Thursday, March 30, 2017

MUATHIRIKA

SIMULIZI : MUATHIRIKA

Mtunzi : Iddi Siraji
.................

Nilisahau kuwa hakuna furaha inayodumu milele hapa duniani niliona na bahati kubwa ilioje kupendwa na mtu nilie mpenda sana na niliona sasa ulikuwa wakati wangu wa mimi kuyaanza maisha mapya ya mume na mke kumbe mungu nae alikuwa amepanga la kwake, nilicho kiwaza mbele yangu ili kuwa ni kuishi maisha ya furaha na upendo kutoka kwa mpenzi ISSABELLA ....sikufikiria hata mara moja kama ndoa ile isinge fungika kwani nilijiamini sana mbele ya upendo mkubwa ulijengeka baina yangu na  issabela.... nilisahau kabisa kila unacho upanga mungu nae ana panga na kupangua ulicho panga.......

Nasikitika sana mpenzi msomaji kwani katika mkasa huu nimepoteza kila kitu furaha na watu wangu wa karibu.....mungu azilaze mahali pema roho za marehemu wote waliopoteza uhai katika mkasa huu wa MUATHIRIKA.
°°°°°°°°°°

ISABELLA alikuwa mwanamkee pekee alienipenda sana katika hii dunia licha yakuwa mimi ndo nilikuwa mwanaume wa kwanza kuujua usichana wake mimi nilikuwa mwanaume pekee kwenye swala mahusiano kwake , mara nyingi Isabella aliwahi kuniambia tangu aingie kwenye ulimwengu wa mahusiano mimi nimekuwa mwanaume wa kwanza kwake na hakuwahi kujaribu na mwanaume mwingine.

Maneno ya isabella yalinifanya nifurahi sana na kujiona wapekee kwa kukabidhiwa moyo na msichana mrembo isabella tangu nilipo kuwa nae shule ya sekondali mpaka anafika chuo hakuwahi kunisaliti, ila mimi nakiri kwamba mara kadhaa nilimsaliti na kuchepuka na wasichana fulani hii ni kutokana na wanaume tumeumbwa kutamani.

Isabella alipo kuwa chuo mwaka wa pili aliniletea habari kuwa yeye ni mjauzito amenasa ujauzito kutoka kwangu ile ilikuwa habari njema kwangu na kwake pia kwani issabella alithibitisha wazi furaha yake ya kubeba ujauzito niliompa na hakuwa tayari kuitoa hata kwa kulazimishwa.

Kwakuwa yeye alikuwa yupo chuo na mimi nilikuwa ni muajiliwa wa kampuni moja kubwa ya biashara hapa nchini mimi na Isabella tulipanga kufanya mikakati ya ndoa ili tukaishi maisha ya mume na mke na mtoto azaliwe ndani ya ndoa...
"Ila inabidi mpenzi wangu dotto tukapime afya zetu kwa ajili ya kiumbe kilichomo tumboni mwangu " mpenzi wangu isabella aliongea kwa sauti ya upendo.
"Kweli mpenzi wangu ila subiri zipite wiki mbili zipite nimalizie majukumu ya kiofisi sawa mama kijacho" nilimjibu kwa furaha
"sawa dotto...ila naomba hiyo siku tukapime kwenye ile hosptal anayo fanya kazi kaka yako kulwa" isabella aliongea na kuitaja hispatal ambayo pacha wangu kulwa alikuwa doctor pale....kwani sisi katika familia yetu tulizaliwa mapacha wawili naamu mapacha wa kufanana sana tulikuwa tuna fanana sana usinge weza kututofautisha kiurahisi yeye aliitwa kulwa nami niliitwa dotto, .

Basi bwana hatimae ile siku tuliyopanga tukapime kujua afya yetu ilifika , mida ya saa tano asubuhi tulifika kwenye hosptal ambayo kaka yangu kulwa alikuwa doctor mkubwa kwenye hiyo hosptal ilio sifika kutibu vizuri japo kwa gharama za juu.

Tuliingia kwenye ofisi ya kulwa ambae tulimkuta akipulizwa na kiyoyozi . baada ya salamu na maongezi mawili matatu basi ndugu yangu akaweka sawa vifaa vyake ili zoezi lililo tuleta lianze...

Kwanza alianza kupima Issabella ambae hakuonekana kuwa na wasiwasi hata kidogo...
"Ah shemeji yangu Isabella wewe huna tatizo damu yako ni safi kabisa" aliongea na kumpa mkono wa hongera mpaka hapo sikuwa na wasi wasi hata kidogo kama Issabella hana mimi naupataje nilijipa moyo kisha kaka yangu kulwa alienizidi saa moja kuliona jua katika kuzaliwa kwetu, akanipima na kabla hajatoa majibu alionekana kushtuka na kuwa kama haamini anacho kiona....
"vipi kaka"  nilihamaki
"No i think some mistake" alijibu kisha akarudia tena kunipima na kuangalia vipimo vyake ghafla sura yake iliingiwa na simanzi na mfadhaiko mkubwa huku safari hii machozi yakimlenga.

LAHAURA! vipimo vilisema mimi ni MUATHIRIKA....

Hakuna alie weza kuikabili simanzi ile ilio letwa na vipimo vilivyo thibitisha kuwa mimi nimuathirika ...Isabella alichanganyikiwa na muda huo pacha wangu alikuwa kainamia meza yake ya ofisi....sasa niliona dunia inazunguka kwa kasi kiasi cha kufanya ni hisi kizungu zungu..(inamaana kati ya jeska na mariamu mmoja wapo kaniambukiza virusi) nilijiuliza na kuwakumbuka wasichana wawili nilio chepuka nao kwa wakati tufauti mwezi mmoja nyuma.

Nikahisi kitu kizito kimenikaa kooni, nikajikuta nikisimama na kupiga hatua

"Dotto why .....nani kakuambukiza....." Issabella aliuliza huku akilia....

Nilishindwa kuvumilia nikafungua mlango na kutoka nje ya ofisi kulwa akajiribu kuniita lakini sikugeuka nyuma nikashusha ngazi za hospatal ile na kuelekea nilipo egesha gari haraka nikatoeka eneo lile.

Naam nilikuwa nina maambukizi ya virusi vya ukimwi na hili halikuwa pigo kwangu tu ilikuwa hadi kwa baba na mama niliwahudhunisha sana japo walijitahidi kunipa moyo na kuniambia ni ule ni ugonjwa kama magonjwa mengine lakini pamoja na kunipa moyo hudhuni yao ilionekana wazi.

Nilikata tamaa kwakila kitu lakini kila nilipo mfikiria issabella moyo wangu uliuma sana na alinipigia simu mara nyingi ila sikupokea kwani sikujua nimueleze nini.

Mara nyingine kaka yangu kulwa aliniletea simu akiniambia kuwa issabella anataka kuongea na mimi lakini nilikataa kabisa.

Hatimae nilifanya maamuzi nayo yalikuwa nikumtumia ujumbe wa maandishi mpenzi wangu mpendwa issabella....ujumbe ulikuwa ni wa kumuomba msamaha issabella nikimwambia ajitahidi kusahau kuhusu mimi mwanaume ni siye kuwa na bahati ,na nikamsihi atafute mume mwingine ambaye ataishinae pamoja na mwanangu atakae zaliwa hapo baadae "ila iwapo kama itatokea mume wako akawa hampendi mwanangu haraka sana mrudishe nyumbani....ni hayo tu mpenzi Issabella najua jinsi gani umeumia ila hata mimi naumia sana huwenda zaidi yako kwaheri mpenzi please usitoe hiyo mimba maana mtoto atakae zaliwa ndie atakuwa kumbu kumbu yetu sote wawili."

Baada ya kumtumia ujumbe huo nilizima tena simu na kuitoa laini na nikaweka line nyingine mpya , nikaendelea kufanya maandalizi ya safari yangu safari ya arusha! ndio nilikuwa nimechukua maamuzi ya kwenda kwa bibi yangu arusha ,kutoka.a na hali iliyo nikuta niliona bora nikapumzishe akiri kwa bibi .

Saa kumi ya alfajri ya siku iliyofuata nilitoka nje ya geti letu nikiwa ndani ya gari la kulwa mama na baba waliniaga huku wakini sihi nisichukue maamuzi yoyote mabaya kwani wao wananipenda sana na kuathirika sio mwisho wa uhai ila nikifuata mashariti nitaishi vizuri sana....ndugu yangu kulwa alinipatia vidonge vingi sana vya ARV "mdogo wangu ukifuatisha mashariti ya vidonge hivi utaisha maisha marefu pengine kutupita sisi" kulwa alinisihi, wakanipeleka stendi na kuniacha ndani ya basi nikielekea arusha wao wakarudi nyumbani.

************-ARUSHA********
Niliona ndoto zangu zote za maisha ya badae zilikuwa zimefikia tamati kwani siku zote nilisoma kwa bidii na nilipo ajiliwa nilijituma sana kwani malengo yangu ilikuwa ni siku moja niwe mfanya biashara mkubwa ,Lakini sasa ndoto zote nilizizika maana niliona haina maana kufanya hayo yote wakati wakati natembea na kifo.
Jijini arusha niliishi maisha ya upweke sana nikiwa kwenye nyumba ya bibi iliokuwa na ndugu wengi..usoni niliwaonesha furaha na tabasamu kubwa lakini moyoni nilikuwa na majonzi tele.

Mara nyingi bibi alinipa moyo nakunisitizia nisiache kunywa vidonge nami nilimkubalia lakini nilikuwa si mkweli kwake kwani tangu nifike arusha sikuwahi kunywa kidonge hata kimoja ila nilikuwa navitupa kwenye sinki la choo na kuwaongopea nimekunywa, niliona haina maana ya kunywa vidonge na kuishi maisha ya kutumaini  vidonge vya ARV ambavyo nilitakiwa ninywe kila siku ...mimi niliona bora nisinywe ili nife haraka na kuiacha hii dunia iliyo sheheni visa maatatizo ya kila aina.

Ilipita miezi mitatu tangu nipate maambukizi ya virusi na nilikuwa sina mawasiliano ya aina yoyote kwa mpenzi wangu issabella , siku moja  nilipokea ujumbe wa Issabella alionitumia kwa njia ya email yangu ujumbe ulikuwa wa kuuchoma moyo wangu....."Kwako mpenzi wangu doto nimimi wako nikupendae kwa dhati  naakuandikia haya nikiwa nipo na pacha wako kulwa napenda kukujulisha kwamba familia yangu na familia yako imekaa na kuamua kwamba niolewe na kaka yako kulwa ili kuficha aibu yako kwa watu waliojua kua utanioa hivi karibuni ....hivyo siku ya harusi wengi watajua wewe ndio unanioa kwa  kuwa umefanana vyema na kaka yako kulwa ....kwa upande wangu mimi sina pingamizi la swala hili nakupenda sana mpenzi wangu dotto nakutakia maisha mema." ...

Jasho lilikuwa linanitoka baada ya kuisoma barua ile ilioumiza moyo wangu nikiwa bado nafikiria mara bibi aliniletea simu akisema mama kampigia anataka kuongea na mimi amepiga simu yangu haipatikani, nilichukua simu ile na kuiweka sikioni na kukutana na sauti ya mama ilio nisalimu kwa kunijali na baada ya salamu alinipatia taarifa ambayo nilisha isoma muda mchache uliopita ...mama yangu alinisihi na kunibembeleza kuwa nikaze moyo kuyashinda maumivu ya moyo
"Ahhh am usijali mama mimi hii mitahani nilisha ishinda" niliongea kwa kujikaza huku sauti yangu ikitetemeka
"Lakini mwanangu kama hujapendezwa na swalala kulwa kumuoa issabella niweke wazi ili swala hili lisifanyike" mama aliongea kwa kunibembeleza.
"Ah mama moyo wangu ni mkunjufu acha kulwa amuoe ili hata mwanangu akizaliwa asiteseke kwa baba asie nijua " niliumaliza mjadala huku moyo wangu ukiniuma sana...
"Haya kila la heri mwanangu mpendwa" mama aliongea na kukata simu.

Baada ya mama kukata simu niliwasha simu yangu kisha nikaziblack list namba ya kaka yangu kulwa na issabella kisha nikiblack list namba za marafiki wangu wa dar esalaam kisha nikablock akaunt zangu za mitandao ya kijamii ili siku ya harusi yao nisizione picha zao..

nikaendelea kuishi arusha huko moyo wangu ukiendelea kuwa kwenye maumivu makali na majeraha ya sio pona nikawa na isubiri kwa hamu siku yangu ya kufa kwani sikunywa dawa za dawa za kupunguza makaoi ya ukimwi makusudi ili nife mapema .

************************************

Ulipita mwaka mmoja na miezi minne tangu harusi ya Issabela na ndugu yangu ifanyike na nilishapata taarifa kuwa issabella alijifungua salama mtoto wakike alie mpatia jina la MARIA...nilimshukuru mungu kwa mwanangu kuzaliwa salama japo sikutaka kwenda kumuona ....nilikuwa sina mawasiliano na issabela wala kulwa hata taarifa ya kujifunguwa kwake nilipewa na mama kupitia simu ya bibi.

Afya yangu haikuwa nzuri nilikuwa nimedhohofika sana nilikonda sana mpenzi msomaji wa mkasa huu .

**"""TAHARUKI********

Katika hali yakutotegemea nililetewa taarifa kwamba kaka yangu amefariki dunia baada ya kuwawa na alie mua alikuwa ni mke wake ISSABELLA alie muoa mwaka mmoja uliopita..!!!! jeshi la polisi linamshikilia issabella kwa mauaji aliofanya.

Nikitu kigumu sana kuamini eti issabella amemua kulwa nilihisi kuchanganyikiwa sana siku iamini taarifa ile .
haraka nilifanya maandalizi ya safari ya kurudi jijini dar esalaam.

Niliwasili jijini dar es salaam na kukodi tax ilionifikisha nyumbani ambapo palikuwa na umati mkubwa watu , kufikia hapo moyo wangu ukathibitisha ni kweli kulwa amekufa nilishindwa kuyazuia machozi.

Msiba ulikuwa ni pigo la kushtukiza liliyo piga mioyo ya kila mwanafamilia, niliambiwa kuwa mtoto wa issabella ambae ni damu yangu yupo kwa shangazi kwani mama yake yupo rockup.

Nikiwa kwenye udhuni ile ya kumpoteza pacha wangu mara ilikuja taarifa nyingine ya kushutua  nayo ni kujinyonga mtuhumiwa alieshikiliwa na polisi kwa kufanya mauaji ya kaka yangu......Eti issabella alikuwa,
matukio haya  yalinifanye nihisi nipo ksenye ndotona muda wowote ningeshtuka kutoka usingizini.

"Issabella kajinyoga akisa rockup na katika kujinyonga kwake aliacha barua alioiandika kabla ya kujininginiza kwa kitambaa cha gauni lake." aljongea I.S.P aluoleta taarifa .

Nililetewa barua ile ilio achwa na issabella kwani marehemu aliandika ili ni fikie mimi ...

Nikaanza kuisoma huku nikitetemeka.....

"Habari mpenzi wangu nikupendae kwa dhati ni matumaini yangu ni mzima wa afya..nakuandikia haya ili upate kujua ukweli ambao umefichwa kwa muda mrefu...
mpenzi dotto ndoa ya mimi na kaka yako sio kwamba familia zetu zilikaa na kupanga ile ndoa, hapana ni kaka yako alianza kunitongoza baada ya wewe kuondoka na kwenda arusha , kaka yako alinishawishi sana akisisitiza anahitaji kuziba pengo lako na kunifuta maumivu ulioniachia alinisihi nimuone yeye kama wewe kwani mmefanana sana .
kila siku alinipigia na kunisihi sana na hatimae nikakubali kwani mioyo yetu bina damu imeumbwa kurubunika...mikakati yote ya ndoa aliifanya yeye huku familia yangu na yako ikimuunga mkono kwani walijua kwa ndoa ile wangeficha fedheha yako kuwa umeshindwa kunioa sababu una ukimwi.

Hatimae ndoa ilifungwa na watu wngi walijua kuwa wewe ndio umenioa...kaka yako alionesha kunipenda sana na aliijali mimba ulionipa kana kwamba yake hata mtoto alipozaliwa alimpenda sana.

Lakini tatizo limeibuka kuanzia wiiki tatu zilizo pita baada ya mimi kugundua kuwa kaka yako kuna vidonge anatumia kila siku anakunywa na nilipo fuatilia kimya kimya juzi nili fanikiwa kuviona vidoge vile kwenye begi lake la kazi nikagundua vile ni vidonge vya A R V vya kuzuia makali ya H I V , mpenzi niliogopa sana na sikutaka kuamini kwamba mume wangu ambae ni kaka yako ni MUATHIRIKA ikanilazimu kukaa na kumsubiri atoke kazini, nikaenda kumlaza mtoto wangu maria kwenye kitanda chake, kisha nikarudi sebuleni   nika kaa kumsubiri kaka yako huku nikiwa na vidonge vile mkononi... nili msubiri sana kwani alirudi saa tano usiku akiwa kalewa kidogo kwani ni kawaida yake kunywa siku moja moja....alipo niona nimeshika vidoge vile alishtuka sana na nilipo muuliza kwa hasira aliniomba msamaha na kukiri kuwa ni kweli yeye ni muathirika!!!!!!!!!!! nusu nipoteze fahamu kwa mshtuko.

Alikiri kuwa alipata maambukizi tangu akiwa chuo ila alifanya siri kiasi kwamba wazazi wako na wewe hamkujua swala lile na hakutaka mjue , .....na alifanikiwa.
Kaka yako aliongea huku machozi yakimtoka akiniomba nimsamehe kwani hata wakati wa ndoa alinidanganya na kuniletea vyeti bandia vilivyo thibitisha hana virusi hii ni kutokana alinipenda sana asinge weza kukubali kunikosa Kwani alikuwa ananipenda tangu nilipokuwa na wewe kwenye mahusiano yetu ya awali tulivyokuwa seondary....

Kaka yako alifichua siri nyingine nzito na kusema kuwa wewe huna virusi vya ukimwi ila siku ile tulipo enda kupima alikuzushia kwamba unaukimwi ile ndoto zako za kunioa zife kisha anioe yeye !!!!! na alifanikisha mpango wake...Mpenzi wangu wewe huna virusi vya ukimwi ...
Baada ya ndugu yako mshezi kuniambia hayo nililia sana kwani hata mtoto nilie mzaa nae ni muathirika baada ya mimi kuambukizwa na kaka yako kabla sijamzaa , roho iliniuma sana lakini alini bembeleza na nikamwambia nimemsamehe!! tukaenda kulala .

Hivi kwa ubaya ho alio ufanya marehemu kaka yako  ni mwana damu gani anaweza kumsamehe kaka yako?? ok acha nikumalizie mkasa.
usiku wa manane kaka yako akiwa kalala fofofo niliamka na kwenda jikoni ni kachukua kisu na kumsogelea marehemu kaka yako kisha kwa nguvu kubwa na kwakishindo nilizamisha kisukile kwenye kifua chak....."  ....***********

Ndugu msomaji nilishindwa kumalizia barua ile nguvu ziliniisha na nikahisi pumzi zikiniishia....

Issabela alikuwa amemua kulwa kumchoma kisu kwenye kifua chake upande wa kushoto na na kurudia mara kadhaa kitendo kile cha ukatili ..
. Mungu azilaze mahali pema roho za marehemu walio poteza uhai wao katika mkasa huu wa MUATHIRIKA, malaika wa faraja awafute machozi na kuwapa furaha watu wote wanaoishi na maambukizi ya ukimwi.

Mpenzi msomaji kupata ukimwi sio mwisho wa maisha yako lakini jihadhari ukimwi unaua....

0746206428 whatsup kwa maoni zaidi juu ya mkasa huu wa MUATHIRIKA.

MWISHO.

Huu ni mwisho wa simulizi hii ya muathirika ila jiandae kusoma kipande kingine kitakacho husu maisha ya mtoto maria ambae ni MUATHIRIKA.  simulizi hii imeandikwa na ndugu IDDI SIRAJI.

No comments:

Post a Comment

Iblame my body

RIWAYA   : I'BLAME MY BODY ( NAULAUMU MWILI WANGU ) Imezaminiwa na   Simulizimahiri.blogspot.com Mahakama kubwa ya kesi za jina...