Sunday, November 27, 2016

MUHANGA

riwaya : Muhanga
What,sup: 0746206428
Cover: SIMULIZIMAHIRI.BLOGSPOT.COM
     

       LIBERIA  GBARNG

Yowe kubwa lilisikika na kusababisha magwi mkubwa katika jengo moja la jeshi liliopo mji wa Gbarng ndani ya nchi ya Liberia huku sauti za watu zenye rafudhi ya ki liberia zikifoka na kuendelea kumtesa mtu alie endeleza kupiga mayowe huku matusi ya kiswahili yakimtoka bila mpangilio.
kama  ni wewe msomaji ungesikia yowe lile na matusi yale ungeweza kujua aliekuwa akiteswa waliberia wale alikuwa ni mtanzania halisi!
"muachenini muda wake wakuteswa vizuri bado hujafika mfungeni tukamuite boss" mliberia mmoja alie valia nguo za jeshi la liberia aliongea na mwanajeshi mwingine akachukua kamba na kumkalisha kwenye kiti mtanzania alie tapakaa damu na majeraha kadhaa kwenye mwili wake ambayo kwa hakika yalikuwa ni majeraha ya risasi.
mwenajeshi yule alimfunga mtu yule ambaye bila shaka alikuwa ni mateka wao ,alimfunga ki ustadi kwenye kiti kile alipo maliza kumfunga akampiga ngumi nzito ya kifua  mguno wa maumivu ukamtoka mtanzania.
"tayari tuondokeni tusije kumua kabla ya boss kufika" alisema

Baada ya kuachwa kwa muda akiwa kwenye kiti kafungwa kwaustadi mkubwa  kwenye kichwachake kikiwa kimeinamia moja kwa moja kifuani pake ambapo pametapaa damu na kufanya tshirt aliyo ivaa iogepeshe kuitazama , alikuwa kimya wala mwili wake haukutikisika ungeweza kusema amekufa . akili na mawazo yake havikuwa eneo lile alicho fikiria ilikuwavni jinsi ya kujikoa kutoka mahabusu ile mahabusu iliyo jaa kila dalili za umauti. mawazo yake yalikatishwa na sauti ya hatua za watu walio kuwa  kwenye kolido wakija chumba alicho kuwa yeye
"they coming"  alijisemea moyoni huku presha yake ikipanda kwani alikuwa anajua kilicho kuwa kina fuata .alitulia vile vile kichwa chake kikiwa bado kime angukia kifuani .
alisikia sauti ngeni ya kijeshi ikiamulu kwa lugha iliofanana na kiarabu  na hapo akasikia kufuri la chumba likifunguliwa  akili yake ikampa kuwa askali walikuwa wamekuja na mkubwa wao . hakujitikisa wala kuinua kichwa na mara alihisi wapo mbele yake
"ame kufa..." mwanajeshi wa ki liberia aliuliza kwa lugha yao
mmoja wa maaskali  alichukua ndoo yenye maji na kummwagia 
"ni mzima afande huyu ..." alisema askali alie kua kavalia tishirt ya kijeshi na  suruale yake, kisha akaitupa ile ndoo pembeni .
kisha yule mwanajeshi alieonekana kuwa mkubwa alipiga hatua na kuvuta kiti kingine na kukaa mbele ya mateka wao na kumkabili sawa sawa uso kwa uso  kisha akawapa ishara wamtoe kile kitambaa cheusi usoni .
askari mmoja akasogea na kukitoa kile kitambaa na hapo macho manne yalitazamana sambamba baina ya  mateka huyu mtanzania na mwanajeshi wa ki liberia kwa sekunde mbili..
"now you see the light?"
"or you see my face?" aliongea mwajeshi yule wa ki liberia huku akimtazama mtazania alie mbele yake
"hapana hujaona chochote ila kifo! naam kifo kipo mbele yako kina subiri sekunde ifike kichukue nafasi yake" aliendelea kuongea kwa lugha ya kingereza ,alinyamaza kidogo kisha akaendelea....
"watu wana lia watoto wanakufa jeshi la nchi ya liberia linapoteza wanajeshi wake kila kukicha kwa kupambana na waasi ambao wanapata  msaada kutoka kwako na wenzako wengine. kwa tamaa ya pesa mnawa uzia silaha" maneno haya yalimshtua  mtanzania huyu aliekua kafungwa kwenye kiti kwani hakuelewa maada alie iongelea mwanajeshi wa ki liberia
"unajua silaha mnazo wa uzia waasi zimeua wanajeshi wangapi? zime ua watoto wa ngapi? na nifamilia  ngapi zime sambalatishwa kwa vita vina vyo endeshwa na waasi wanao tumia siraha mnazo wauziampaka sasa una shilingi ngapi kwenye akaunti ambayo umeeipata kwa kuuza siraha na . na angekuwa mtoto wako amekufa kwa kuuliwa waasi kwa siraha ulizo uza mwenyewe hiyo pesa inge rudisha uhai wa mwanao?" aliuliza mfululizo kwa sauti huku akaikunja kunja tshirt ya mateka yule na kumtikisa kwa nguvu na hali hii ilimuogopesha mtanzania..
"unacho cha kulipa kwa matatizo mnayo tuletea ?" mliberia aliuliza tena huku akimkazia macho . mtanzania alitikisa kichwa kukataa
"nani jina lako" mwanajeshi aliuliza . na muda wote aliongea kwa lugha ya kingereza kwani ndo ilikuwa lugha pekee ya kuongea na mateka wao ambae hawa kujua taifa lake
"unaitwa nani"
"hassani  " alijibu kwa sauti iliyo kwaruza. hapo wale wanajeshi wengine waliangaliana kwa wao wali mpiga sana hakusema jina wala taifa lake .
"vizuri kijana. naitwa mustaph" aliongea kwa kushusha pumzi na kijitambulisha kwani aliamini mateka wake anaenda kujibu maswali yake japo alihisi kuongopewa jina.
"hivi unahisi tukikutesa ukafa kisha mwili wako ukafukiwa kwenye aridhi ya liberia unafikiri nani ata peleka taarifa hizi kwenu unazani ndugu zako watajua umepotelea wapi?" mwanajeshi mustaph aliuliza na mtanzania aliejitambulisha kwajina la hassani alitingisha kichwa kumaanisha wasinge pata taarifa .
"sisi hatukuhitaji sana wewe hivyo tuna muhitaji mtu alioko nyuma yako . nani alie kutuma unatokea nchi gani?" mustaph aliuliza kwa utulivu . hakuna jibu lolote alilopata kutoka kwa hassani.

kimya!

kimya kikapita..
"where you come from " ali uliza tena kwa utulivu swali hili lilikuwa gumu kwa huyu mtanzania kwani alijua madhara  ya kutaja nchi yake na lazima nchi yake ingemkataa ..(swala ni kwamba aliingia  hata yeye mwenyewe amejikuta kaisha ingia kwenye janga hili bila kutaraji baada ya ku wrong order)
"kijana jiepushe na matatizo ..nakuuliza unatokea wapi"
mustapha aliuliza kwa sauti ya juu
"bwana hili swala halihusiani na nchi yangu na wala mimi sio muuza siraha nyie...." hassan aliamua kuropoka lakini kabla haja malizia sentesi yake kwa wepesi mustaph alisisima na kumshindilia teke la kifua na kumtupa nyuma hatua tatu akawa chini na kiti chake alicho fungiwa..
muda huo huo mustaph akamfuata palepale chini na kuchutama pale alipo anguka chali.
"sasa utasema"  mustaph aliongea huku aki peleka mkono wake kwenye bega la hassan palipokua na jeraha na kuingiza kidole dumba chake kwenye jiraha la risasi begani mwa hassani..
yowe kubwa lili mtoka hassani kwa maumivu makali aliyo yapata nusu aongee kiswahili lakini aliji control na kuugulia maumivu yale kwa kupiga mayowe hakuhitaji wajue taifa lake hata kidogo..
"nani boss wako na unatokea wapi?"

hukujibu

"hassan hua hatuna muda wa kupoteza ... sekunde chache zijazo utakuwa maiti katika aridhi hii ya liberia..
"bora nife kwani mimi sihusiki na biashara za siraha na siwezi kuihusisha nchi yangu kwenye tuhuma hii. mnani lazimisha ni kubali na wakati hamkunikamata na ushahidi wa kuwa mimi nilikuwa nauza siraha" hassani alijieleza..
"wewe ni jeuri.. kwahiyo bora ufe  enhee?" mustaph alisema huku akiingiza mkono mfukoni
"ndio ni bora mniue" mtanzania hassan alisisitiza akiamini kuwa wasinge weza kumuua
"vizuri hasani" mustaph alisema na muda huo alitoa mfuko maarumu na raba bendi kisha  akamvika kichwani ule mfuko mweupe wa prastiki kisha akuchukua raba bendi na kuufanga ule mfuko maeneo ya shingoni ili isipite hewa ,alifunga kwa ustandi na kwakuzungusha shingoni, kichwa  cha hassani kilikuwa ndini ya mfuko wa plastic ambao haupitishi hata chembe ya hewa...
"leo unakufa kifo unacho stahili" mustaph aliongea na kuamulu wana jeshi waondeke wote mule ndani ili mateka afe kifo alicho stahili.

mtanzania huyu hakuamini kilichokua kinatokea pumzi ilikuwa inakata na kwa shangao mkubwa macho yake yakiwa ndani ya mfuko ule alimuona mustaph na wanajeshi wengine wakiondoka mle ndani na kutoka nje . kisha mstaph aligeuka na kumpungia mkono wa kejeli  na kuufunga ule mlango wa mahabusu ndogo ..mustaph hakugeuka tena aliondoka..

Alitamani amuite  amueleze ukweli lakini ikawa ngumu kwake.

Pumzi ilikita macho yake yakavamiwa na kiza akajaribu kuzuia hali ile lakini ikawa kazi bure  picha ya msichana nzuri wa tanzania ikipita kichwani mwake  'mpenzi wangu nakufa'  nafsi yake ilikiri na hapo hakuona tena kila kitu kwenye mwili wake kikazima.

HII NI RIWAYA YANGU AMBAYO ITAWAFIKIA HAPA 2017 MWANZONI NA HUENDA IKATOKA KITABU.  SHARE KWA AJIRI YA MAANDALIZI MEMA YA RIWAYA HII.

0746206428

No comments:

Post a Comment

Iblame my body

RIWAYA   : I'BLAME MY BODY ( NAULAUMU MWILI WANGU ) Imezaminiwa na   Simulizimahiri.blogspot.com Mahakama kubwa ya kesi za jina...