Thursday, March 30, 2017

MUATHIRIKA

SIMULIZI : MUATHIRIKA

Mtunzi : Iddi Siraji
.................

Nilisahau kuwa hakuna furaha inayodumu milele hapa duniani niliona na bahati kubwa ilioje kupendwa na mtu nilie mpenda sana na niliona sasa ulikuwa wakati wangu wa mimi kuyaanza maisha mapya ya mume na mke kumbe mungu nae alikuwa amepanga la kwake, nilicho kiwaza mbele yangu ili kuwa ni kuishi maisha ya furaha na upendo kutoka kwa mpenzi ISSABELLA ....sikufikiria hata mara moja kama ndoa ile isinge fungika kwani nilijiamini sana mbele ya upendo mkubwa ulijengeka baina yangu na  issabela.... nilisahau kabisa kila unacho upanga mungu nae ana panga na kupangua ulicho panga.......

Nasikitika sana mpenzi msomaji kwani katika mkasa huu nimepoteza kila kitu furaha na watu wangu wa karibu.....mungu azilaze mahali pema roho za marehemu wote waliopoteza uhai katika mkasa huu wa MUATHIRIKA.
°°°°°°°°°°

ISABELLA alikuwa mwanamkee pekee alienipenda sana katika hii dunia licha yakuwa mimi ndo nilikuwa mwanaume wa kwanza kuujua usichana wake mimi nilikuwa mwanaume pekee kwenye swala mahusiano kwake , mara nyingi Isabella aliwahi kuniambia tangu aingie kwenye ulimwengu wa mahusiano mimi nimekuwa mwanaume wa kwanza kwake na hakuwahi kujaribu na mwanaume mwingine.

Maneno ya isabella yalinifanya nifurahi sana na kujiona wapekee kwa kukabidhiwa moyo na msichana mrembo isabella tangu nilipo kuwa nae shule ya sekondali mpaka anafika chuo hakuwahi kunisaliti, ila mimi nakiri kwamba mara kadhaa nilimsaliti na kuchepuka na wasichana fulani hii ni kutokana na wanaume tumeumbwa kutamani.

Isabella alipo kuwa chuo mwaka wa pili aliniletea habari kuwa yeye ni mjauzito amenasa ujauzito kutoka kwangu ile ilikuwa habari njema kwangu na kwake pia kwani issabella alithibitisha wazi furaha yake ya kubeba ujauzito niliompa na hakuwa tayari kuitoa hata kwa kulazimishwa.

Kwakuwa yeye alikuwa yupo chuo na mimi nilikuwa ni muajiliwa wa kampuni moja kubwa ya biashara hapa nchini mimi na Isabella tulipanga kufanya mikakati ya ndoa ili tukaishi maisha ya mume na mke na mtoto azaliwe ndani ya ndoa...
"Ila inabidi mpenzi wangu dotto tukapime afya zetu kwa ajili ya kiumbe kilichomo tumboni mwangu " mpenzi wangu isabella aliongea kwa sauti ya upendo.
"Kweli mpenzi wangu ila subiri zipite wiki mbili zipite nimalizie majukumu ya kiofisi sawa mama kijacho" nilimjibu kwa furaha
"sawa dotto...ila naomba hiyo siku tukapime kwenye ile hosptal anayo fanya kazi kaka yako kulwa" isabella aliongea na kuitaja hispatal ambayo pacha wangu kulwa alikuwa doctor pale....kwani sisi katika familia yetu tulizaliwa mapacha wawili naamu mapacha wa kufanana sana tulikuwa tuna fanana sana usinge weza kututofautisha kiurahisi yeye aliitwa kulwa nami niliitwa dotto, .

Basi bwana hatimae ile siku tuliyopanga tukapime kujua afya yetu ilifika , mida ya saa tano asubuhi tulifika kwenye hosptal ambayo kaka yangu kulwa alikuwa doctor mkubwa kwenye hiyo hosptal ilio sifika kutibu vizuri japo kwa gharama za juu.

Tuliingia kwenye ofisi ya kulwa ambae tulimkuta akipulizwa na kiyoyozi . baada ya salamu na maongezi mawili matatu basi ndugu yangu akaweka sawa vifaa vyake ili zoezi lililo tuleta lianze...

Kwanza alianza kupima Issabella ambae hakuonekana kuwa na wasiwasi hata kidogo...
"Ah shemeji yangu Isabella wewe huna tatizo damu yako ni safi kabisa" aliongea na kumpa mkono wa hongera mpaka hapo sikuwa na wasi wasi hata kidogo kama Issabella hana mimi naupataje nilijipa moyo kisha kaka yangu kulwa alienizidi saa moja kuliona jua katika kuzaliwa kwetu, akanipima na kabla hajatoa majibu alionekana kushtuka na kuwa kama haamini anacho kiona....
"vipi kaka"  nilihamaki
"No i think some mistake" alijibu kisha akarudia tena kunipima na kuangalia vipimo vyake ghafla sura yake iliingiwa na simanzi na mfadhaiko mkubwa huku safari hii machozi yakimlenga.

LAHAURA! vipimo vilisema mimi ni MUATHIRIKA....

Hakuna alie weza kuikabili simanzi ile ilio letwa na vipimo vilivyo thibitisha kuwa mimi nimuathirika ...Isabella alichanganyikiwa na muda huo pacha wangu alikuwa kainamia meza yake ya ofisi....sasa niliona dunia inazunguka kwa kasi kiasi cha kufanya ni hisi kizungu zungu..(inamaana kati ya jeska na mariamu mmoja wapo kaniambukiza virusi) nilijiuliza na kuwakumbuka wasichana wawili nilio chepuka nao kwa wakati tufauti mwezi mmoja nyuma.

Nikahisi kitu kizito kimenikaa kooni, nikajikuta nikisimama na kupiga hatua

"Dotto why .....nani kakuambukiza....." Issabella aliuliza huku akilia....

Nilishindwa kuvumilia nikafungua mlango na kutoka nje ya ofisi kulwa akajiribu kuniita lakini sikugeuka nyuma nikashusha ngazi za hospatal ile na kuelekea nilipo egesha gari haraka nikatoeka eneo lile.

Naam nilikuwa nina maambukizi ya virusi vya ukimwi na hili halikuwa pigo kwangu tu ilikuwa hadi kwa baba na mama niliwahudhunisha sana japo walijitahidi kunipa moyo na kuniambia ni ule ni ugonjwa kama magonjwa mengine lakini pamoja na kunipa moyo hudhuni yao ilionekana wazi.

Nilikata tamaa kwakila kitu lakini kila nilipo mfikiria issabella moyo wangu uliuma sana na alinipigia simu mara nyingi ila sikupokea kwani sikujua nimueleze nini.

Mara nyingine kaka yangu kulwa aliniletea simu akiniambia kuwa issabella anataka kuongea na mimi lakini nilikataa kabisa.

Hatimae nilifanya maamuzi nayo yalikuwa nikumtumia ujumbe wa maandishi mpenzi wangu mpendwa issabella....ujumbe ulikuwa ni wa kumuomba msamaha issabella nikimwambia ajitahidi kusahau kuhusu mimi mwanaume ni siye kuwa na bahati ,na nikamsihi atafute mume mwingine ambaye ataishinae pamoja na mwanangu atakae zaliwa hapo baadae "ila iwapo kama itatokea mume wako akawa hampendi mwanangu haraka sana mrudishe nyumbani....ni hayo tu mpenzi Issabella najua jinsi gani umeumia ila hata mimi naumia sana huwenda zaidi yako kwaheri mpenzi please usitoe hiyo mimba maana mtoto atakae zaliwa ndie atakuwa kumbu kumbu yetu sote wawili."

Baada ya kumtumia ujumbe huo nilizima tena simu na kuitoa laini na nikaweka line nyingine mpya , nikaendelea kufanya maandalizi ya safari yangu safari ya arusha! ndio nilikuwa nimechukua maamuzi ya kwenda kwa bibi yangu arusha ,kutoka.a na hali iliyo nikuta niliona bora nikapumzishe akiri kwa bibi .

Saa kumi ya alfajri ya siku iliyofuata nilitoka nje ya geti letu nikiwa ndani ya gari la kulwa mama na baba waliniaga huku wakini sihi nisichukue maamuzi yoyote mabaya kwani wao wananipenda sana na kuathirika sio mwisho wa uhai ila nikifuata mashariti nitaishi vizuri sana....ndugu yangu kulwa alinipatia vidonge vingi sana vya ARV "mdogo wangu ukifuatisha mashariti ya vidonge hivi utaisha maisha marefu pengine kutupita sisi" kulwa alinisihi, wakanipeleka stendi na kuniacha ndani ya basi nikielekea arusha wao wakarudi nyumbani.

************-ARUSHA********
Niliona ndoto zangu zote za maisha ya badae zilikuwa zimefikia tamati kwani siku zote nilisoma kwa bidii na nilipo ajiliwa nilijituma sana kwani malengo yangu ilikuwa ni siku moja niwe mfanya biashara mkubwa ,Lakini sasa ndoto zote nilizizika maana niliona haina maana kufanya hayo yote wakati wakati natembea na kifo.
Jijini arusha niliishi maisha ya upweke sana nikiwa kwenye nyumba ya bibi iliokuwa na ndugu wengi..usoni niliwaonesha furaha na tabasamu kubwa lakini moyoni nilikuwa na majonzi tele.

Mara nyingi bibi alinipa moyo nakunisitizia nisiache kunywa vidonge nami nilimkubalia lakini nilikuwa si mkweli kwake kwani tangu nifike arusha sikuwahi kunywa kidonge hata kimoja ila nilikuwa navitupa kwenye sinki la choo na kuwaongopea nimekunywa, niliona haina maana ya kunywa vidonge na kuishi maisha ya kutumaini  vidonge vya ARV ambavyo nilitakiwa ninywe kila siku ...mimi niliona bora nisinywe ili nife haraka na kuiacha hii dunia iliyo sheheni visa maatatizo ya kila aina.

Ilipita miezi mitatu tangu nipate maambukizi ya virusi na nilikuwa sina mawasiliano ya aina yoyote kwa mpenzi wangu issabella , siku moja  nilipokea ujumbe wa Issabella alionitumia kwa njia ya email yangu ujumbe ulikuwa wa kuuchoma moyo wangu....."Kwako mpenzi wangu doto nimimi wako nikupendae kwa dhati  naakuandikia haya nikiwa nipo na pacha wako kulwa napenda kukujulisha kwamba familia yangu na familia yako imekaa na kuamua kwamba niolewe na kaka yako kulwa ili kuficha aibu yako kwa watu waliojua kua utanioa hivi karibuni ....hivyo siku ya harusi wengi watajua wewe ndio unanioa kwa  kuwa umefanana vyema na kaka yako kulwa ....kwa upande wangu mimi sina pingamizi la swala hili nakupenda sana mpenzi wangu dotto nakutakia maisha mema." ...

Jasho lilikuwa linanitoka baada ya kuisoma barua ile ilioumiza moyo wangu nikiwa bado nafikiria mara bibi aliniletea simu akisema mama kampigia anataka kuongea na mimi amepiga simu yangu haipatikani, nilichukua simu ile na kuiweka sikioni na kukutana na sauti ya mama ilio nisalimu kwa kunijali na baada ya salamu alinipatia taarifa ambayo nilisha isoma muda mchache uliopita ...mama yangu alinisihi na kunibembeleza kuwa nikaze moyo kuyashinda maumivu ya moyo
"Ahhh am usijali mama mimi hii mitahani nilisha ishinda" niliongea kwa kujikaza huku sauti yangu ikitetemeka
"Lakini mwanangu kama hujapendezwa na swalala kulwa kumuoa issabella niweke wazi ili swala hili lisifanyike" mama aliongea kwa kunibembeleza.
"Ah mama moyo wangu ni mkunjufu acha kulwa amuoe ili hata mwanangu akizaliwa asiteseke kwa baba asie nijua " niliumaliza mjadala huku moyo wangu ukiniuma sana...
"Haya kila la heri mwanangu mpendwa" mama aliongea na kukata simu.

Baada ya mama kukata simu niliwasha simu yangu kisha nikaziblack list namba ya kaka yangu kulwa na issabella kisha nikiblack list namba za marafiki wangu wa dar esalaam kisha nikablock akaunt zangu za mitandao ya kijamii ili siku ya harusi yao nisizione picha zao..

nikaendelea kuishi arusha huko moyo wangu ukiendelea kuwa kwenye maumivu makali na majeraha ya sio pona nikawa na isubiri kwa hamu siku yangu ya kufa kwani sikunywa dawa za dawa za kupunguza makaoi ya ukimwi makusudi ili nife mapema .

************************************

Ulipita mwaka mmoja na miezi minne tangu harusi ya Issabela na ndugu yangu ifanyike na nilishapata taarifa kuwa issabella alijifungua salama mtoto wakike alie mpatia jina la MARIA...nilimshukuru mungu kwa mwanangu kuzaliwa salama japo sikutaka kwenda kumuona ....nilikuwa sina mawasiliano na issabela wala kulwa hata taarifa ya kujifunguwa kwake nilipewa na mama kupitia simu ya bibi.

Afya yangu haikuwa nzuri nilikuwa nimedhohofika sana nilikonda sana mpenzi msomaji wa mkasa huu .

**"""TAHARUKI********

Katika hali yakutotegemea nililetewa taarifa kwamba kaka yangu amefariki dunia baada ya kuwawa na alie mua alikuwa ni mke wake ISSABELLA alie muoa mwaka mmoja uliopita..!!!! jeshi la polisi linamshikilia issabella kwa mauaji aliofanya.

Nikitu kigumu sana kuamini eti issabella amemua kulwa nilihisi kuchanganyikiwa sana siku iamini taarifa ile .
haraka nilifanya maandalizi ya safari ya kurudi jijini dar esalaam.

Niliwasili jijini dar es salaam na kukodi tax ilionifikisha nyumbani ambapo palikuwa na umati mkubwa watu , kufikia hapo moyo wangu ukathibitisha ni kweli kulwa amekufa nilishindwa kuyazuia machozi.

Msiba ulikuwa ni pigo la kushtukiza liliyo piga mioyo ya kila mwanafamilia, niliambiwa kuwa mtoto wa issabella ambae ni damu yangu yupo kwa shangazi kwani mama yake yupo rockup.

Nikiwa kwenye udhuni ile ya kumpoteza pacha wangu mara ilikuja taarifa nyingine ya kushutua  nayo ni kujinyonga mtuhumiwa alieshikiliwa na polisi kwa kufanya mauaji ya kaka yangu......Eti issabella alikuwa,
matukio haya  yalinifanye nihisi nipo ksenye ndotona muda wowote ningeshtuka kutoka usingizini.

"Issabella kajinyoga akisa rockup na katika kujinyonga kwake aliacha barua alioiandika kabla ya kujininginiza kwa kitambaa cha gauni lake." aljongea I.S.P aluoleta taarifa .

Nililetewa barua ile ilio achwa na issabella kwani marehemu aliandika ili ni fikie mimi ...

Nikaanza kuisoma huku nikitetemeka.....

"Habari mpenzi wangu nikupendae kwa dhati ni matumaini yangu ni mzima wa afya..nakuandikia haya ili upate kujua ukweli ambao umefichwa kwa muda mrefu...
mpenzi dotto ndoa ya mimi na kaka yako sio kwamba familia zetu zilikaa na kupanga ile ndoa, hapana ni kaka yako alianza kunitongoza baada ya wewe kuondoka na kwenda arusha , kaka yako alinishawishi sana akisisitiza anahitaji kuziba pengo lako na kunifuta maumivu ulioniachia alinisihi nimuone yeye kama wewe kwani mmefanana sana .
kila siku alinipigia na kunisihi sana na hatimae nikakubali kwani mioyo yetu bina damu imeumbwa kurubunika...mikakati yote ya ndoa aliifanya yeye huku familia yangu na yako ikimuunga mkono kwani walijua kwa ndoa ile wangeficha fedheha yako kuwa umeshindwa kunioa sababu una ukimwi.

Hatimae ndoa ilifungwa na watu wngi walijua kuwa wewe ndio umenioa...kaka yako alionesha kunipenda sana na aliijali mimba ulionipa kana kwamba yake hata mtoto alipozaliwa alimpenda sana.

Lakini tatizo limeibuka kuanzia wiiki tatu zilizo pita baada ya mimi kugundua kuwa kaka yako kuna vidonge anatumia kila siku anakunywa na nilipo fuatilia kimya kimya juzi nili fanikiwa kuviona vidoge vile kwenye begi lake la kazi nikagundua vile ni vidonge vya A R V vya kuzuia makali ya H I V , mpenzi niliogopa sana na sikutaka kuamini kwamba mume wangu ambae ni kaka yako ni MUATHIRIKA ikanilazimu kukaa na kumsubiri atoke kazini, nikaenda kumlaza mtoto wangu maria kwenye kitanda chake, kisha nikarudi sebuleni   nika kaa kumsubiri kaka yako huku nikiwa na vidonge vile mkononi... nili msubiri sana kwani alirudi saa tano usiku akiwa kalewa kidogo kwani ni kawaida yake kunywa siku moja moja....alipo niona nimeshika vidoge vile alishtuka sana na nilipo muuliza kwa hasira aliniomba msamaha na kukiri kuwa ni kweli yeye ni muathirika!!!!!!!!!!! nusu nipoteze fahamu kwa mshtuko.

Alikiri kuwa alipata maambukizi tangu akiwa chuo ila alifanya siri kiasi kwamba wazazi wako na wewe hamkujua swala lile na hakutaka mjue , .....na alifanikiwa.
Kaka yako aliongea huku machozi yakimtoka akiniomba nimsamehe kwani hata wakati wa ndoa alinidanganya na kuniletea vyeti bandia vilivyo thibitisha hana virusi hii ni kutokana alinipenda sana asinge weza kukubali kunikosa Kwani alikuwa ananipenda tangu nilipokuwa na wewe kwenye mahusiano yetu ya awali tulivyokuwa seondary....

Kaka yako alifichua siri nyingine nzito na kusema kuwa wewe huna virusi vya ukimwi ila siku ile tulipo enda kupima alikuzushia kwamba unaukimwi ile ndoto zako za kunioa zife kisha anioe yeye !!!!! na alifanikisha mpango wake...Mpenzi wangu wewe huna virusi vya ukimwi ...
Baada ya ndugu yako mshezi kuniambia hayo nililia sana kwani hata mtoto nilie mzaa nae ni muathirika baada ya mimi kuambukizwa na kaka yako kabla sijamzaa , roho iliniuma sana lakini alini bembeleza na nikamwambia nimemsamehe!! tukaenda kulala .

Hivi kwa ubaya ho alio ufanya marehemu kaka yako  ni mwana damu gani anaweza kumsamehe kaka yako?? ok acha nikumalizie mkasa.
usiku wa manane kaka yako akiwa kalala fofofo niliamka na kwenda jikoni ni kachukua kisu na kumsogelea marehemu kaka yako kisha kwa nguvu kubwa na kwakishindo nilizamisha kisukile kwenye kifua chak....."  ....***********

Ndugu msomaji nilishindwa kumalizia barua ile nguvu ziliniisha na nikahisi pumzi zikiniishia....

Issabela alikuwa amemua kulwa kumchoma kisu kwenye kifua chake upande wa kushoto na na kurudia mara kadhaa kitendo kile cha ukatili ..
. Mungu azilaze mahali pema roho za marehemu walio poteza uhai wao katika mkasa huu wa MUATHIRIKA, malaika wa faraja awafute machozi na kuwapa furaha watu wote wanaoishi na maambukizi ya ukimwi.

Mpenzi msomaji kupata ukimwi sio mwisho wa maisha yako lakini jihadhari ukimwi unaua....

0746206428 whatsup kwa maoni zaidi juu ya mkasa huu wa MUATHIRIKA.

MWISHO.

Huu ni mwisho wa simulizi hii ya muathirika ila jiandae kusoma kipande kingine kitakacho husu maisha ya mtoto maria ambae ni MUATHIRIKA.  simulizi hii imeandikwa na ndugu IDDI SIRAJI.

Thursday, February 23, 2017

SIMULIZI ZA PICHA http://simulizimahiri.blogspot.com/2017/02/simulizi-za-picha.html

Monday, January 9, 2017

SEHEMU YA TATU

RIWAYA ;ROAD 2017
MTUNZI ;IDDI SIRAJI
WHATS'AAP-0746206428

  Usiku wa kafara..

ilipoishia.....

Gola akamuinua diana ambae hakuwa na fahamu kabisa akamuweka begani kisha akamtazama mama diana kwa macho ya chuki.
gola akageuka na kutikomea akiwa na diana begani...

"Haya mliobakia anzenu ibada ya kukaribisha sadaka ya usiku huu wa kafara"..

endelea..

31December.
Baraka alishuka na kwenda mbele ya gari na kufunua lile bati linayo ifunika injini na hapo macho yake yaka kutana na moshi kutokea kwenye injini.

"Dah gari imechemsha tukisema tuisubiri ipoe inabidi tukae saa zima ....ila kutoka hapa hadi kwenye mashine ya wind walter ni kama dakika kumi na tano hivyo napendelea tukachukue maji huko ili tusichelewe sana"  baraka aliongea huku akiliangalia gari lake lilio fuka moshi...
baraka alikuwa mzoefu wa barabara  hii mara nyingi alishawahi kuitumia na kutembea sana eneo la wind walter

"dah hii ilishakuwa mbaya na mama nilimuahidi nitampigia jioni mpaka sasa hivi saa mbili usiku sijampigia na hapa naona mtandao haukamati" sarah alilaani maana alijua muda ule wazazi wake wanamtafuta kwenye simu...
"Ah usijal chukua tablet yangu  uwa pigie kwa namba yangu ya zantel maana zantel hapa ina kata kwa njia ya satelite" baraka alio ngea kisha akawageukia gadyson na john
"oya wazee wa kazi tufanye maamuzi ya haraka" baraka aliwasihi
"ok kama vipi hawa bibie tuwaache sisi tukachukue hayo maji haraka" john aliongea na muda huo baraka akafungua mlango wa mizigo na kuchukua dumu lisilo na kitu ndani kisha akamsogelea neema.
"sasa jamani tunawaacha humu kwenye  gari sisi tunakuja haraka" baraka aliongea na kumbusu neema kwenye paji la uso(neema na baraka walikuwa na mahusiano ya kimapenzi"

John nae alimsogelea msichana dolla na kumbusu kwenye midomo yake..."kuwa na amani sawa mpenzi" john aliongea baada ya kumpiga busu na dolla alitikisa kichwa kuafiki. ..pia john na dolla walikuwa ni wapenzi

Ni sarah pekee ndie alikuwa msichana asie kuwa na mpenzi kwenye safiri ile yeye mpenzi wake alikuwa akimsubiri kwenye ile hotel walio panga kwenda kushrehekea mwaka mpya pale bagamoyo.

Gadyson nae hakuwa na mpenzi kwenye safari ile ila kuna wakati alijaribu kumchombeza sarah walipo kuwa mbugani mikumi, lakini sarah alionesha msimamo na gadyson akawa kalifutilia mbali lile swala.

Baraka akachomoa ufunguo wa gari yake na kuutia mfukoni akiwa na kidumu aliwasha touch yake yenye mwanga mkali akaaanza kuongoza njia akiwaongoza john na gady kuelekea kwenye maji wakiwaacha wasichana watatu ndani ya gari.

Tayari ilikuwa ni saa mbili usiku na upande wa magharibi mwezi mkubwa wa kuvutia ulikuwa una chomoza.

Kile kikosi cha vijana mbweha kikiongozwa na mzee juma kilikuwa kime wasili eneo lile kwa usiri na  ukimya wa hali ya juu  na wao walikuwa upande wa pili wa barabara na waliwashuhudia akina baraka wakiwaacha wasichana ndani ya gari na wao wakitokomea ndani ya msitu.

"sasa watu watatu wafuateni hao wa kiume sisi tunaenda kuwakamata hao wasichana wao tuna wapeleke kwa goroza" mzee juma aliongea na muda huo vijana watatu wakainuka na kuwafuata kina baraka ...vijana watatu hao walifuata kwa kuwazunguka na kwa mwendo wa ukimya mkubwa.

"dalu wanyatie kimya kimya na wasikuone ukifika jaribu kuufungua mlango wa gari" mzee juma aliongea na kijana dalu akiwa na panga aliondoka akiwa kajikunja kuanzia kiunoni huku aki hama mti hadi mti akihofia ule mwanga wa mbala mwezi usije kumfanya aonekane.

Ilimchukua dakika kumi na mbili  kufika pale kwenye gari ali kokota kokota akiwa anatembele magoti aliufikia mlango na kujaribu kuvuta kile kitasa lakini haukufunguka  akauwacha na kutambaa tena ili akajaribu kufungua mlango wa upande mwingine..

Ndani ya gari wasichana hawakutambua lolote dolla na neema walikuwa wakisikiliza mziki kwenye ear phone na sarah alikuwa busy na tableti akihamisha namba za wazazi wake ili awapigie.....

Baraka na wenzake walitembea kama dakika kumi  kisha akasita kichwani kwake akiwa kuna kitu amekumbuka
"ah nime fanya ujinga ujue humu ni mstuni na kuna wadudu wa na wanyama siku paswa kuiacha bunduki"  baraka aliongea huku akisimama
"ilo nalo neno" gadyson alijibu
"ok ikimbilie sisi tuna kusubiri hapa" john aliongea na baraka akaweka dumu chini akaanza kukimbia kuirudia bunduki yake huku touch yake ikimulika msituni mule  ipasavyo .

Dalu wakati ule ana zunguka ghafla aliona mwanga wa touch kwa mbali ukija kueleke kwenye gari akahamaki na haraka akajua kina baraka wana kuja... haraka dalu akaingi uvunguni mwa gari...

Sarah alijaribu kumpigia  mama yake lakini mama yake alipo pokea simu sarah aliisikia sauti  ya mama yake lakini mama yake hakumsikia sarah..
"dah mtandao una sumbua kweli" sarah alisema na hapo akaona mwanga wa touch ukija upande wao  "oh mara hii wamesha pata maji... ngoja nishuke nimpigie mama huenda nje ya gari nitaongea nae vizuri" sarah aliongea na kutoa lock ya mlango na kushuka akakifuata kisiki cha mti wa mbuyu akakipanda mara moja na kuanza zoezila kumpigia mama yake..

na muda huo baraka nae alikuwa ameisha ifikia gari...

nini kita tokea hapo ?
vipi gadyson na john ? iwapo watatokewa na wale vijana watatu waliotumwa na mzee juma.

like share iendeleee

Friday, January 6, 2017

RIWAYA YA ROAD TO 2017

RIWAYA : ROAD TO 2017

SEHEMU YA PILI.

31 DECEMBER.

ILIPO ISHIA..
"Hatuna haja ya kuuana sisi kwa sisi leo usiku mtapata damu ya kutosha na gozola atalizika.... kuna watu wanakuja kupitia ukanda huu leo leo wote sita watakuwa chakula chetu usiku huu" bibi yule kizee aliongea kwa sauti ya juu huku kichwani mwake akiwaona wale watalii wakiendeshwa na baraka....!

"ndio wanakuja kupitia barabara jirani leo tutafurahia damu zao" aliongea tena kwa msisitizo.

Endelea..
USIKU WA KAFARA.

Wote walikuwa kimya hata gola nae hakusema kitu.
"haya kila mtu arudi mahali pake na binti wa mama diana ahifadhiwe mpaka nitakapo rudi kutoka ndani" yule Mzee ali waamulu
"sawa malikia" wote walijibu na kuanza kurudi sehemu waliyo kaa mwazo huku mzee juma akimuhifadhi vizuri yule binti kigoli diana.. na yule malikia kikongwe akarudi tena pangoni aakanene na gunzani.

*****************

Baraka aliendesha gari kwa speed tena kwa umakini mkubwa
"Dah hawa askali wametupotezea muda mwingi sana" baraka aliongea na kuvunja ukimya wa punde
"Ah ila mimi niliogopa sana nilipo muona yule askali katoa bunduki kwenye gari yako " sauti ya msicha mmoja kati ya wale watatu aliongea
"Umeonae dolla ...halafu wewe baraka unatabia mbaya kumbe una bunduki humu muda wote huja tuambia" msichana mwingine alidakia kumuunga mkono msicha dolla namsichana huyu alie dakia aliitwa Neema

"AH vitu vidogo sana kumiliki bunduki kama ile kwangu kama fimbo tu" baraka aliji gamba

"ehee ulisha anza kujisifu mr misifa ...sio ajabu hata hajui kuitumia bunduki yenye" sauti ya kiume kati ya wanaume watatu ndani ya gari ile ili msanifu baraka kwa kumtania

"Umeonaeeh john kaishaanza kujisifu" kijana wa tatu aliimuunga mkono john . nahuyu  aliemuunga mkono john aliitwa   Gadyson huku

wote wakicheka...

Kabla kicheko chao hakijaisha baraka alikanyaga brek ya ghafla kisha wote wakayumba kwa kwenda mbele na kurudishwa nyuma na muda huo baraka akashuka na kwenda kuufungua mlango wa nyuma kabisa kulipo kuwa na mizigo akaipekuwa na kuichukua ile bunduki akarudi nayo kwa wenzake akaingiza mkono mfukoni akatoa mfuniko wa simu akamkabidhi john na kumwambia auinue juu mfuniko ule..

"ENHEEE hivyo hivyo uinuie juu nataka ni ulenge niupige risasi huo mfuniko" baraka aliongea huku akirudi nyuma akawa anaikoki kwa kuvuta kitasa kichoopo juu ya bunduki ile
"ahh acha boya wewe" joh alimaka huku gadyson akitaka kuingia chini ya kiti na muda huo baraka akaanza kuwacheka
"mbona mmeogopa si mmesema sijui kuitumia"  baraka aliongea huku maneno yake yakiambatana na kicheko....muda huo wasichana walikuwa wakicheka kwani wanayajua masihara ya hawa vijana watatu..
"haya tazameni jinsi ya kuitumia " aliongea na wote wakamtazama
"ukitaka kupiga una vuta hiki chuma cha standby kisha hii triger unaibonyeza kwa kidole cha shahada ..." aliongea kisha akageuka akailekezea bunduki mstuni  na kufyatua risasi na mlipuko mkubwa ukasikika pale na wale wote watano waliziba masikio
"HAPPY NEW YEAR"  baraka alilalama kwa sauti ya kusherehekea
"Oya mzee wa manchester tuondoke naona ushaanza sifa zako" gadyson aliongea baraka nae akarudisha ile bunduki huku akicheka
"kumbe wa oga .. " aliongea huku akifungua mlango wa nyuma akaiweka juu ya mizigo akafunga mlango akaingia kwenye uskani..

"Yani huyu jamaa kila kitu chake anacho penda kibaya hilo bunduki lake bovu bovu sauti yake mbaya hata mwizi akija na mshale ana kutagisha... bado timu unayo shabikia mbovu....unavyo penda vyote vibovu kasoro demu wako neema"  john aliendeleza tena utani huku wale mabinti wakicheka
"acha wewe huyo movic ana goli kumi na moja bado mbili amkamate coasta then spurs man city asanal tupo nyuma yao tuna wakimbiza na baiskel lao la miti..nyie acheni timu yangu noma "baraka aliongea huku akianza kuchochea speed

"Ila hawa watu wana masihara sana wamenifanye niwe na furaha sana huu umekuwa mwaka mpya wa furaha sana nime enjoy kupita kiasi"  ilikuwa ni sauti ya sarah  msichana wa tatu ambae muda mwingi alikuwa kimya akicheka na kufurahia ucheshi ulio endeshwa na kina baraka.

"Hata mimi nime furahi sana NASHUKURU MWAKA HUU NIMEUMALIZA SALAMA! kuanzia mwanzo wa 2016 mpaka mwisho sija sumbuliwa na homa maradhi wala matatizo yoyote nimevuka mwaka salama thanks god" gadyson aliongea akiwa kwenye furaha.

NAAMU ! gadyson alihesabu kuwa amesha umaliza mwaka 2016 ! ama kweli usio lijua ni usiku wa giza mpenzi msomaji...

Safari ya furaha ilizidi kusonga huku maongezi ya kiucheshi yakitawala ndani ya gari lile..

Wakati baraka anaendelea kuendesha mara ghafla aliutambua muungurumo tofauti kwenye gari yake na hapo akakunja sura akilaani
"Ah chuma kilishaanza kuchemsha acha niweke maji ili ipoe mdogo mdogo" baraka aliongea huku akifunga brek na kuchukua touchi na kushuka nayo akazunguka kwenye mlango wa mizigo akaufungua na kulitafuta dumu la maji lakini hakuliona..
"ujinga huu hili dumu limeenda wapi" aliongea peke yake  huku akizidi kupanga na kupangua mizigo lakini ilikuwa kazi bure...
"wadau  kidumu cha maji tume kitupa wapi" aliwauliza wenzake na wao hawakujua
"kwani wale maafande walikirudisha kweli? maana walikishusha ule muda walipokuwa wana kagua" sarah aliwakumbusha wenzake..
"aah pumbavu zao watakua hawakukipandisha" baraka aliwalaani wale askali wa barabarani... baraka akafunga mlango wa mizigo na kurudi kwenye uskani.
"Hapa ina bidi niendeshe mwendo mdogo mdogo kwani gari inakaribia kuchemsha... ila kilo meta kazaa kutoka hapa kuna sehemu ina mashine ya walter wind hapo kuna kisima tutapata maji" baraka aliongea na wenzake wakaafiki na safari iliendelea kwa mwendo wa speed hamsini.

Kila walipo zidi kutokomea ndipo gari nayo ilizidi kuchemsha na baraka nae akapunguza speed hatimae gari ikawa inatembea taratibu kabisa kana kwamba ilikuwa kwenye foleni za tanzara.

Na mwishoe kabisa gari ile ilizima kabisa na baraka alijaribu kuwasha lakini haikuwaka hata kwa kujaribu...

Wakawa wamekwama katikati ya msitu na hapakuwa mbali sana na lile  pango la goroza!

******--*********;**************

Malikia wa viumbe wale yule mzee kikongwe alikuwa ndani ya pango akisubiria kwa hamu muda ufike na kwenye taswila yake aliwaona jinsi kina baraka walivyo hangaika na gari lao ..!
kikongwe yule aliwasha mshumaa mkubwa uliokuwa pembeni ya sanamu la goroza na kupunguza kiza ndani ya pango..

"Sadaka imefika ..." aliongea na kuanza kutoka nje ya pango lile huku kichwani mwake akiliona lile gari la kina baraka linavyo jikokota kwa mwendo dhaifu...

"Haya muda umefika mbweha mtaenda kuchukua sadaka sita zipo barabarani    ....mzee juma njoo nikuoneshe ukawachukue tuje tufurahie damu zao" malikia kikongwe aliongea baada ya kutoka nje na mzee juma haraka akamsogelea mzee yule..

Kwa hisia na maajabu malikia akamuelekeza mzee juma sehemu waliyo kwama akina baraka.. na mzee juma kwa muujiza mkubwa aliwaona wale marafiki sita waliokuwa ndani ya gari .

"Haya chukua mbweha sita uwaongeze mkalete hiyo zawadi  "  malikia alimuamuru mzee juma...

Wakatoka vijana sita kwenye kile kikundi cha washirikina wakiongozwa na mzee juma wengine wakiwa na mishale  mashoka na wengine mikuki huku wengine mapanga ambayo hutumika na kikosi hiki cha mbweha kukutolea sadaka .
jumla walikuwa saba wakaanza kuondoka kwa kukimbia wakielekea barabarani kuwachukua akina baraka ....huku mioyo yao ikiwa imetawaliwa natamaa ya kumwaga damu...

"gola mchukue diana mrudishe kwao haraka kwanjia ulio itumia kumleta"  mzee yule akamuamuru gola ambae hakupendezwa na amri ile kwani nia na matamanio yake ilikuwa kwa msichana diana usiku wa leo.

Gola akamuinua diana ambae hakuwa na fahamu kabisa akamuweka begani kisha akamtazama mama diana kwa macho ya chuki.
gola akageuka na kutikomea akiwa na diana begani...

"Haya mliobakia anzenu ibada ya kukaribisha sadaka ya usiku huu wa kafara"..... yalikuwa maneno ta malikia.....itaendeleaa...
like na kushare ili kesho iwahi kupostiwa...

RIWATA HII NI SPACIAL KWA MSIMU HUU WA MWAKA MPYA

PENZI LA FUKARA

RIWAYA PENZI LA FUKARA MATESO

MTUNZI : ZUBERI MARUMA

WHATSUP : 0652281153

CHAPISHO NO 01

(FUMBO LILILOFUMBWA)

SURA YA KWANZA

UTANGULIZI

Kila ninapojaribu kufumba macho yangu nikusahau uwa nashindwa.

Siuamin moyo wangu kama kweli ipo  siku ungeniacha

Tena katika kipindi ambacho nakuitaji zaidi.kipindi ambacho ndo ningetakiwa nile  matunda ya masomo yako

Leo hii Mimi na wewe tumekuwa kama paka na panya

Lazima nilipize kwa ulilolitenda?!

                   ************

Uso  wake ulikunjamana kwa hasira,mapigo yake ya moyo yaliongezeka kila muda ulipokuwa ukipotea,

Akalifungua kabati lililokuwa Mbele ya macho yake na kupeleka mkono ndani ya kabati lile,akawa anatafuta kitu katikati ya nguo

Akakipata

Ilikuwa ni bastola ndogo,akaiangalia kwa sekunde kadhaa na kuipachika kibindoni

Akalifunga vizuri kabati lile

Hakika moyo wake ulijaa majonzi,simanzi
,sononeko,maumivu tele yaliushambulia moyo wake....

kama kulia alishalia sana mpaka machozi yakamkauka!

maumivu makali yalikishambulia kichwa chake! yamkini ni kutokana na msongo wa mawazo ama kitendo chake ya kulia sana.....

kulilia mapenzi.

Akalifata droo lake akalifungua na kutoka na kalamu na karatasi akakaa katika meza na kuanza kuiandika barua,

huku machozi mepesi yakiloanisha mashavu yake na baadhi ya matone yakiangukia karatasi lile...

barua ile aliianza kwa kuiandika hivi:

"Kwako mpenzi SHONAIZAR!,

najua u mzima wa afya!,mimi kifikra sipo vizuri!
sidhani kama utaniuliza kwa nini!

sababu nadhani waijua

ila tambua kama mapenzi ni hisia!, hisia zangu zilikuwa kwako , uliniteka kifikra sikutaka nichomoke moyoni mwako, ulinifanya mfungwa katikati ya moyo wako, sikuona mwanamke kwa uzuri afikiaye umbo lako...

Ulitumia udhaifu huo kuntesa mwenzako, ni ahadi ngapi ulini ahidi kwamba utonisaliti?!, ni mara ngapi ulinambia kwamba UNANIPENDA sana?!,

kumbe wewe ni mwanahizaya ulojaa unafki eeh!?!...au kisa mimi ni fukara?,au kisa sina pesa?!

shone penzi langu kwa gharama yoyote lazima litalipwa!, machozi yangu niyatoayo kwa sababu yako yatakugarimu my x!,

tambua kama uliunyakua moyo wangu kwa kuni adaa kwamba unanipenda,

malipo yako nitakunyanganya roho yako,...

leo nayachukia mapenzi

kumbuka wewe ndo ulinifanya niyapende!

nakumbuka kipindi kile kwa mara ya kwanza tulipo onana, ndo kwanza ulitoka masomoni TABORA GARLS na kuja kijijini kwetu kufanya utafiti wa mimea na majani ukiwa na wenzako

mimi nikiwa mchungaji wa Mbuzi ndo kazi nlostaili kwa kipindi kile.

mbona marafiki zako wote walikukimbia pale nyoka mwenye sumu kali alipokugonga?

ZUBERI nikajitolea SHONAIZAR kukusaidia!

kosa langu lipo wapi hapo?

najuta kukufahamu

CHOZI LANGU LAZIMA LILIPWE

niliamua kukuchukua mpaka nyumbani kwangu nilipo kuwa naishi peke yangu

nikaanza kuku hudumia kwa madawa asili mpaka ukapona....

Malipo yangu yalikuwa nin?!
kama si kufungwa?

ulishindwa kunsaidia pale marafiki zako walipokuja na wazazi wako wakanikamata heti nimekuteka!!

msaada wangu ukawa adhabu kwangu ,kwa mara ya kwanza mchunga mbuzi kutoka kijijini nikaingia mjini nikiwa chini ya ulinzi mkali!

nyumbani kwangu pakawa segerea!

yani ung'atwe na nyoka nkuchukue nkutibu nionekane nlikuteka?! ila yote nilivumilia,

ulikuja kuniangalia!

na dhamana ukanitolea!, ukisema wazi kwamba mimi ndiye niliyekusaidia! nadiriki kusema msaada wako ndo ulikuwa huo kwangu!

mpz nishkuru kwa ilo!

kwa kunitoa mahabusu na kunitafutia kazi DAR!

sawa pengine labda kwa kuwa sikujua lengo lako mpaka pale ulipontamkia kwamba UNANIPENDA wewe ndo ulinambia siyo mimi niliyekutamkia!.

.kama kweli ulikuwa unanipenda iweje leo hii uje unsaliti?! utamu wa penzi lako ugeuke shubiri kwangu?

naapa my! lazima penzi langu utalilipa!...

hata ikibidi kwa ncha ya upanga!

ila sitokuacha mzima ama zangu ama zako!

SHONE mpenzi kumbuka!!!.....

nilikukubali kwa kuwa u! mwanamke mrembo,mwenye wajihi wa "black beuty" na macho malegevu kama unasinzia!,

dimpozi mashavuni, ulijaliwa miguu minene ya bia!, ni vigumu kwa mwanaume kukataa ombi lako!...

ni mara ngapi ulililia kifuani kwangu?, 

ukinielezea jinsi unavyonyanyasika kwenu?! kisaa.....

hata ulivyonielezea stori yako ya maisha, iliniuma mpenzi sikusita kulia kwamba mama yako alishafariki na sasa unaishi na mama wa kambo, 

anayekunyanyasa kwa masimango bila huruma kukupatia!  sikuweza kuzuia machozi kunitoka!

shetani mkubwa wewe!

nilikulilia nikikuonea huruma kwa nini nisingekuacha ukateseka? nakuchukia wewe mwanamke! nawachukia wanawake wote.....

sababu ikiwa ni wewe kahaba mmoja!

nitaridhika nitakapo ugawanya ubongo wako! kwa furaha sitosita kuula kwa ukatili ulontendea nipo tayari kufungwa,nipo tayari kunyongwa,pindi nikisababisha mauti yako....

KWA NINI KIJANA HUYU ANA HASIRA HIVI KIPI KIPO NYUMA YA PAZIA ITAENDELEA

UKITAKA VIPANDE VYA MBELE VYA RIWAYA HII JIUNGE NA GRP LA MALIPO WHATSUPP 1500 KWA MWEZI PATA VIPANDE 20 KWA 1000

Iblame my body

RIWAYA   : I'BLAME MY BODY ( NAULAUMU MWILI WANGU ) Imezaminiwa na   Simulizimahiri.blogspot.com Mahakama kubwa ya kesi za jina...