Saturday, October 22, 2016

sophia

simulizi :sophia
mtunzi: iddi siraji
0746206428 WHATSUP
ilipo ishia...
donge zito lika mkaba kooni akashindwa hata kuipokea simu  kilio cha sauti kikataka kumtoka akijikaza na kuya ruhusu machozi yatiririke..
simu ikakata na hapo sophia akapiga hatua kwenda kwenye ule mlango aufungue atoke nje kufanya maamuzi ambayo aliyaona ni sahihi kwake ...
simu ilianza kuita lakini safari hii sophia hakurudi nyuma  alikwenda kuufungua ule mlango wadharula akajitupe
endelea....
alishika kitasa cha mlango ule wa dharula na kukinyonga kwa nguvu  na kuufungua ule mlango lakini hapo hapo alisikia mtu akibisha hodi kwenye mlango ambao ni mahususi kwa ajili ya wodi ile,sophia akawa ametambua kua aliekuwa ana bisha hodi ni muhudu alie kuwa dhamu usiku sophia akawa anajiuliza akamfungulie au atokee mlango wa dharula akafanye maamuzi yake kabla hajaamua cha kufanya macho yake ya liona kitasa cha mlango wa kawaida kikitikisika hapo sophia akajua muhudumu anaingia  ndani ikamlazimu sophia apige hatua za haraka na kurudi kitandani akatoa haraka ile barua kwenye meza na kuirusha uvunguni kisha akajilaza na muda huo simu yake ilikua ina endelea kuita...
milango ya wodi hua haifungwi hivyo muhudumu alivyo gonga mlango bila kuitikiwa ikamlazimu kuingia ndani huku jasho likimtoka !
"hey sophia umelala simu yako inaita" muhudumu huyo aliongea huku macho yake yakionekana kutoka kwenye usingizi wa muda mfupi..
"sophia" aliita tena
"aaaagh ah madamu Glory" sophia aongea akijifanya katoka usingizini
"dada sophia simu yako imeita sana ..." glory aliongea huku akisogea na muda huo simu ikakata kwani iliita kwa muda mrefu..
"ah nilikuwa kwenye usingizi mzito siku isikia" sophia aliongea huku kukata kwa simu ile ikiwa ni ahueni kwake.. glory alisogea na kukaa juu ya meza kumkabili sophia ambae tayari alishainuka na kukaa kitako kitandani pale.
ajabu glory hakuongea kitu ila alimtazama usoni sophia kwa muda!
"dada kuna nini mbona umeniangalia hivyo.." sophia alihoji kwa kushangaa
"sura yako inaonesha ulikuwa unalia  na macho yako hayakuwa kwenye usingizi hata kidogo ..." glory aliongea huku akiendelea kumtizama sophia
"hapana dada kweli nilikuwa nimelala....ulikuwa una fanya nini mbona unajasho dada glory" sophia alihamisha mada
"ngoja nikwambie kweli....
nilikuwa nimeptiwa na usingizi wa muda mfupi lakini nikiwa Karina usingizi nimeijiwa na ndoto mbaya
"ndoto gani dada glory"
"nime ota kuna wodi inawaka moto mkubwa usiozimika na kuna mnyama mkubwa wa aina yake mwenye uwezo wa ajabu akimnyemelea mgonjwa aliekuwemo ndani ya wodi hiyo inayo waka moto " glory akamezamate kisha akaendelea
"lakini ndani ya chumba hicho kuna kengele inapiga mfululizo kisha sauti ya kengele hiyo ikawa inaumiza kichwa changu . nilipo shtuka kutoka usingizini nikasikia chumbani mwako simu yako ikiita kwasauti jasho ndomaana nimekuja kukuamsha jasho likinitoka"
maneno haya yalimshtua sana lakini akajikaza
"ah hapana dada ni ndoto hutu ... ndoto huja mtu anapokuwa na mawazo mengi "
sophia alimzuga glory huku moyoni akijiuliza glory alikuwa mtu wanamna gani
muda huo wakati glory akimtazama alifanikiwa kuona michirizi ya damu kwenye mkono wa sophia na kisha macho ya glory yakaangalia juu kwenye chuma iliyo ning'iniza dripu ambayo bado ilikuwa haija kwisha hii ikamfanya glory ashituke .kama dripu ilikuwa imeisha kwenye  asinge pata mashaka lakini  dripu ilikua haijaisha hii ilimaanisha sophia alichomoa ile dripu na kuna kitu alikusudia kukifanya..
"niambie kwanini umechomoa dripu" glory alimuhoji kwa ukali kidogo huku sura ya glory ikiwa imeanza kubadilika . swali hili lili mshitua sana sophia
"ah doctor aliniambia nikijisikia vibaya niichomoe"
"hakuna daktari mpuuzi wa kukuambia hvyo daktari gani huyo"
"madam Nasra"
sophia alimsigizia nasra ambae hakuwepo muda huo.
na  kabla glory hajauliza uliza tena ghafla upepo ulivuma nje na kwakuwa ule mlango wadharula hakufungwa vizuri na sophia ulifunguka wote wakashtuka na kuangalia na hapo glory akapata kujua kulikuwa kuna kitu cha hatari katika wodi hii usiku huu..
"ah madam nasra kasahau kuufunga huu mlango wa dharula alitumia kutolea maboksi ya dawa kabla hajaondoka"
sophia alionganisha uogo wake na kumshtumu nasra bila kujali
"inamana alitoa kima gendo"
"nafikiri" sophia hakuwa na wasi wasi juu ya kumhujumu nasra kwani yeye binafsi alijua wazi asinge liona jua la siku inayofuata ilikuwa lazima ajiondoe katika ulimwengu usiku ule..
glory aliinuka na kuufunga ule mlango wa dharula huku moyo wake ukiwa umeanza kumshutumu nasra akiamini kweli nasra alitoa maboksi ya dawa kimagendo kupitia mlango wa dharula wa wodi ya sophia , maskini ya mungu glory hakujua kwamba kaongopewa na sophia...
"ok lala sophia kesho tukijaliwa " glory alimuaga sophia na kutoka nje.
Sophia akashusha pumzi huku akaichukua simu yake akaizima asipatikane hewani.kisha akaichukua ile barua akaiweka mezani kwa mara nyingine...
"nisamehe madamu nasra nisamehe glory nisamehe GIKA" alisema sophia
upande wa gika...
wakati yale yote yakiendelea gika alikuwa ndani ya ofisi ya daktari wa magonjwa ya figo usiku ule  akiwa katika maandalizi ya kufanyiwa opareshen!
"kijana wangu gika upo tayari kwa hili tunalo kwenda kufanya usiku huu" daktari mwenye umri wa makamo alimuuliza Gika huku akimtazama kwa kumchunguza
"ndio mzee nipo lidhaa" gika alijibu
"wewe ni kama mwanangu hakuna baba ambae angekubali kumruhusu mwanae wa wa kiume atoe figo yake na ampe mpenzi wake ambaye anatakiwa awekewe figo"
"lakini doctor naamini baba yangu anaweza kutoa figo kwa ajili ya mama iwapo mama atakuwa anaugonjwa wa figo"
"lakini gika sophia sio mke wako na aliwahi kukusaliti" daktari alizidi kumuweka sawa ili gika aachane na wazo la kuitoa figo yake kwa ajili ya sophia alie kuwa taabani akihitaji huduma ya kubadilishwa figo
"kila kosa husamehewa hakuna kosa jipya duniani hapa sophia nilisha msamehe na naya saidia maisha yake kisha tukaanzishe familia bora"
"iwapo utakufa katika oparesheni hii" daktari alimuuliza kwa sauti ya chini
"itakuwa baba amekufa katika harakati za kumsaidia mama..na mama atabaki mzima akisimulia wema wa gika kizazi na kizazi" gika aliamua kumaliza na kumkatisha tamaa daktari juu ya wazo lake la kuzuia
"ok nani atakuwa shahidi wako wa kusaini hii oparesheni hii" daktari ali uliza na kumfanya gika anyongee kwani gika katika hili hakutaka kumshirikisha ndugu ata rafiki mmoja kwa alijua wazi wange mpinga
"ni mimi na wewe doctor ... muonee huruma sophia kama nikuoneavyo mimi usinipinge baba yangu" gika aliongea kwa upole kisha akavuta karatasi ilio kuwa mbele yake na kuitia sahihi yake!
"ok heri mwenye moyo safi.... umekuwa na moyo wa ajabu kijana" daktari aliongea huku nae akiichua ile karatasi akatia sahihi yake na kuibana ile karatasi kwenye file.
"saa saba kamili usiku huu utaingia kwenye chumba cha opareshin mpaka saa tisa opareshen itakuwa tayari kisha itafuatia kwa sophia"  aliongea daktari moyo wa gika ukapata furaha gika akaitazama saa yake ya mkononi..
"bado dakika thelathini na tano.. acha nikapige simu dakika kadhaa" gika alisema
"ok najua unaenda kuogea na sophia...ok maandalizi mema" daktari alisema huku akitabasamu
"gika nae akatabasamu nakutoka nje kwenda nje kupiga simu..
gika alipiga simu lakini hakupokelewa !
(ulikuwa ndo ule muda ambao sophia alikua anataka kufungua mlango wa dharula"
gika akapiga tena lakini hakupokelewa tena...
(ndo ule muda glory alio amka na kumfunguza sophia..)
gika akarudisha simu mfukono na kwenda carteen akisubiri muda wa opsresheni...
saa saba kamili usiku kwa moyo mmoja na upendo wa ajabu gika aliingia kwenye chumba cha oparesheni ambako alikutana na jopo la madakari na bila kupoteza muda oparesheni ilianza..
saa tisa na dakika kumi uparesheni ilikuwa imefanyika na na kundi la wahudumu lilitoka kuelekea ilipokuwa wodi ya sophia ili wampeleke chumba cha oparesheni ili abadilishwe figo awekewe ya gika!
walimkuta glory na kumpa taarifa kwamba wanamchukua sophia akafanyiwe mabadilisho ya figo ..glory alishangaa sana kusikia gika amesha tolewa figo na hapo !
glory akampa file kiongozi wa wahudumu hawa akasaini glory akawaaongoza kwenye wodi ya sophia..
glory aliingia kwenye wodi ya sophia na kumuona sophia akiwa kalala kwenye sakafu!
"dada sophia!" glory aliita huku moyo wake ukipinga
kimya!
glory haraka akamsogelea sophia pale na kumuita huku akimtikisa ...
macho yalimtoka glory baada yakuona kisu sakafuni kikiwa na damu nchani kisha akaona kijeraha kidogo kwenye mkono wa sophia akapeleka sikio lake kifuani mwa sophiaa.....
hapo yowe kubwa likamtoka glory...
sophia hakuwa tena dunia hii alikua kajiua kwa kujikata mshipa mkuu wa damu katika mkono wake wa kushoto.....
itaendelea...
share ili upate mwendelezo

No comments:

Post a Comment

Iblame my body

RIWAYA   : I'BLAME MY BODY ( NAULAUMU MWILI WANGU ) Imezaminiwa na   Simulizimahiri.blogspot.com Mahakama kubwa ya kesi za jina...