Monday, November 14, 2016

SIMULIZI: DHIKI

MTUNZI   :iddi siraji

Naitwa iddi siraji, miaka kumi iliopita nilijikuta nikikosa tumaini la maisha na nikipoteza furaha kama waliyo kuwa nayo binadamu wenzangu nilitamani mtu yoyote atokee anishike mkono lakini hakuwahi kutokea na matatizo yakazidi kuniandama matatizo tabu na shida vikawa ni sehemu kubwa ya maisha yangu hii ilinifanya niamini kuwa mungu ananichukia anauchukia uwepo wangu kwenye dunia hii. ndio msaada wa mungu ulikuwa mbali na familia yetu,,,,,unaweza sema nakufuru lakini labda nikikusimulia simulizi ya maisha yangu utaona nipo sahihi katika haya nisemayo,,,,
2006 TABORA
Nilishtushwa kutoka usingizini na matone ya maji ambayo yalini dondokea karibu mwili wangu wote haraka niliamka nikagundua kuwa kulikuwa na mvua kubwa iliyo kuwa ikiendelea kunyesha niliamka haraka nakuanza kupapasa huku na kule nikiwa katika ya giza na katika kupapasa nilifanikiwa kupata toch yangu , nikaanza kuiangakia juu ya kuiwasha maana ilikuwa mbovu mbovu , nilifanikiwa kuiwasha ikatoa mwanga mkali na mara hapo hapo mwanga ukaanza kufifia..
niliangaza na kusogea kwenye kona moja ya.
Chumba nilichokuwemo kona hii
kipande kidogo juu ya paa
nilikuwa nimeenze matawi ya
mahama hivyo palikuwa hapa
vuji nilijisogeza kwenye kona
hiyo na kukaa na kujikunja kwa
ukiwa mkubwa sana na mawazo
mengi juu ya maisha yetu
magumu,. niliinua macho na
kutazama za kuta za chumba kile
zilikuwa ni kuta za miti na
udongo ,na kulikuwa na matobo
yenye uwazi katika kuta hizo
ilikuwa ni nyumba yenye chumba
kimoja na ilikuwa ya zamani ila
ilikuwa imara sana tatatizo la
chumba kile ilikuwa inavuja
sana wakati wa mvua....
Mara ghafla mawazo yangu
yalikatishwa na sauti ya
kugongwa kwa mlango wa
chumba kile kutokea nje ..haraka
niliinuka bila kuuliza ni nani alie
kuwa akigonga nikatoa mti
uliokuwa umeegemea kwenye
mlango na ndo mti huu ulikuwa
umezuia mlango usifunguke ,.
Baada ya kutoa mti huu niliinua
mlango na kuweka pembeni,
hapo hapo nilishtuka kidogo na
nikapatwa na fedheha baada ya
kumuona mama yangu akiwa
kalowa kiasi
"he! mama" niliongea huku
nikimshika mkono aingie
ndani,,,,,"mhh mwanangu nimeamua kuja
humu mwako mvua ni kubwa na
na ule ufa wa nyumba yangu
nimeona kama umeongezeke
tusije tukadondokewa na ukuta
" mama aliongea
mfulululizo na maneno yake
yakanitia simanzi moyoni "ah
hawa mafundi walitutapeli sijui
ndo walijengaje hiyo nyumba"
niliongea huku nikalaani mafundi
walio tujengea"tuna muachia
mungu mwanangu" mama
aliongea kwa unyonge huku
akijisogeza sehemu ambayo
ilikuwa haivuji, nili muonea sana
huruma mama akiwa na mdogo
wangu mgongoni na muda huo
mama alikaa kitako chini pakavu
na kumshusha mdogo wangu
kutoka mgongoni (mdogo huyo
alikuwa anaitwa mussa na
alikuwa ana miaka mitatu
kasoro )
Muda huo niliegesha tena ule
mlango wa chumba kile kisha
nikaanza kutafuta sehemu nzuri ya
kuweka toch ili iangaze mule
ndani na muda huo upepo mkali
ulianza kuvuma na upepo huu
ulipenya ndani kupitia matundu
yenye uwazi mkubwa yaliyokuwa
kwenye kuta za chumba kile,,
"mwanangu mdogo wako
amekamatwa na ugonjwa wake
wa pumu" nilimsikia mama
akiongea kwa sauti nami haraka
nilipiga hatua kadhaa na kusogea alipo kuwa mama na kumuona mdogo wangu aki hangaika kuitafuta pumzi, hii ilisababishwa na upepo mkali uliovuma"hii mitihani ya mungu ,, dawa yake nimeiacha mule ndani mwangu,,, mshike mdogo wako niendee" mama aliongea akitaka anipe mtoto"hapana mama acha niendee mimi""haya mwanangu ipo kwenye tandiko karibu na nipo chagamiaga,,,," kabla mama haja malizia kuongea kilisikika kishindo kikubwa nje ya chumba tulichokuwemo, mimi nikaruka pembeni kwa uoga mkubwa na kukaa chini . kishindo kilikuwa kikubwa mno,,,
"ni nini hicho" mama aliuliza kwa hamaki
mi nilibaki kimya lakini muda huo huo nikakumbuka kuwa nilitakiwa nikalete dawa ya mdogo wangu ya pumu , haraka niliinuka na kujisogeza mlangoni nikachungulia kwenye moja ya tundu ukutani nilikutana na kiza kizito na kupata tabu kutazama lakini muda huo huo radi ilimulika na kuleta mwanga mkubwa nilitazama palipokuwa na nyumba yetu lakini ajabu ni kwamba sikuiona nyumba yetu niliona tu kitu kama kichuguu kidogo!!
Lahaula! Nyumba yetu ilikuwa imeanguka Kumbe kile kishindo tulicho kisikia ni nyumba yetu ilikuwa imeanguka
"mama nyumba yetu imeanguka mama" nilijikuta nikiongea
Lakini mama hakujibu chochote kamya!
Haraka nikageuka alipo kuwa mama na hapo nilimuona mama akiwa busy na mdogo wangu ambae alikuwa anatapatapa kwa pumu....na dawa yenyewe ndio ilikuwa kwenye ile nyumba iliyo anguka ..
Nilimsogelea mama alipokuwa na nilimuona mama machozi yakimtoka akihangaika na mdogo wangu . Hapo hapo wazo lilinijia la kumsaidia mdogo wangu
"mama niende kwa mama pendo atakuwa na dawa nikamfunguze" niliongea huku nikiinuka
"sawa mwanangu fanya haraka tumsaidie mdogo wako" mama alijibu na muda huo nilikuwa nikitoka nje bila kujali mvua giza na upepo mkali , nikuanza kukimbia kuelekea kwa mama pendo,...
Mama pendo alikuwa ni mama aliekuwa akiishi kijiji kile kile tulicho ishi na alikuwa ni nesi wa zahanati yakijiji jirani na alikuwa akifahamiana na mama hivyo safari yangu ilikuwa ni kwenda kuomba msaada kwa huyo mama nakulikuwa na umbali wa mrefu kidog...
Kijiji kilikuwa kimya mvua kubwa ikiendelea kunyesha nikiwa peke yangu katika mvua ile na giza kubwa la kutisha huku nikibahatisha bahatisha njia na mara moja moja radi ilimulika na kufanya kutokee mwanga na kisha giza kutawala tena, mpenzi msomaji sito sahau usiku huo kwani ilikuwa ni giza la kuogepesha lakini sikuwa na woga nilikuwa najaribu kuokoa maisha ya mdogo wangu...,
Niliku nakimbia mchakamchaka nikijaribu kuwahi kwa mama pendo ., nikiwa katika kukimbia nilianza kusikia sauti za maji na hapo nikatambua kuwa nilikuwa nimekaribia kwenye kijito ambacho ukikavuka ndio unafika kwa ma pendo , niliongeza mwendo wa mchaka mchaka .
Nilipo fika sehemu ya kuvuka siku amini macho yangu!
Mbele yangu kulikuwa na mto mkubwa na sauti za maji zilitawala sikuamini kuwa mvua hii imeweza sabisha mto ufurike...
Nilisimama kwamuda lakini nilipo kumbuka hali ya mdogo wangu niliamua kuchuku mti mrefu nakujaribu kuuvuka mto huu huku nikichoma choma mti nijue wapi parefu na wapi pafupi, nilisogea taratibu huku ule mto ukiendelea kupitisha maji kwa kakasi nilijitahidi na kupiga hatua ka tisa lakini maji yale yalikuwa na nguvu na nilipo jaribu kuendelea nilijikuta nikipoteza stamina baada ya mguu wangu wa kushoto kukanyaga kwenye kijishimo, maji yalini zidi nguvu nikajikuta nikielea na kusombwa na maji ! nilijaribu kupiga kelele lakini maji yali ingia mdomoni nikashindwa, maji yalinipeleka kwa nguvu huku nikitapa tapa kujiokoa, ghafla kitu kigumu mithiri ya jiwe kilinigonga kwa nguvu kwenye paji la uso nikapata maumivu na muda huo nikahisi giza zito picha ya mama ikipita kichwani kwangu na giza zito likakubika taswila yangu ....itaendelea..
0746206428

No comments:

Post a Comment

Iblame my body

RIWAYA   : I'BLAME MY BODY ( NAULAUMU MWILI WANGU ) Imezaminiwa na   Simulizimahiri.blogspot.com Mahakama kubwa ya kesi za jina...