msichana
ambae walisema ni mzuri na ni
lazima angempenda!
moody akiwa bado anafikiria
msichana huyo ana uzuri kiasi gani
mpaka kusifiwa na kina rebeca ndipo
gari aina ya noah iliegesha eneo
maalumu la kuegeshea magari na
wasichana wanne wakashuka
akiwemo mariamu alie valia sketi
ndefu na viatu vizuri na bilauzi ya
blue huku nywere zake za kiarabu
zikiwa zime wekwa vizuri zikafanya
urembo wake uonekana dhahiri,
macho ya moody moja kwa moja
yalitua kwa mariamu na hapo
hakuamini kilichokuwa mbele yake
na tayari akaelewa yule mwenye asili
ya kiarabu ndo yule mariamu alie
ambiwa!
"wow karibuni warembo" moody
alisema huku akijiinua kwenye kiti
"ahsante shemu" rebeca ndo alikuwa
wa kwanza kuitikia
"vipi umefika muda mrefu" sauti ya
mpenzi wa rebeca aliendasha gari
aina ya noah ili uliza huku akizidi
kusogea
"hapana john ...karibuni viti" moody
alijibu kwa furaha
kina rebeca wakakaa na kutengeneza
mduara kuizunguka meza ambayo
dakika chache baadae ilifurika
nyama na vinywaji ambavyo asilimia
kubwa mariamu hakuvitumia.
mazungumzo ya hapa na pale
yaliendelea huku mariamu akiwa
kama msindikizaji wa mazungumzo
yale , muda wote moody mawazo
yake yalikuwa yame hamia kwa
mariamu na muda huu alifikiria
kumpata mariamu.
mara mariamu alianza kuhisi hali
tofauti na kuhisi kuna plan ilikuwa
imepangwa mbele yake
mariamu alilitambua hili baada ya
kuona kina rebbeca na john
wameenda kubarizi upepo ufukweni
na yeye walikuwa wamemuacha peke
yake akiwa na moody,
tayari mariamu alianza kuwa na woga
na muda huu alikuwa ameinamisha
sura yake chini akivichezea vidole
vyake,
"ah mariamu mi naitwa moody erick
naishi ostery bei...nimefurahi
kuonana na wewe!" moody aliongea
kuvunja ukimya
"mh mimi naitwa mariamu rakhimu
naishi tabata" mariamu aliongea
huku akijitahidi kutoonesha uoga
aliokuwa nao,
kwa upande wa moody aliona kama
anachelewa kumuambia mariamu
kuwa anampenda kwani mpaka hapo
uzuri wa mariamu ulikuwa
umemchanganya,
moody akaanzisha mazangumzo
yaliyo beba maneno mazuri yaliyo
muashiria mariamu kuwa moody
anamtaka , mariamu akazidi kujawa
na woga huku akiumiza kichwa kuwa
ampe jibu gani kijana huyu ambalo
lingetosha kumuambia kuwa
hamuhitaji
"by short mariamu mi nakupenda
toka moyoni" hatimae moody
aliamua kumuambia mariamu nia
yake, mariamu akakaa kimya kana
kwamba haja sikia
"mary i love you please ni amini
usinifikirie vibaya!" moody alisema
huku akianza kupeleka mikono yake
kwenye mabega ya mariamu na hapo
moody akatokewa na tukio ambalo
hakulitarajia!
mariamu kwa haraka aliisukuma
mikono ya moody kwa nguvu hu sura
yake ikionesha dalili zote za kuchukia
"sikiliza wewe mi sio maraya kama
unavyo dhani shika adabu yako"
mariamu alifoka huku akianza
kuinuka tayari alishajua kina rebeca
walikuwa wamemuwekea plan,
"hah kwani ugomvi mariamu"
"ahkah unikome..." mariamu alifoka
safari hii akianza kuhesabu hatua
kuondoka, mariamu alikuwa kaamua
aondoke peke yake akapande hiace
arudi kwao kwani hii ndo aliona njia
sahihi ya kuwepa vishawishi vya
moody,
mariamu akaaondoka huku akiwa
anapiga hatua kama za mtu mwenye
haraka kupita kiasi huku akielekea
kwenye geti la kutokea nje ya eneo
lile !
moody nae alishindwa kuvumilia
kumuacha mariamu akiondoka eneo
lile ,moody akasimama na kumfuata
mariamu ikiwezekana amzuie!
**rebbeca akiwa ufukweni na
wenzake muda wote macho yake
yalikuwa yanaangalia eneo walilo
kuwepo moody na mariamu, na
ghafla rebbeca alikishuhudia kitendo
cha mariamu kuinuka na kuanza
kuondoka
"shit huyu mariamu sijui ataacha lini
ushamba wake bwege kweli" rebeca
alisema huku akianza kuhesabu
hatua kwenda kuwahi kumzuia
mariamu ili asije kuleta aibu ambayo
rebbeca hakutaka imkute , hata
enjoy amina na john wakaanza
kumfuata nyuma rebeca kuelekea
walipokuwa kina mariamu!

4

Moody alimuwahi mariamu na
kumshika mkono "niache" mariamu
alifoka huku mkono wake mmoja
ukifanya kazi ya kutoa mkono wake
mikononi mwa moody na muda huo
rebbeca alifika!
"mariamu kuna nini" rebeca alimaka
"sikia nikwambie rebbeca tuna
heshimiana mi sio maraya....naomba
miniache" mariamu alifoka huku
akifanikiwa kuutoa mkono wake kwa
moody na kuondoka!
"samahani shemeji moody naomba
unisamehe, hii kazi naomba uniachie
please " rebbeca alisema kumuambia
moody aliekuwa ameduaa! na muda
huo waka ondoka na kuikatisha
weekend ile!
***
ilikuwa ni juma tatu kama kawaida
ilikuwa ni siku ya masomo na
wanafunzi wengi waliwasiri shuleni.
mariamu alikuwa amewasili shuleni
pale ila siku hii kulikuwa na tofauti
kubwa baina ya mariamu na kina
rebbeca !
mariamu tangu afike hakusalimiana
nao kabisa muda wote alionesha uso
wa kuwa alikuwa amekasirika!
rebeca aliamua kuvunja ukimya na
kujishusha kwa mariamu ili afinikishe
adhima yake ya kumuonganisha na
moody
"mambo mariamu jamani best hata
salamu leo hamna" rebbeca alisema
huku akijichekelesha
"ah poa mmeni boa" mariamu
alisema akiwa hamuangalii rebbeca
usoni
"ah tusamehe ila..ah tutaongea
badae best usijali" rebbeca alisema
huku akimpiga piga mariamu begani
na kurudi kwenye kiti chake.
muda wa mapamziko ulifika na
rebbeca akiwa na wenzake
walimfuata
na rebbeca akawa na kazi kubwa ya
kumshawishi mariamu juu ya moody
"mariamu wewe umeshakua na
isitoshe yule kijana anapesa na ni
mtoto wa mbunge!" ni maneno ya
rebecca aliyo tumia kumshawishi
mariamu ambae hakuwa tayari
kabisa
"bwana mi naya penda masomo
yangu wanaume wapo tu" mariamu
aliongea huku akihisi kina rebbeca
wanampango mbaya na usichana
wake
"ha! masomo yanaendelea kama
kawaida yule moody unakuwa
unaspend nae tu...fikiria yule ni
mtoto wa mbunge na anakupenda
ukimaliza masomo mnafunga ndoa
unaendelea na maisha kama
kawaida.... yaani anavyo kupenda
yupo tayari hata kukunulia gari!"
rebbeca alizidi kumuambia mariamu
maneno ambayo mariamu alianza
kuyafikiria .
mariamu aliyafikiria mara mbili
akafikiria maisha yakuwa na mtoto
wa mbunge! mariamu akamuomba
rebbeca ampe muda alifikirie lile
swala!
"jitahidi mariamu iyone kama bahati
watu wana zililia nafasi kama yako"
rebbeca alizidi kumshawishi
mariamu..,.
mawazo ya tamaa ya maisha
yalifanikiwa kupata nafasi kwenye
kichwa cha mariamu na mariamu
aliafiki kuwa na uhusiano na kijana
moody!
hii ilikuwa furaha kubwa kwa moody
kumpata msichana mariamu ambae
kwa muda mchache alifanikiwa
kuteka moyo wa moody!
taratibu mariamu alianza kuingia
kwenye mahusiano huku akiwa hajui
alikuwa alikuwa amejiingiza kwenye
janga.
upendo kati ya moody na mariamu
uliachipuka na kukua kwa kishindo
huku desturi yao ikiwa kila juma pili
lazima wakutane kwenye kumbi za
burudani na za kifahari, na kila
kulipo kucha upendo wao ulizidi
kukua.
mariamu akawa amebadirika kwa
kiasi kikubwa kwani hakuwa mariamu
aliekuwa mpole na hekima sasa hivi
mariamu alikuwa msichana aliejisikia
huku akiwa na jeuri ya kumjibu mtu
anavyo taka.
robbin aliweza kuona mabadiliko
haya kwa mariamu ambae
alimpenda toka utotoni. robbin kwa
haraka haraka aliweza kuhisi
mariamu yupo kwenye mahusiano,
robbin aliamua kujikaza na kujaribu
kwenda kumtongoza mariamu kwa
mara ya pili lakini mariamu alikataa
huku akimpa maneno makali ,robbin
akajua ni wazi kuwa hakuwa na
chake pale na robbin akajikuta
kwenye maumivu makali ya kumkosa
mariamu ambae aliwahi sababisha
chuki kati ya david na yeye
mwenyewe robbin!
starehe na upendo mkubwa kutoka
kwa moody vili fanikiwa kwa kiasi
kikubwa kuteka akili mariamu,
mariamu akawa anahisi anachelewa
kumaliza masomo yake ili aolewe na
aolewe na kijana moody ambae kwa
muda huo mariamu aliona alikuwa ni
chaguo lake sahihi!
japo mariamu aliyafanya haya lakini
bado aliyapenda masomo kitu
ambacho kilikuwa tofauti na wenzake
kwani yeye alifanikiwa kufaulu
mtihani wa form four hata rebbeca
pia ,amina na enjoy wao walifeli kitu
ambacho kili wapelekea kulisiti ,
robbini nae alifaulu ila alipelekwa
shule nyingine tofauti na aliyo
pelekwa mariamu ,robbin aliona bora
kusoma shule tofauti na mariamu
kwa alihisi ndo njia pekee ya
kukwepa maumivu ya mapenzi, siku
zote robbin alikuwa na ndoto za kuja
kuwa polisi wa ngazi za juu kwani
aliupenda sana upolisi!
mariamu akiwa form five akajikuta
akiupenda music kuliko burudani
nyingine, na baada ya kujichunguza
akajitambua kuipenda fan ya music
na kuona kama akijaribu ataweza na
anaweza kuwa nyota wa music
mariamu akapatwa na ndoto ya kuwa
muimbaji,
mariamu akamwambia moody kuwa
alikuwa na ndoto ya kuwa muimbaji
na kwa kuwa moody alimpenda
mariamu akamtafutia sehemu ya
kujifunza music na kukuza kipaji
chake, mariamu akawa anaendelea
na masomo huku na music akiupa
kipaumbele katika maisha yake na
hakutaka wazazi wake wajue.
"mariamu ujue nakupenda sana na
nafanye every thing for you?" ni
maneno ambayo moody aliambiwa
na mariamu wakiwa kwenye ukumbi
wa burudani
"yah nafahamu beby na hata mi
nakupenda zaidi ya unavyo fikiri"
mariamu alijibu kwa kujiamini
"ok, kuna kitu naomba unizawadie"
moody alisema kwa utulivu
"kitu gani"
"mariamu naomba unizalie mtoto !
please nakupenda" moody alisema
kwa kusisitiza, mariamu alifikiria na
kuona moody alikuwa sahihi
"mmh hata mi natamani ila masomo"
mariamu alisema kwa upole,
mariamu na moody walikaa
wakajadiri hatimae wakakubaliana
kuwa mariamu atamzalia mtoto
moody pindi akianza masomo ya
chuo kikuu!
**
mariamu alifanya mitihani ya form
six na kufaulu kwa alama nzuri huku
akiwa ameanza kufanya vizuri
kwenye music na alikuwa amesha
anza kuweka ndoto ya kutoa nyimbo
mmoja ya audio na video.
muda wa mariamu kwenda chuo
ulifika na mariamu aliwaambia
wazazi wake kuwa anataka awe
boarding na sio kwenda chuo na
kurudi nyumbani,mpaka hapa wazazi
wa mariamu tayari walisha ona
mariamu ameanza kuwa mtu tofauti
ila wao wakapuuzia waki dhani ni
usichana tu!
mariamu alipelekwa chuo alicho
faulia ndani ya jiji la dar na akawa
huko huko bwenini, wazazi wa
mariamu hawakujua kuwa kwa
kufanya vile kumpeleka mariamu
chuo na kuishi huko huko walikuwa
wamempa nafasi kubwa ya mariamu
kutimiza mpango wake wa kumzalia
mtoto moody!
moody alitafuta chumba kizuri kilicho
kuwa karibu na chuo hicho kwa ajili
ya mariamu.
chumba kile kikajazwa samani za
ndani na mariamu akawa anaacha
kwenda kulala kwenye mabweni na
kwenda kulala kwenye chumba alicho
pangishiwa na moody, kila siku
aliwasili na ndipo walipo afikiana
waanze zoezi lao la kuzaa mtoto,
mariamu bila woga wala kujiuliza
akaingia kwenye kazi ya kumzalia
moody mtoto!
muda huu mariamu alikuwa
ameshaanza taratibu za kurekodi na
kushoot wimbo wake wa kwanza
uliokuwa mfumo wa RNB.
tino alikuwa ni msanii ambae alikuwa
nyota chipkizi wa music wa kizazi
kipya tino alikuwa ameshakuwa
maarufu katika jiji hili la dar es
salaam , kwa kuwa moody alimpenda
mariamu aliamua kwenda kukutana
na tino na kupanga nae mipango ya
kumshirikisha kwenye wimbo wa
mariamu ,baada ya makubaliano kati
ya moody na tino ,tino alikubali
kwenda kufanya kazi na mariamu na
tino akaanza kufanya mazoezi ya
kuandaa wimbo akiwa na mariamu.
hata tino alipo kutana na mariamu
alihisi kwamba alikuwa yupo na miss
world ,tino akawa ameanza
kumtamani mariamu japo alijua ni
mchumba wa mood tino akanuia
kumpata mariamu kwa gharama
yoyote!.
ilikuwa ni furaha kubwa kwa
mariamu pale alipo jigundua kuwa
alikuwa na mimba , haraka
akamtaarifu moody ambae alipata
furaha iliyo pita kiasi ,siku hiyo hiyo
moody alimchukua mariamu na
kwenda nae kwenye eneo lilokuwa na
magari ya biashara, moody
akamnunulia mariamu gari nzuri ya
kutembelea , mariamu alifurahi sana
kupata gari ambalo lilikuwa la
thamani.
moody hakuishia hapo usiku wa siku
hiyo alifanya tafrija ndogo iliyo
husisha watu wanne tu, mariamu
rebbeca moody pamoja na camera
man aliekuwa na kamera yake
akirekodi mkanda wa video kipindi
tafrija ile ndogo ikiendelea, rebbeca
kwa macho yake alishuhudia
mariamu akikabidhiwa ufunguo wa
gari la kutembelea moyo wa wivu
ukamuingia rebbeca, kwa ni yeye
rebbeca aliewaonganisha mariamu
na moody na sasa mariamu
amekabidhiwa gari na
amepangishiwa chumba kitu
ambacho yeye hajabahatika kukipata
wivu huu wa rebbeca ukaanza
kujenga chuki ya kuchukia
maendeleo ya mariamu!
mariamu alimshauri moody kuwa
wafanye haraka arekodi wimbo wake
na video kabla mimba haijawa
kubwa, moody hakuwa na pingamizi,
maandalizi yakafanyika huku moody
akitumia pesa zake kufanikisha
malengo ya mariamu, hatimae
wimbo uliokuwa unazungumzia
mapenzi ulioimbwa na mariamu na
tino akishirikishwa ulitoka na kuingia
dukani ukiwa audio na video.
nyota njema huonekana
mapema, wimbo wa mariamu
ulipendwa na wapenzi wengi wa
nyimbo za rnb huku jina la chipkizi
mariamu likizidi kuenea na kuwa
maarufu jijini dar es salaam, na
ndipo mariamu alipoamini kuwa
ndoto yake ilikuwa sahihi.
hili likawa pingo lingine kwa
rebbeca , rebbeca alipatwa na wivu
kuona mariamu anakuwa maarufu,
japo mariamu alimuamini rebbeca
kama dada yake na hata kuwa nae
kwenye manzingira mbalimbali na
hata kumuazima gari lake mara kwa
mara ,ilikuwa ni bure kwa rebbeca
aliekuwa na wivu wa kichawi.
umaarufu na ustar alioanza kuupata
mariamu ulimfanya mariamu ahisi
hakuwa sahihi kumkubalia moody
kumbebea mimba kwani pale alipo
alikuwa anakaribia kuwa star
mariamu akaona pindi mimba ikiwa
kubwa na kuzaa atakuwa
ameuharibu usichana wake na hata
kujishusha kithamani kwa wasanii wa
kubwa ambao kwa muda ule
walianza kumtafuta wafanye nae
music!
mariamu akaamua kumuita rebbeca
nyumbani kwake na kumuomba
ushauri juu ya mimba aliyo kuwa
nayo ukiringanisha na umaarufu
ulioanza kumfuata
"wewe hiyo mimba itoe moody
utamwambia imeharibika
yenyewe...tangu lini nyota akawa na
mtoto akiwa bado binti"
rebbeca alimshauri mariamu
"kweli? but naogopa" mariamu
aliongea
"woga wako ndo umaskini wako, mi
nimewahi kutoa mimba nikiwa form
one.... mi nitakupeleka kwa doctor
ambae ni profession wa kutoa
mimba" rebbeca alimwambia
mariamu ambae aliona ulikuwa
ushauri wa maana mariamu
akakubali kwenda kuitoa mimba
huku akimsihi sana rebeca kuwa
inatakiwa iwe siri.
baada ya mariamu kutoa mimba kwa
siri akampigia simu mpenzi wake
mood na kumuambia kuwa mimba
imeharibika!
ilikuwa ni pigo kubwa kwa moody na
taarifa mbaya kabisa akatamani
aridhi ufunuke imfukie!
moody alipenda sana kuwa na mtoto
na sasa tegemeo la kupata mtoto
limepotea.!
moody akiwa kwenye hari ya
kuchanganyikiwa mara akapokea
simu kutoka kwa rebbeca
"hellow shemu" moody aliongea kwa
sauti iliyo pwaya
"shemeji wangu pole...ila
nakusikitikia sana kweli usilo lijua ni
usiku wa giza " sauti ya rebbeca
iliongea kutokea upande wa pili
"kwanini shemu mbona sikuelewi"
"shemeji mi siwezi kukuficha ..ukweli
ni kwamba mariamu ameitoa mimba
yako kwa makusudi, kwa maana
aliona ameanza kuwa nyota wa mziki,
ameona wewe sio type yake kwa
kuzaa nae mtoto shemu niamini
ninacho kuambia kama huamini
nikupeleke hata kwa doctor alie itoa
hiyo mimba" rebbeca alimaliza kutoa
maelezo kwa moody rebbeca alikuwa
ameamua kumsaliti mariamu kisa
wivu wa maendeldo,
akiri ilimruka moody na kuhisi
kuchanganyikiwa, alijiuliza ni kitu
gani mariamu alimuomba akakosa
kwake mpaka aue mtoto wake
mtarajiwa, moody akakumbuka
gharama alizo mgharamia mariamu
mpaka kufikia pale,
wazo likamuijia moody kuwa
mariamu atakuwa amepata
mwanaume mwingine ambae
atakuwa ni msanii mkubwa alie
mshawishi atoe mimba na kumuona
yeye hana thamani na hapo moody
aliposema mwanamke hathaminiki
"KAMA AME MUUA MWANANGU
MTARAJIWA NA YEYE HANA THAMANI
ONE DAY ATANIUA NA MIMI KWA
TAMAA YA MALI, LAZIMA NIMUUE
MARIAMU" aliongea moody huku
kichwa chake kikiwaza mpango wa
kumuua mariamu ambae muda huo
alimuona kama shetan.

5

moody alishindwa kudhibiti asila
zake akaingia kwenye gari na
kuwasha akaendesha kwa kasi
akienda kwenye nyumba aliyo
mpangishia mariamu !
hakuchelewa akawa amefika na
muda ulikuwa ni jioni ya saa kumi na
mbili lakini cha ajabu alikuta
mariamu hayupo ikabidi ampigie
simu
"upo wapi mariamu" moody aliuliza
baada ya simu kupokelewa
"sorry sikutaarifu nipo studio nafanya
mazoezi" mariamu alisema, hapo
moody akajihakikishia kuwa mariamu
alitoa ile mimba kwa makusudi kwani
kama ingekuwa bahati mbaya muda
huu mariamu angekuwa kwenye
masikitiko na sio kuwa studio, moody
akakata simu na kuingia kwenye gari
na kuondoka kwa kasi.
****
mzee rakhimu na mama mariamu
walishtuka walipo sikia kuwa mwanao
eti ni mwanamziki, hawakuamini
mpaka walipo letewa cd ya video ya
wimbo wa mariamu ambao aliimba
akiwa kavaa mavazi ya siyo maadili,
walishindwa kujua imekuaje mpaka
kufikia hatua ile na wakati walijua
yupo chuo kimasomo, walimpigia
simu mariamu na kumfokea sana na
kukilaani kiendo chake cha kuwa
msanii kitu ambacho kilipingwa na
imani ya dini yao, kitu ambacho
mariamu alijibu ni kwamba ile
ilikuwa ni fani yake na asinge weza
kuiacha, wazazi wa mariamu
wakabaki katika fedheha!
***
usiku huu moody hakupata usingizi
na mpaka kufikia saa sita alikuwa
amesha lewa chakari kichwa
kikimuuma akifikiria ubaya
aliotendewa na mariamu , moody
hakuwa na majibu sahihi zaidi ya
kuamua kulala na kesho yake
angempigia simu mariamu na
kumuita kwenye moja ya bar alio hisi
ingefaa kwa maogezi yake na
mariamu!
asubuhi ilipofika tu moody
akachukua simu na kumpigia
mariamu na kumuomba wakutane
kuna kitu wanataka kukijadili!
mariamu alishangaa siku hiyo
kupigiwa simu na moody asbuh na
mapema na sauti ya moody ilikuwa
tofauti sana siku hiyo ,mariamu
akaanza kuhisi kulikuwa kuna kitu
tofauti ,mariamu akajikaza na
kuamua kwenda kwenye wito wa
moody.
mariamu alifika kwenye mgahawa
ambapo moody alimwambia amkute
akamkuta moody akiwa amekaa
akiwa na chupa ya maji tofauti na
siku zote.mariamu alimsalimia
moody na moody akajibu kwa sauti
nzito iliyo pwaya , hapo mariamu
akaanza kuhusi kuna mambo hayapo
sawa, macho ya moody yaliyokuwa
mekundu yakatosha kumuambia
mariamu kuwa moody hakuwa sawa,
"mariamu kitu gani uliwahi kuniomba
ukakosa kwangu" moody aliongea
akiwa hamuangalii mariamu usoni,
mariamu alishangaa kuulizwa swali
akiwa hata hajakaa na wala
hajaagiza chochote kama ikivyokuwa
kawaida
"mmh mbona umeniuliza hivyo
baby?" mariamu aliuliza swali badala
ya kujibu swali la moody
"kwanini wanawake hamthaminiki? "
moody aliongeza swali ,mpaka hapo
mariamu akajua hakuna amani
"niambie huyo mwanaume
amekuahidi zawadi gani mpaka
uamue kuitoa mimba yangu na
kummua mtoto wangu mpendwa
mariamu" moody aliongea huku
machozi yakimrenga, mariamu
alishtuka na kujua mambo
hadharani, mariamu akajiuliza
moody amejuaje bila shaka kuna
mtu katoboa siri ndio ikawa wazo la
mariamu
"moody haki ya mungu i swear to god
mimba imeharibika na sija itoa
makusudi" mariamu alisema
kujitetea na mara simu ya mariamu
ikaita mariamu akaangalia kwenye
kioo cha simu na kupokea "hallow
tino nipigie baadae kuna shughuli
nafanya now..poa"aliongea mariamu
na kuweka simu mezani, moyo wa
moody ulishtuka nyewre zika
msisimuka baada ya kujua maria
akimtaja tino aliekuwa msanii katika
jiji la dar hapo hapo moody
akaingiwa na fikra kuwa tino ndo
alimrubuni mariamu na kumtogoza
na mpaka mariamu kuiharibu mimba
ya moody,
"ok tino amekulaghai mpaka umefikia
hatu a ya kumuua mwanangu akiwa
kwenye tumbo lako linaloshikwa
every day na tino" moody aliongea
kwa hasira, kauli hii ilimchukiza
mariamu, ni kweli tino alimtongoza
mariamu lakini mariamu
hakumkubalia japo tino kila siku
alimsihi mariamu, mariamu akajua
moody amesema vile kwa sababu
ameona kaongea na tino kwenye
simu
"sikia nikwambie wewe mwanaume
mimi sio maraya kama unavyo zani
usiwe na wivu kwenye kazi mi
sijawahi kukuingilia kwenye kazi na
watu wako unaofanyanao kazi tino
nimtu tunaefanya nae kazi na wewe
ndo ulimleta kwangu" mariamu
alifoka ikiwa kama njia ya kumzuia
moody asiweke hoja za nadharia,
marumbano ya hapa na pale
yalitokea kati ya mariamu na moody
huku mariamu akiwa na msimamo
wake wa kuwa hakutoa mimba na
hana mahusiano tino
"ok kama kweli hukutoa ile mimba
basi fanya ubebe mimba yangu
nyingine" moody aliongea maneno ya
kukata mzizi wa fitina na kumtega
mariamu, hili likawa neno kwa
mariamu mariamu akamwambia
moody ampe muda afikirie ,
mariamu na moody wakaondoka
huku mariamu akiwa amemuambia
moody ampe muda afikiri juu ya
swala la kubeba mimba ya pili....
mariamu alihisi huenda rebbeca
amemsaliti na kutoboa siri mariamu
kwakuwa alikuwa hana uhakika
hakumuambia kitu rebec na
kumshtumu kuwa kapeleka umbea
kwa moody.
siku zilikwenda huku kila siku moody
akimuambia mariamu ampe jibu juu
ya swala lake la kumbebea mimba
nyingine, kwa upande wa mariamu
hili swala lilikuwa gumu kwani muda
huo alikuwa ameshakuwa msanii
maarufu huku wasanii wengi
wakimuomba afanye nao music , na
mariamu alikuwa ana malengo ya
kufika mbali kimziki na hapo badae
ange gombea umiss tanzania ,kwa
malengo haya yalimfanya mariamu
apinge swala la kubeba mimba ya
moody kwani ingemuharibia malengo
yake kwanjia moja au nyingine
"sikia nikwambie moody mi nimeanza
kuwa super star na nina malengo
mengi kiukweli siwezi kubeba mimba
yako sorry" haya yalikuwa maneno ya
mariamu aliyo mwambia moody kwa
njia ya simu!
hapa moody akajihakikishia kuwa
mariamu alikuwa anatembea na
msanii maarufu kama sio tino alie
mpa kiburi cha kutoa mimba . moody
alifikiria kuwa niyeye aliemfikisha
pale mariamu lakini mariamu
alikuwa kaanza kuota mapembe
"lazima nimuue huyu maraya pamoja
na tino anaempa kiburi" moody
alijisemea huku hisia zake zikimuhisi
tino ndo anae mlaghai
mariamu ,moody akawa anaumiza
kichwa juu ya kutekeleza mauaji ya
watu wawili mariamu na tino "mimi
ni mtoto wa mbuge nitawaua na
maiti zao hazita onekana milele."
alijiongelea moody, moody akaanza
mikakati ya kutekeleza mauaji!
ukweli ni kwamba mariamu hakuwa
na mahusiano tino japo tino tayari
alikuwa amemtongoza, na mariamu
bado alimpenda moody ila alifanya
vile kulinda usuper star na
umaarufu, mariamu hakujua kuwa
moody alikuwa na mkakati mbaya
zidi yake!
***
moody alitulia na kupanga mpango
wa mauaji ,na alipanga aanze kumua
mariamu alie msaliti , moody alitaka
amue kwa usiri ili isije gundulika
kuwa yeye ndo muuaji moody
akatafuta mtu mmoja ambae
alipanga atamsaidia kutimiza adhma
yake!
baada ya moody kukamilisha
mipango yake na kupata mtu wa
kumsaidia aliarudisha upya
mahusiano kwa mariamu na
kumuambia wasahau yaliyo pita
waendelee na penzi na mariamu
akakubali kwa furaha kwani
alimpenda moody mariamu hakujua
moody alikuwa anaumendea uhai
wake!
ilikuwa ni mida ya saa mbili moody
alikuwa kwenye yake iliyopo mbezi,
moody alikuwa amekaa kwenye sofa
na mbele yake kulikuwa na meza
iliyokuwa na chupa ya pombe kali
iliyo nywewa nusu, pembeni ya
chupa kulikuwa na bastola iliyo
wambwa kiwambo cha kuzuia sauti,
hii ni siku ambayo moody aliazimia
kutekeleza azma yake, moody
alichukua simu yake na kwenda
kwenye orodha ya majina na
kumpigia mariamu simu ikaita...
"hallow baby" mariamu aliongea
kwenye simu
"ah mariamu nakuomba uje mbezi
kwenye ile nyumba yangu kuna
bonge la surprise for you" moody
aliongea kwa uchangamfu
"mbona usiku na hiyo barabara huwa
inafoleni sana?" mariamu aliuliza
"we chukua bodaboda uje ni muhimu
sana"moody alibembeleza,
"sawa baby na kuja dakika sifuri"
mariamu aliongea na moody akakata
simu "leo atakufa na umaalufu wake"
alisema moody na kuendelea kunywa
pombe!
wakati mariamu akiongea na moody
alikuwa yumo ndani ya gari yake
akiwa na rebbeca wakielekea club
"oya wewe tangulia moody kaniita
nitakukuta club" mariamu aliongea
na kushuka akachukua bodaboda na
kuianza safari ya mbez huku
akimuahidi rebbeca kuwa atamkuta
club.
boda boda ilimfikisha mbezi na
mariamu akaamua kushuka na
kununua chips ili akale na mpenzi
wake kwani alijihisi njaa ,baada ya
kuchomewa chipsi na kufungiwa
kwenye mfuko mariamu akaanza
safari kwa miguu kwani hapakuwa
mbali kutoka pale, ama hakika
malaika mtoa roho alimuongoza
mariamu kuzimu!
moody akiwa amekaa akimsubiri
mariamu kwa hamu mara mlango
ukagongwa "maraya kajileta" alisema
moody na kuchomeka bastola yake
kiunoni na kufunika na shati
isionekane na kwenda kufungua
mlango, moody akafungua mlango
mariamu akaingia kwa furaha na
moody akafunga mlango kwa
ufunguo na kuzichukua funguo
akazia tia mfukoni mwake.....
mariamu akawa amejipeleka kwenye
kaburi lake mwenyewe.

....6....

mariamu alipo msalimia moody moody akaitikia na hapo mariamu akakutana na harufu kali ya pombe kutoka kinywani mwa moody na kitu kingine kilicho mshtua mariamu ni pale moody alipo funga mlango kwa ufunguo na kisha funguo kuzitia mfukoni
"vipi mbona unafunga mlango " mariamu aliuliza kwa mastaajabu
"ah tusije tukavamiwa hii mbezi bwana sio osterbey" moody alisema na kumlizisha mariamu
"baby mi acha nioge kwanza nahisi joto" alisema mariamu na kwenda bafuni na kuziacha chips zake mezani,
haikuchukua muda mariamu kuoga kwani bafu ilikuwa ni ya kisasa iliyokuwa na bomba maalumu kwa ajili ya kuogea, mara mariamu akatoka bafuni akiwa na kijitaulo kifupi kilicho acha sehemu kubwa ya mwili wake wenye ngozi ya kuvutia mariamu hakumkuta moody sebureni mariamu akaenda moja kwa moja hadi kwenye kabati nakuchukua sahani na umma na kwaajili ya kula chipsi zake
"moody mi nakula chips wewe huli" mariamu alipaza sauti baada ya kuwa amesha weka chips kwenye sahani
"nakuja"sauti ya moody ilitokea chumbani, na mariamu akiwa bado na taulo yake akaanza kula chips kwa umma na mara muda huo akamuona moody akitokea chumbani
moya wa mariamu ulilipuka kwa hofu akatamani kukimbia lakini hakuiona njia kwani alihisi malaika mtoa roho alikuwa mbele! mikononi moody alikuwa amevaa grove za mpira zinazo tumiwaga mahosptalini na kilicho mshtua zaidi mariamu nipale alipoiona bastola iliyo wambwa kiwambo cha sauti ikiwa kwenye mkono wa moody wa kulia mariamu tayari akawa amesha gundua kilichokuwa mbele yake! mariamu alivyo mtazama moody usoni akakutana na sura iliyo jaa chuki mariamu akataka kuinuka akimbie
"kaa chini usithubutu kupiga kelele " moody alifoka na kumsogelea mariamu , mariamu alitetetemeka huku mapigo ya moyo yakimuenda mbio jasho la taharuki likimtoka "sali sala zako za mwisho nyau wewe... mimi ndo nimekufanya uwe maarufu lakini umenisaliti ..." moody alifoka
"please moody usinuuwe nakupenda moody nisame.." kabla mariamu haja mariamu hajamaliza kuongea kofi zito la moody lilitua shavuni kwake na kumsukuma ukutani yowe likamtoka maraimu moody akaenda kwenye tv na kuiwasha mziki sauti ya juu ili majirani wasisikie kinacho endelea humo ndani na kurudi alipo anguka mariamu
"wewe kwa wema nilio kutendea na maovu ulie nilipa chagua nikuuwe kifo kipi" moody alikalipia mariamu ambae muda huu shavu lake lilikuwa na alama za vidole vya moody,
"moody kwanini unanitenda hivi moody ...kama ni mtoto nipo radhi kuku zalia" marianu alisema kwa kulia huku akiwa haamini kama ni mpenzi wake alie mbele yake na muda huo moody akatoa simu yake mfukoni na kupiga namba flani
"hallow ramso...oya njoo haraka mbezi tukamilishe ile kazi..yah ni nae...poa usisahau kuchukua koleo " moody aliongea na mtu wa upande wa pili kwenye simu, mtu aliongea nae moody ndio yule mtu ambae moody alimtafuta ili washirikiane kumuua mariamu kisha wakamfukie
"mariamu nakuua na utabaki historia na hakuna atakae hisi kuwa ni mimi nilie kuua" moody aliongea na kisha akaanza kufuta namba ya simu ya mariamu na meseji zote kwa kifupi moody alifuta kila kitu kwenye simu yake kilichomuhusu mariamu ilikupoteza ushahidi , mariamu akajua tayari kifo kilikuwa mbele yake mariamu akaishiwa nguvu na kujihisi alikuwa njiani akielekea kuzimu na mara moody akamsogelea pale alipo kuwa mariamu akapiga magoti akimuomba moody asimuue na hapo teke la mguu wa moody uliokuwa peku ukampiga mariamu na kumsukuma mpaka pembezoni mwa meza
"nyie wanawake ni mashetani sasa na kuua ili ukakatane na ibirisi alie wapa kazi ya kuwa wafuasi wake'" moody aliongea kwa kwa hasira huku akiwa hana huruma hata kidogo na mariamu , moody akamsogelea mariamu alipokuwa pale chini na kuzikamata nywele zake laini na kuzivuta kwa nguvu yowe likamtoka mariamu huku sauti yake ikimezwa na sauti ya mziki alio uwasha moody " mariamu wewe umeniulia mwanangu lazima ufe" moody aliongea kwa hasira huku akimkazia macho mariamu na kuzidi kuzivuta nywele zake na mariamu akazidisha kulia kwa nguvu akiomba msaada, pombe aliyo kunywa moody ilikuwa imeondoa kabisa huruma yake kwa mariamu !
kwa nguvu zake zote moody alimnyanyua maria na kwanguvu akabamiza paji la mariamu kwenye ukuta na kumkandamiza mpaka pale kwenye ukuta kukabakia alama ya damu na hapo hapo moody akapeleka mkono wake shingoni kwa mariam na kumkaba kwa mkono mmoja huku mkono mwingine ukiwa umeshika bastola...mariamu akawa amebanwa kwenye ukuta huku akipalangana kutoka lakini alishindwa kutoka kwa mkono wa moody, na hapo moody akapeleka bastola kwenye kichwa cha mariamu na kumkandamiza kwenye paji la uso wa mariamu ambao tayari ulikuwa na kovu pembeni kidogo ya paji la uso.na uso wake ulikuwa umeiva na kuwa mwekundu sababu ya makofi ya moody, moody alikuwa kadhamilia kumuua mariamu na muda huu alikuwa anataka akamue trigger na kukipasua kichwa mariamu kidole cha shahada cha moody taratibu kikaanza kubonyeza kifyatulio cha kuruhusu risasi!

mara ghafla mkono wa moody uliachia shingo ya mariamu! na muda huo yowe kubwa likamtoka moody bastola yake ikimtoka na kudondoka na muda huo damu nyingi zikaanza kumtoka moody shingoni !!

<<<sehemu mariamu alipokuwa amebanwa na moody ukutani pembeni yao kulikuwa na meza ambayo muda mchache uliopita mariamu alikuwa amekaa akila chips na uma aliokuwa anautimia kulia ulikuwa pale pake juu ya meza!
wakati moody anaendelea kumbana mariamu na kujianda kumtwanga risasi ,mkono wa mariamu ulitapa tapa akiutupa huku na kule na hatimae alishika juu ya meza na kushika ule uma na hapohapo mariamu akapata cha kujisaidia, mariamu hakusita alinuua uleuma na kumchoma moody na kuzamisha umma ndani ya shingo ya moody na damu zikamrukia mariamu ambae kwa muda huu mwilini mwake alikuwa amebakia na nguo ya ndani taulo ilikuwa imedondoka!
umma ulikuwa umezama sawia kwenye shingo ya moody, moody alipepesuka huku yowe likimtoka mikono yake yote ikiwa imeshika shingoni mwake !
mariamu alipata woga mkubwa kwani alimchoma moody na umma kwa kujitetea mariamu akabaki ameduaa ukutani akiwa anamuangalia moody akitapa tapa na mara mariamu akamuona moody akiyumba huku akielekea palipo anguka ile bastola hapo mariamu akajua moody alitaka achukue bastola ili amuue, mariam alitoka mbio pale alipo kuwa na kumkalibia moody na kumsukuma kwa nguvu moody akaanguka pembeni na mariamu akachukua bastola na kuelekeza alipokuwa moody na kufyatua risasi tatu mbili zikamkosa moody na moja ikatoboa kifua cha moody yowe hafifu likamtoka moody na kutulia palepale akipumua pumzi za mwisho mariamu akawa amemuua mpenzi wake moody!
woga ukamvaa mariamu pale alipo jua tayari ame ua tena kamua mpenzi wake, mariamu alikuwa ] anampenda sana moody lakini ndo tayari imesha tokea, wazo la kesi ya mauji likamuijia mariamu, mariamu akajua kama atagundulika kuwa yeye ndo aliingia mule ndani basi kesi ya mauaji ingemkabili ,mariamu akakurupuka na kwenda alipo lala moody na kuchukua funguo mfukoni mwa moody na kwenda kufungua mlango mariamu akafungua mlango na kuangaza nje hakuona mtu mariamu akaamua aende bafuni haraka aoge ajifute damu kisha atoeke eneo lile mariamu akaingia bafuni na kuanza kuoga!

kosa alilo fanya mariamu nikuto kufunga mlango wa nje! kwani akiwa bafuni mtu alikodiwa na moody kuja kusaidizana kumua mariamu aliwasili eneo lile akiwa na gari akashuka na kusogea mlangoni na kwa kuwa alisikia mziki ndani akaona bora aingie ndani ,jambazi huyu alie itwa ramso akafungua mlango na kuingia ndani mule palipo tapakaa damu ya moody!

....7....

ramso alisukuma mlango na kuingia ndani! "oya moody" ramso aliita akiwa bado hajaangalia vizuri hali ya mule ndani , ramso akatembeza macho na ndipo alipoiona hali iliyo msababishia kihoro, macho yalimtoka ramso baada ya kuona mwili wa moody ukiwa katikati ya dimbwi la damu, ramso akataka kupiga yowe lakini akashindwa , ramso alimjua moody kuwa ni mtoto wa mbunge ramso akajua kama atagundulika au kukutwa kwenye hiyo nyumba basi angekuwa na kesi ya mauaji ambayo hata yeye hakujua yalifanywa na nani!hapo hapo ramso akafungua mlango na kutoka nje kwa kukimbia huku akiacha mlango ukijibamiza ramso akakimbia mpaka kwenye gari lake na kuliwasha akaliondoa kwa kasi akiwa amechanganyikiwa akijiuliza ni nani ame muua moody!

mariamu alipokuwa bafuni aliweza kuhisi kama mtu akiita "oya moody" mariamu akatulia akisikiliza huku akitetemeka na mara mariamu akazisikia vishindo vya mtu vikitoka nje huku mlango ukibamizwa ,mariamu akajikaza na kutoka bafuni akaenda dirishani na kuchungulia , mariamu akamuona ramso akimalizikia kwenye tax yake na kuiwasha kwa kasi na kukimbia, hapo mariamu akaanza kuhisi yupo kwenye hatari na jela ili kuwa mbele yake, mariamu hakujua yule mtu alikuwa ni nani na alifuata nini, au alikuwa polisi mariamu akawaza, au ni ndugu wa moody?wazo hili kidogo mariamu alilipa kipaumbele "inamaana ameshudia mauaj4...na ameenda kuoa taarifa kituo cha polisi " hili wazo likamfanya mariamu aione balaa inayo mkabili mbele yake , haraharaka mariamu akanda zilipokuwa nguo zake na kuzivaa haraka haraka na kuanza kutoka nje maraiamu akiwa anataka kutoka nje aliuangalia mwili wa mpenzi wake alie muua kwa kujitetea , mariamu akatazama kuwa moody alikuwa kava grove ili kama angemua mariamu isije ikatokea zikakutwa alama ya vidole vayake kwenye mwili wa mariamu, hapo mariamu ikawa kama kaamshwa kutoka usingizini akawaza kuwa yule ni mtoto wa mbunge kwa hiyo ni lazima upelelezi mkubwa ungefanyika ili kumnasa muuaji, hapo mariamu akapata wazo la kuhakikisha anafuta sehemu zote anazokumbuka kuzishika humo ili alama za vidole vyake visigundulike kwa wa pelelezi, mariamu akaingia chumbani mwa moody na kuchukua grove na kuzivaa akachukua taulo kubwa na kuanza kufuta sehemu zote alizokumbuka aligusa kwa mikono yake.
mariamu muda huu alikuwa kama aliechanganyikiwa na hata akiri yake haikuwa vizuri, baada ya mariamu kufuta sehemu zote alisogea kwenye mwili wa moody na kuanza kuufuta sehemu alizo hisi kuwa alimshika !

mariamu alipo ridhika kuwa amefuta arama za vidole taratibu akafungua mlango akiwa na wasiwasi wa kukutwa na polisi eneo lile,akatoka nje na kukutana na hari ya hewa ya upepo ulio puliza ,mariamu akatembea kwa woga mkubwa akihisi kusimamishwa muda wote . hari aliyo kuwa nayo mariamu kama angetokea mtu akamsimamisha basi huwenda mariamu angekimbia mbio ambazo hakuwahi kukimbia lakini bahati ilikuwa upande wake hakusimamishwa na mtu yeyote -
muda ulikuwa kama saa tano usiku mtaa wa mbezi ulikuwa kimya sana hari iliyo zidi kujenga hofu kwa mariamu na kumfanya atembee kama anakimbia na muda huu alikuwa na viatu mkononi akihofia kuanguka . mariamu alishusha pumzi ndefu pale alipofanikiwa kufika barabara kubwa inayokwenda ubungo na kabla hajasimama sana basi ya mbezi kwenda ubungo ilipita na mariamu hakuchelewa akapanda kwenye basi lile akiwa kainamisha uso asije kuonekana na watu walimfahamu.

****
ramso akiwa kwenye gari aliendesha gari kwa kasi ya ajabu akiwa amechanganyikiwa huku maswali yasiyo na majibu yakikiandama kichwa chake . ramso alivyoingia barabarani tu akakutana na trafiki akipiga mkono gari yake , ramso alishtuka sana kupigwa mkono muda kama ule saa nne usiku ,hapo kwa haraka haraka ramso akajua itakuwa taarifa za mauji ya moody zimesha wafikia polisi na sasa wanasimamisha kila gari linalotiliwa mashaka , ramso alifikiria ndani ya gari lake alikuwa na koleo na hata mfukoni alikuwa na bastola ,ramso akajua kama atakaguliwa na kukutwa na vitu hivyo basi kesi ya mauaji ilikuwa ina muangukia ramso akaona njia rahisi ni kukimbia na kutoweka , haraka ramso akabadilisha gia nakuogeza speed akaliondoa gari kwa kasi huku akimkosa kosa kumgonga yule trafiki ,ramso akaona kama atashika barabara ya kwenda ubungo ni wazi angeweza kukuta foleni ambayo ingepelekea kukamatwa ramso akaamua kushika upande wa kuelekea kibaha aweze kukimbia ile kesi ikiwezekana atoroke dar es salaam, ramso alijua hata kama atatoroka lazima angetafutwa kwani alijua kama watakuja makachero kupeleleza kifo cha moody basi wangeweza kugundua moody kabla ya kufa alimpigia simu ramso ,hizi hisia ndio zilimfanya ramso awe na mashaka na kuwa na maamuzi ya kutoroka, ramso akaongeza speed akidhani kuwa alikuwa sahihi kumkimbia yule trafiki!

yule trafki alishangaa sana kumuona mtu alie msimamisha akikimbia na hapo akawa na mashaka kuwa huwenda mtu huyo akawa na madawa ya kulevya ,trafki akachukua radio call na kutoa taarifa kituo cha polisi na kwa wenzake wa barabarani akiwaambia kuna mtu amemsimamisha lakini haja simama amewasha gari na kuelekea kibaha!

***
ramso akiwa kwenye gari hakuona dalili ya kufuatwa na polisi kitu ambacho kilimpa matumaini kuwa atafanikiwa kutoroka dar es salaam!

akiwa anaendesha gari kwa speed mara ghafla alishtuka alipona mbele ya kuna gari mbili za polisi zilizo ziba barabara na polisi wakiwa wamesimama ,ramso akataka ageuze gari na arudi alipo toka na hapo hapo nyuma yake akaona difenda ya polisi ikija mwendo wa kasi hapo ramso akajua tayari amekwisha , ramso alicho amua ni kuchuka bastola yake na kuificha ndani ya gari na muda huo polisi walishuka kutoka kwenye difenda iliyokuwa nyuma yake na kumuweka chini ya ulinzi!

****

mariamu alishuka ubungo mataa na kuchukua tax iliyo mpeleka mpaka kwake ,mariamu alifika na kujitupa kitandani akiwa hoi na hapo akakumbuka tukio alilofanya masaa machache yaliyo pita mariamu akaangusha kilio cha kwikwi akijua wazi alikuwa matatani mariamu hakutaka kuamini kuwa alikuwa amemuua mpenzi wake .woga wa mauti ukamkumba mariam akahisi kuiona sura ya marehemu moody ,mara mariamu akashituliwa na mlio wa simu yake alikuwa akipigiwa mariamu akachukua simu yake na kuangalia mpigaji alikuwa ni rebbeca!
"hellow marry bado upo kwa moody"sauti ya rebeca kwenye simu ilimfedhehesha mariamu
"ah na... we...we fanya hivi hiyo gari utaenda kupark kwenye eneo la kulipia usije home" mariamu aliongea kwa kitetemishi na kumshangaza rebbeca
"ok"simu ikakatwa, na hapo mariamu akajua kuna balaa lingine, ni kwamba rebbeca anajua kuwa mariamu alienda kwa moody usiku nini kitatokea rebbeca akijua usiku huo moody ameuwawa! kama rebbeca alishindwa kuficha siri ya mariamu kutoa mimba je? angeweza kutunza siri kuwa usiku moody ameuwa ndio usiku ambao mariamu alienda kwa moody! mariamu bado akawa kwenye nyakati za mashaka, usiku huo mariamu hakupata hata lepe la usingizi!

****

ilikuwa ni saa tatu kasoro katika mtaa wa mbezi kwenye nyumba ya moody polisi walikuwa wamejaa nje wakizunguka zunguka wakisubiria oda kutoka ngazi za juu, polisi walikuwa wamefika hapa baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mfanya usafi aliekuwa ameajiliwa na moody kufanya usafi akija asubuh anafanya usafi na kuondoka , mtu huyu alitoa taarifa baada ya asubuhi hii kuja kufanya usafi na kukuta mwili wa moody ukiwa kwenye damu iliyoanza kukauka!

mbali na polisi ndani ya nyumba hii kulikuwa na timu ya makachero watatu walio wasili muda sio mrefu eneo la tukio!
katika makachero hawa mmoja wao alikuwa ni ROBBIN ! naam ni yule robbin ambae aliwahi kusoma shule moja na mrembo mariamu na alimpenda ila alimkosa!
<<<robbin baada ya kufika form six na kuwa yupo shule tofauti na aliyo soma mariamu, robbin akamua kusomea masomo ya I. P. L yaani INTERNATIONAL POLICE LAW, na kwa kuwa alipenda kuwa polisi alifanya vizuri na hatimae akabahatika kuwa mpelelezi wa makosa ya jinai, mpaka kufikia hapa robbin alikuwa amesha shiriki kwenye uchunguzi wa kesi kadhaa kubwa za mauaji na alifanya vizuri na kumkamata muuaji, na leo alikuwa kaja kwa ajili ya kuchunguza ni nani alie muua moody mtoto wa mbunge akiwa na timu yake iliyo aminiwa na serekali.

robbin tangu afike na wenzake kuna baadhi ya vitu alianza kuvihisi na kuvigundua, afande robbin akasogea na kuchutama pembeni ya mwili wa moody akiwa na grove zake kazivaa "mazingira yanaonesha mara ya mwisho kurikuwa na mwanamke humu na kulikuwa na purukushani" robbin aliongea kwa sauti ya chini...tayari robbin alianza kuhisi hari tofauti....

...8....

"kwanini na umejuaje sir robbin" sauti ya kike iliuliza ,ilikuwa sauti ya kachero veronica aliekuwa mmoja wa makachero
"tazama hapo chini kwenye damu kuna alama ya soli ya kiatu cha kike..." robbin aliongea nakisha kwa mkono wake wenye grove ukaenda kwenye kiganja cha mwili wa mood na kuchukua baadhi ya nyewe zilizokuwa kwenye kiganja cha mariamu (zilikuwa ni nywele zilizobaki kwenye kiganja cha moody pale alipo zishika nywele za mariamu)
"hizi ni nywele za kike inamaanisha huyu mwanamke alikuwa na pulukushani na marehemu"robbin alitoa maelezo
"kitu kimoja kina nitatiza... mwili wa marehemu viganjani una grove hivi kulikuwa kuna nini kinaendelea kabla ya moody kufa" sauti ya kachero alie alie julikana kwa jina la fadhili ilisikika
"ni utata mtupu " veronica alisema akiwa anatazama eneo la tukio kwa makini .

uchunguzi uliendelea huku makachero hawa watatu wakichunguza kila kitu na kutafuta kielelezo kitakachowawezesha kumjua muaji.
katika uchunguzi waliweza kugundua kuwa muaji alimpiga moody risasi moody akiwa sakafuni, na walifanikiwa kuziona risasi zilizo mkosa moody na kuchimba sakafu kitu ambacho kilimaanisha alie fyatua risasi hakuwa mzoefu wa kutumia siraha, robbin katika chunguza chunguza yake aliweza kuona doa kubwa la damu lililokuwa ukutani (ni pale alipobamizwa mariamu paji lake la uso ukutani) robbin alisogelea ukuta huo na kuchunguza na hapo robbin akatambua kuwa kuna mtu alibamizwa kwenye ukuta huo kwa paji la uso na kuacha alama ile, robbin akauangalia mwili wa moody haukuwa na kovu kwenye paji la uso swali likamuijia robbin kuwa ni nani aliebamizwa pale na ni nani alimbamiza, utata wa kesi hii ukazidi kujidhihiriasha robbin na makachero wengine kwani mazingira yalionesha kuwa kabla ya kifo cha moody kulikuwa kuna mvutano wa ugomvi kati ya moody na mtu anae hisiwa kuwa ni mwanamke, na kitendo cha kuzikuta grove viganjani mwa moody kilimaanisha kuwa kuna tukio moody alikusudia kulifanya .
makachero walitafuta tafuta hatimae walibahatika kuipata simu aliyo kuwa akitumia moody hii kidogo ikawapa matumaini ya kufanikisha upelelezi wao ! hawakutaka kupoteza muda muda huo huo walianza kuipekua simu ya moody ,cha kwanza kabisa wali anza kukagua kwenye namba zilizo toka na kuingia yaani zilizo pigwa na kupigia na ndipo walipo kuta jina na namba ya ramso ikiwa ni namba ya mwisho aliyo ipigia marehemu moody na tena ilipigwa usiku saa nne, hapo makechero wakajua bila shaka huyu ramso atakuwa anahusika kwa ukaribu na hili tukio!
"ok, hakuna kupoteza muda, veroneca chukua hii namba ya ramso uipigie kwa simu yako uongee utakavyo weza ili uweza weka nae promise ilitumtie mikononiikiweze kana leo" fadhili aliongea na kumpa simu veroneca.
veronica alikuwa mzoefu wa kaziya upelelezi alikuwa takiribani anamiaka mitatu kwenye kazi hii ,ni robbin pekee alikuwa ndo kwanza anatimiza mwaka wa kwanza na alikuwa bado kijana mdogo,tofauti na fadhili aliekuwa mtu wa makamu huku akiwa ana miaka zaidi ya mitano kwenye kazi hii, ni uchapa kazi mzuri wa robbin ndio ilimfanya ateulewe kuwa kwenye timu hii ya makachero ambao mara nyingi hupewa kesi za kuchunguza mauaji kama haya ya moody.

veronica baada ya kuweka namba ya ramso kwenye simu yake alipiga na kweka sikioni kisha akakohoa kidogo kulegeza sauti simu ikaita kidogo ikapokelewa
"hellow ramso"sauti nyororo ya kachero vernica iliongea
"halo, ndugu mwenye hii simu yupo kituo cha polisi kuna tuhuma zimemkuta ,anaomba taarifa hii mumpe mjomba wake haruna aje amuwekee mzamana" sauti ya upande wa pili ilosikika kwa lafuzi ya kipolisi,tofauti na mategemeo ya veronica
"yupo kituo gani" verokica aliuliza huku safari hii sauti yake ikiwa ya kikakamavu
"kituo cha mbezi"
"ok," veronica alizungumza na kukata simu na kuwageukia wenzake! uso wake ukiwa umejenga taharuki
"vipi veronica" robbin aliuliza.
"huyu mtu yupo kituo cha polisi ameshikiriwa na polisi anatuhumiwa..." veronica alibainisha
"itawezakana vipi....ok sio mbaya tunaweza kwenda hapo kituoni na kama atakuwa ndo yeye aliwasiliana na mareheu tuta angalia utaratibu" kachero fadhili alisema na kuanza kuamka akifuatiwa na wenzake, kabla ya kuondoka robbin akatoa camera yake na kupiga picha mwili wa moody na eneo alipo lala pamoja na pale ukutani penye doa la damu, na muda mchache baadae wakaanza kuondoka wakiacha polisi wakifanya harakati za kuupeleka mwili wa moody sehemu maalumu kwa ajili ya kuchunguzwa zaidi.

Waliingia kwenye gari yao na kuanza safari ya kituo cha polisi cha mbezi na hapakuw waliwasili haraka.
Wakafika wakajitambulisha kwa mkuu wa kituo na kumueleza kuwa walikuwa wapo kwenye kazi ya uchunguzi wa kesi ya mauaji yaliyotokea jana usiku na ndipo walipofanikiwa kujua kuwa ramso ndo alikuwa mtu wa mwisho kuwasiliana na marehemu na aliwasiliana nae usiku huo huo wa tukio! afande baada ya kusikia hivyo akashtuka kidogo ,makachero wakamuuliza afande mbona ameshtuka ikabidi afande aeleze
" jana usiku trafiki wetu akiwa barabarani aliisikia gari ya ramso ikitokea upande wa mashariki ikija kwa kasi barabarani trafiki ikabidi aisimamishe lakini ajabu mtu huyu aliondoa gari kwa kasi na kumkosa kosa kumgonga trafiki, trafiki akatupa taarifa hizo tukaweka ambushi na kumkamata ramso.... baada ya kumkamta tukampekua tukakuta akiwa na bastola kiunoni na ndani ya gari akiwa na koleo na ndomaana tukamshikilia" afande alimaliza kuwapa maelezo kina robbin, hapa kila kachero akaanza kumkodolea macho ramso kuwa ndio muhusika mkuu wa mauaji yaliyo fanyika , kina robbin walitoa taarifa ngazi za juu kuwa baada ya kufanya upelelezi wamefanikiwa kumpata mtuhumiwa mmoja ambae huenda atakuwa muhusika mkuu, R.P.C alishangaa sana taarifa ya kina robbin kuwa wameshamkamata mtuhumiwa mmoja , oda ikatoka kuwa ramso achukuliwe na apelekwe sehemu husika inayotumiwa na makechero kuwahojia na kuwatesa watuhumiwa wanaokutwa na tuhuma nzito mpaka wakili kuwa wamehusika kwenye mauaji.

makachero watatu wakaingia sehemu aliyohifadhiwa ramso wakamchukuwa akiwa na pingu wakampakia kwenye gari yao na kuondoa gari kwa kasi kuelekea sehemu maalumu wakafanye kazi yao,!
kupatikana kwa ramso kulianza kuwafanya makachero hawa wahisi kazi kuwa rahisi, kazi ambayo waliipata kupitia muheshimiwa Athony aliekuwa baba yake moody ambae tangu amezipata taarifa za kifo cha mwanawe alikuwa kama amechanganyikiwa na kumpigia simu R.P.C akimuuliza upelelezi wa makachero umefikia wapi!

kwa upande wa robbin bado aliona utata wa kesi ile upo kwani mazingira yanasema moody kabla ya kufa kuna tukio alitaka kulifanya na ndani ya nyumba kuna onekana kulikuwa na mwanamke, na ramso aliekamatwa alikuwa ni mmoja wa watu waliopigiwa simu na moody kabla hajafa, robbin akaona maswali yake yangejibiwa na ramso walie mkamata!

baada ya muda wa saa moja na nusu gari ya kina robbin ilfunga breki mbele ya jengo kubwa la serekali kati kati ya eneo hili bandela ya tanzania ilipepea, robbin akishirikiana na wenzake wakamtelemsha ramso na kumtembeza mpaka ndani ya jengo lile kisha wakamuingiza kwenye chumba kilicho kuwa na mwanga huku kukiwa na meza kubwa na viti ndani ya chumba hicho wakamkalisha ram kwenye kiti kimoja kilicho kuwa nyuma ya meza iliyo kuwa mule kisha wakafunga mlango na kuondoka kumuacha ramso peke yake akiwa na pingu mikononi.

woga ulikuwa umemtawala ramso muda wote alikuwa na kihoro cha mawazo mpaka hapo hakujua ni kwanini ameletwa eneo lile ,'au wamesha jua moody kauwawa' ramso alijiuliza bila kupata jibu ramso akiwa bado anajiuliza maswali mara mlango ulifunguliwa na kina robbin wakaingia wakavuta viti wakakaa mbele ya meza kumkabili ramso
"unaitwa nani kijana ?" kachero fadhiri aliongea huku akimtazama moja kwa moja ramso
"naitwa ramadhani au ramso" ramso alijibu kwa huku akijitahidi kuficha woga wake

"ni kwanini umemuua moody" fadhili aliuliza ,mshtuko mkubwa ukamkumba ramso mpaka hapo akajua kinacho endelea
"mzee ,..moody... ndo na..ni" ramso alijibu kwa kigugumizi
"wewe mjinga usitake kutopotozea muda ...taja wenzako uliokuwa nao kwenye mpango wa kumuua moody haraka na useme kwanini mlimuua" fadhili alifoka na kumuongezea ramso swali la pili
"mzee mbona mimi siwaelewi..." pah..kabla ramso hajamalizia sentesi yake veronica kwa wepesi alimnasa kofi lilomfanya ramso apate maumivu
"wewe usitake tuka kuua na kuanza kutafuta wenzako watakao jibu maswali yetu,jibu unacho ulizwa" veronica alifoka, lakini ramso alishikilia msimamo wake kuwa hamjui moody na ndipo makachero hawa walipo afikiana kuwa wamtese ramso mpaka aseme ukweli, maandalizi ya mateso yakaanza.

***
rebbeca alishtuka sana alipo pata taarifa kuwa moody ka uwawa ,rebbeca akahisi kuchanganyikiwa, kilicho mchanganya rebbeca ni kuwa usiku alio uwawa moody ndio usiku ambao mariamu aliitwa na moody, rebbeca akakumbuka siku hiyo usiku alipo mpigia simu mariamu mariamu alikuwa tofauti sana, hapo rebbeca akaanza kuhisi kuwa mariamu atakuwa ni moja ya sababu iliyopelekea kifo cha moody ,na kingine kilicho mfanya rebbeca aamini kuwa mariamu alikuwa kwenye balaa la kifo cha moody ni pale alipokutana na mariamu asubuhi na kumuona akiwa na bandeji juu kidogo ya paji lake la uso na uso wake ulikuwa mwekundu kana kwamba jana usiku alipigwa makofi, rebbeca akajua ni wazi mariamu atakuwa anahusika!

tangu mariamu aanze kuwa maarufu rebbeca hakufurahia kabisa mafanikio ya mariamu, na rebbeca moyo ulikuwa unamuuma kila akiyasikia malengo ya mariamu ya kuja kuwa miss tanzania, rebbeca akaona kwenye hii kesi ndo ilikuwa nafasi ya kuharibu ndoto za mariamu, rebbeca akapanga apeleke taarifa kituo cha polisi kuwa siku moody anakufa basi mariamu alikuwa kwa moody na walikuwa wana mahusiano..,


.....9....

ilikuwa inakaribia takribani masaa mawili tangu ramso aanze kuteswa na makachero watatu, muda huu hali ya ramso ilikuwa haitamaniki uso wake ulikuwa umevimba sababu ya kipigo magoti yalimuuma kumfanya ashindwe hata kusimama alikuwa amepigwa sana na virungu kwenye magoti yake, macho ya ramso yalikuwa hayaoni vizuri ktokana na kuvimba kwa uso na kumfanya awe na sura ya ya kuchekesha!
kama haitoshi makachero hawa walileta mifuko ya lailoni iliyokuwa maarumu kwa kazi ya makachero hawa, baada ya mifuko hii kuletwa makachero hawa wakamuinua ramso alie kuwa amelala sakafuni, waka mkarisha na kumfunga mikono yake pingu kwa nyuma kisha wakachukua mfuko mmoja na kukivisha kichwa cha ramso gubi gubi mpaka shigoni ,kichwa chote cha ramso kikawa ndani ya mfuko ule wa laironi kisha wakachukua kamba na kuifunga kwenye nyingo ya ramso waki ubana ule mfuko kwenye shingo ya ramso pasipatikane sehemu ya kupumulia wala tundu la kupitishia hewa ,baada ya kulifanya zoezi hili makachero wakamuachia ramso kichwa chake kikiwa ndani ya mfuko usio pitisha hewa, ramso akaanza kutapa tapa kwa kukuosa pumzi na kina robbin wakawa wanamuangalia anavyo tapatapa, pumzi ilimuishia ramso akawa anatamani awambie kina robbin ukweli lakini hakupata nafasi ile kwani alikuwa yumo ndani ya mfuko ,hatimae pumzi ya ramso iliisha ramso akajitupa chini na kuanza kugalagala akiashiria kuomba msaada lakini makachero wakamuangalia kama hawamuoni. hatimae ramso akaanza kutupa tupa miguu na hapo fadhili akatoa ishara kwa robbin na robbini haraka akaenda kuufungua ule mfuko na kuutoa kisha akakishika kichwa cha ramso kukikandamiza chini ramso akiwa amelala chali akivuta pumzi kwa mfululizo mara veroniica akaja na dumu la maji akaanza kummiminia ramso usoni kwa mfululizo,ghafla ramso akaikosa ilepumzi aliokuwa ameanza kuipata alivyo jaribu kuivuta akawa kavuta maji yaliyo pitia puani na kumpalia huku mengine yakipitia mdomoni ramso akapaliwa mfululizo na muda huo veronica akasitisha zoezi na kina fadhili haraka wakamuinua ramso na kumkalisha kwenye kiti kisha na wao wakavuta viti wakakaa kumkabili ramso "sikia ramso tunajua wewe umehusika na kifo cha moody tunachotaka ututajie wenzako ulioshirikiana nao usitu lazimishe tukuue" robbin aliongea huku akimkazia macho
"hapana wazee mimi siku husika na kifo cha moody ila kuna kazi moody aliniitia nyumbani kwake" ramso aliongea huku akitaka kulia hapo makachero wote wakawa makini kumsikiliza ramso
"wiki iliyo pita ramso alinifuata kwangu na kuniambia kuna kazi anataka nimsaidie ... alisema kuna mpenzi wake kazingua anataka kumua kisha akamfukie mbali na mji tukawa tumekubaliana kuwa atanilipa na mimi nitamsaidia kutimiza kazi yake.... ni jana usiku alipo nipigia simu na kuniambia kuwa huyo mpenzi wake yupo nyumbani akaniambia niende na koleo ili tuka kamilishe kazi yake, mimi ni kafunga safari nikiwa na gari langu nikaendesha mpaka mbezi kwa moody, nilipo fika nikafungua mlango na ndipo nikamuona moody akiwa chini amekufa ....mimi nikajua kesi inaweza kuniangukia nikaingia kwenye gari yangu na kukimbia na ndipo nilipo kamatwa na polisi kwa kosa la kumkimbia trafki" ramso alimaliza kusema ukweli wake, veronica na fadhili walipandwa na hasira na kuona kuwa ramso anawaongopea kwani wao walikuwa na uhakika kuwa ramso ndo muaji!
"huyu mjinga anatengeneza ushuhuda wa uongo" fadhiri alifoka
"no, yupo sahihi ...si mnakumbuka ndani tulikuta vielelezo vyakuwa kulikuwa na mwanamke kweli...na ni kweli moody alikuwa kwenye mpango wa mauaji na ndomaana mwili wake tuliukua uliwana grove" robbin aliongea kwa hisia kali za kipelelezi, maneno ya robbin yaliwafanya makachero wenzake waamini maneno ya ramso,
"inamaana kabla ya moody kufa alikuwa kwenye mpango wa mauaji ya mtu anae sadikika kuwa na mpenzi wake....mbona hii kesi ni ngumu" veronica aliongea kwa utulivu
"unamfahamu huyo mpenzi wa marehemu moody?" robbin alimuuliza ramso
"hapana wala siku wahi kumuona" ramso alijibu na kumfanya robbin ashushe pumzi ndefu mfululizo
"ok, kinachotakiwa ni kujua nani aliekuwa na mahusiano na marehemu moody" fadhili aliongea,
"ina bidi tufikishe kwanza hii ripoti kwa mkuu" veronica alitoa wazo, na wote waka afikiana na robbini akaanza kuiandika ripoti ile, na baada ya kuiandika wakampa ramso asaini ,baada ya taratibu zote kufanyika ramso akarudishwa kwenye chumba maalumu kwa watu wenye kesi kama yake na makachero wakaondoka kupeleka ripoti kwa R.P.C .

****

ripoti ya kina robbin ilimshtua sana mheshimiwa anthony na kuona mambo hayakuwa vizuri kwani ripoti ili onesha kuwa mwanae moody alikuwa kwenye harakati za kumuua mpenzi wake ambae bado hajajulikana, ripoti hii kwa upande wa pili ilikuwa mbaya kwa mheshimiwa. anthony aliona kama ripoti hii itawafikia waandisha wa habari basi ingekuwa ni kashfa ambayo ingeweza kutumiwa na chama pinzani kumvua madaraka anthony huku wakimpa tuhuma za kulea uharifu mpaka kufikia hatua ya mtoto wake kumiliki bastola na kupanga njama za kumuua mpenzi wake, ,hili swala likaonekana kumuweka muheshimiwa kwenye hari ya wasi wasi sana ! pamoja na yote muheshimiwa bado alikuwa na uchungu wa mwanae na alitamani sana muaji akamatwe kisha amfanye kitu ambacho muuaji huyo angejuta ,lakini tatizo hili la ripoti likaanza kumuumiza kichwa !

kina robbin walienda kupumzika kwa muda huku waki kubaliana kuwa watarudi mida ya usiku kwenye kituo walicho muacha ramso na,vilele usiku huu mida ya saa tatu watalamu wa kupima vinasaba (finger print) walitalajiwa kufika kwenye nyumba ya moody ili wajaribu kutafuta alama za vidole vya muuaji.
.....
robbin aliondoka akaenda nyumbani kwake na baada ya kuoga na kula akatoa camera yake akacho meka waya na kuonganisha na laptop yake kisha akaanza kuangalia kwa makini zile picha alizo piga kwenye nyumba ya moody huku akizichunguza kwa umakini, katika picha hizo ni picha moja moja alioitazama kwa makini na kuivutia picha, ilikuwa ni ile picha ya doa la damu kwenye ukuta, robbin alitambua fika pale ukutani itakuwa kuna mtu alibamizwa na kuumia kisha kubakiza damu ukutani, robbin alikumbuka mwili wa moody haukuwa na kovu usoni inamaana alie bamizwa alikuwa ni mtu anae sadikika kuwa ni mwanamke ambae wanamtafuta kwa tuhuma za mauaji , robbin akwa na dhana ya kuwa muuaji atakuwa na kovu kwenye uso japo hakuwa na uhakika , pamoja na yote kuna mambo robbin alikuwa amesha yahisi hayapo sahihi juu ya moody. robbin alijiuliza maswali mengi kuhusiana na moody, robbin akaona ramso ndo mtu pekee atakae mjibu maswali hayo na kumpa maelezo ya kutosha ,robbin akaamua awahi peke yake kituoni ili akamuhoji ramso akiwa peke yake na sio na wenzake kwani kuna mambo hakutaka kuwashirhkisha kina fadhili

haraka robbin akaanza safari ya kwenda kituoni ili akachukue maelezo kwa ramso yaliyo kuwa yanaumuhimu kwake.

robbin alishangaa baada ya kufika kituoni ,kwani alikuta hari tofauti! wakiwa wamezagaa kitu ambacho si kawaida na kabla hajauliza kuna nini akaona watu walio vaa makoti meupe wakiwa na machela iliyo beba mtu! robbin ikabidi aangalie yule mtu alie bebwa kwenye machela ni nani,
robbin alishtuka sana kwani mtu aliekuwa kwenye machela alikuwa ni ramso akiwa hajitikisi!
"kuna nini" robbin ali ropoka
"mtuhumiwa wenu amekufa ...inaonekana mlimtesa sana" polisi mmoja mwenye cheo alimjibu robbin, robbin akashtuka zaidi ya kushangaa kwani mateso waliompa ramso hayukuwa mateso ya kumsababishia kifo!


....10...

Kijasho kikamtoka robbin macho yake yakabaki yana usindikiza mwili wa ramso ukiingizwa kwenye gari la wagonjwa, vitu viwili vilimuumiza kichwa robbin, kwanza amekosa maelezo kutoka kwa ramso ambayo aliamini yangemsaidia ,pili alijiuliza sana kuhusu kifo cha ramso kwani wao walimuacha akiwa mzima kabisa japo alikuwa amechoka kwa kichapo sasa kimemkuta nini mpaka apate kifo cha ghafla ? robbin hakupata jibu na mara simu yake ikaita akatoa na kuangalia kwenye kioo mpigaji alikuwa ni fadhili, robbin akapokea
" robbin tukutane twende kituoni" fadhili aliongea kwenye simu
"nimesha fika kituoni na kuna tatizo sir"robbin aliongea kwa sauti iliyo iliyo pwaya
"tatizo gani" fadhili aliuliza na robbin ikamlazimu amuambie ukweli kuwa ramso amekufa.
hata fadhili alihisi kuchanganyikiwa ikabidi amuambie robbin kuwa amkute kituoni wa jadili!

timu nzima ya makachero wa tatu walikutana kituoni pale huku kila mmoja akishangazwa na kifo cha ramso na kila kachero akiwa na dhana yake juu ya kifo cha ramso ,wasiwasi wao ikawa nilawama kutoka kwa mkuu wao wa kazi na kwa mbunge athony ambae ni baba yake moody, wakiwa wanaendelea kujadili simu ya fadhili iliita na fadhili alishtuka baada ya kujua alipigiwa na mkuu wao wa kazi fadhili akapokea akiwa katawaliwa na nidhamu ya uoga "popote mlipo na wenzako nawahitaji ofsini kwangu haraka" hii ilikuwa sauti ya mkuu wa kazi wa kina fadhili na haraka kina fadhili wakaingia kwenye gari ambayo siku zote iliendeshwa na fadhili.

gari iliendeshwa kwa kasi na walifika haraka kwenye jengo la ghorofa kulipokuwa na ofisi ya r.p.c ,haraka wakapandisha ngazi mpaka kwenye mlango wa ofisi ya mkuu wao wakagonga hodi huku kila mmoja akiwa na hofu moyoni mwake "ingia" sauti ya bosi wao iliwakaribisha fadhili akafungua mlango akaingia akifuatiwa na wenzake ,walipo ingia ndani kila mmoja hofu yake ikaongezeka baada ya kumkuta mheshimiwa anthony akiwa na r.p.c mule ndani!
baada ya salamu makachero hawa walikaribishwa kwenye viti wakakaa
"mtuhumiwa wenu amekufa baada ya nyie kumtesa ...hivyo basi file lake limefungwa hata maelezo yake yamefutwa mnaanza upya upelelezi wenu, mnatakiwa kuchunguza ni nani alie muua moody na sio kujua nini kilitokea kabla ya kifo cha moody" mheshimiwa anthony aliwaeleza kina robbin akimaanisha kuwa ile ripoti ya kuwa moody kabla ya kufa alikuwa na mpango wa kumuua mpenzi wake,ripoti hiyo imefutwa na sasa walitakiwa kujua ni nani alie muua moody na kuchunguza ni msichana gani nchini alikuwa na mahusuano ya kimapenzi na moody.
baada ya kupokea maeleyo hayo waliruhusiwa kuondoka huku kila mmoja akishangaa utaratibu huo na kujiuliza kwanini hawakulalamikiwa juu ya kifo cha ramso....

ni muheshimiwa anthony alie husika na mauji ya ramso baada ya kuona maelezo ya ramso yangeweza kuleta kizaazaa kipya cha wanasiasa wenzake kumshtumu kuwa mwanae alikuwa muhalifu na kumiliki bastola, anthony alimtuma polisi aliempa ramso chakula chenye sumu na kuyaondoa maisha yake, na sasa anthony alikuwa anasubiri kwa hamu kujua ni nani alie muua mwanawe na ni nani aliekuwa na mahusiano na mwanawe!

***

hali ya mariamu kisaikrojia haikuwa nzuri hata kidogo tangu alipo muua moody, mariamu hakuwa na amani muda wote alihisi kukamatwa na polisi . kitu kimoja kilimtia mashaka mariamu ni juu ya siku ile ya tukio akiwa amesha muua moody na yeye akiwa bafuni alisikia muungurumo wa gari likiondoka kwa kasi nje mariamu hakujua ile gari ilikuwa ya nani , macho ya mariamu yakawa ni macho yenye aibu na ya uoga kila alipokutanisha macho yake na mtu wa aina yoyote hii ikampelekea muda wote awe amevaa miwani nyeupe kanakwamba alikuwa na matatizo ya macho, juu ya paji la uso la mariamu alikuwa na plasta ndogo iliyo ziba pale alipo bamizwa ukutani na marehemu moody, muda wote mariamu alikuwa mtu wa mawazo kitu ambacho kilimpelekea atumie kwa wingi pombe kali, mariamu alimpenda sana moody tofauti kabisa na moody alivyo fikiria, moyo ulimuuma sana mariamu kwa kujikuta amemuua mpenzi wake ambae kwa njia moja au nyingine walikuwa wametoka mbali na alikuwa amefanikisha kutimiza ndoto yake ya kuwa msanii , kuna wakati mariamu alihisi kapoteza mwanaume aliekuwa ni mtu sahihi kwenye maisha yake lakini kila mariamu alipokumbuka kuwa moody alitaka kumuua mariamu alijipa moyo na kusema "alianza mimi nikamaliza ". usumbufu wa kupigiwa simu mara kwa mara na wasanii wenzake hasa tino ambae kila siku alimbembeleza mariamu kumwambia anampenda na kumtumia sms kila wakati ,pamoja na mialiko ambayo mariamu alishindwa kabisa kuweza kuhudhuria, kukamfanya mariamu azime simu asipatikane kabisa hewani .mariamu akawa anaishi maisha yasiyo na amani hata kidogo akatamani arudi kwao lakini akajikaza na kuendelea kuishi pale alipo panga.. rebbeca nae kila muda alienda kwa mariamu akidai ameenda kupiga nae stori ,mariamu alimshangaa sana rebbeca kwani rebbeca hakuwa na kawaida ya kumtembelea mara kwa mara na kushinda nyumbani kwake, mariamu akashindwa kujua imekuaje rebbeca aende kumtembelea mara kwa mara kupita kiasi ,hata mara moja rebbeca hakuwahi kumuuliza mariamu juu ya moody kitu ambacho kilimfanya mariamu ajue kuwa rebbeca hajui kama moody amekufa, masikini ya mungu mariam alikuwa anajidanganya hakujua kwamba rebbeca alikuwa na mpango mbaya wa maisha yake! kwani rebbeca alikuwa akienda kwa mariamu kwa ajili ya kuchukua vitu muhimu pamoja na picha ambazo mariamu alipiga na marehemu moody, rebbeca alichukua vitu hivyo kama ushahidi kwa polisi kuwa mariamu alikuwa nauhusiano wa kimapenzi na moody, amahakika rebbeca alikuwa mtu mbaya kwa mariamu.

haiku chukua sana muda rebbeca akawa amefanikiwa kuiba picha za marimu zilizo muonesha mariamu akiwa na moody na sasa rebbeca alikuwa na mpango wa kuzipeeleka polisi .....

No comments:

Post a Comment

Iblame my body

RIWAYA   : I'BLAME MY BODY ( NAULAUMU MWILI WANGU ) Imezaminiwa na   Simulizimahiri.blogspot.com Mahakama kubwa ya kesi za jina...