Sunday, May 21, 2017

JERAHA LA MOYO (utangulizi)

SIMULIZI : JERAHA LA MOYO

      Utangulizi.

Mtunzi : iddi siraji

"Unajua kaka ABRAH jeraha kubwa huacha kovu na macho yanapo  tazama kovu lile hufanya ukumbuke kisa kilicho kufanya upate kovu lile, ila jeraha la moyo ni la aina yake hukufanya ulie na uwe na simanzi wakati wote kamwe halisahauliki japo ukitazama hulioni ,  ni aheri kuumia mguu ama kiungo chochote mwilini kwani utakiuguza na kupona , kuliko kupata jeraha la moyo jeraha ambalo husababishwa na hisia za kuachwa ama kusalitiwa na umpendae " aliongea kijana yule ambae ni rafiki yangu Gerrald ambae alikuwa ni mlemavu wa miguu nami nikawa makini kumsikilizi alicho kuwa anaongea.

"Binadamu unaweza kupoteza  vitu vingi sana ambavyo huku gharimu ghalama ghari ama  pesa nyingi....lakini mimi kuna kitu nilikipoteza na kushindwa kabisa kukirudisha , ,nilitamani ni uze  chochote cha thamani ili nipate pesa ya kuirudisha kitu hicho lakini imeshindikana.....hivi kaka Abrah  katika maisha umeshawahi kupoteza kitu cha thamani na chenye umuhimu wa kuku fanya ukose furaha??" aliniuliza kijana gerrald na kunifanya nishindwe kujibu nikatikisa kichwa kukataa kisha nae akaendelea kuongea.

"Basi mimi nimepoteza vitu muhimu katika maisha yangu ....nimepoteza miguu kama unavyoniona nimlemavu nimepoteza furaha mbaya zaidi nimebaki na jeraha moyoni mwangu linalo niumiza kila kukicha"  aliongea kwa unyonge sana nikahisi machozi yakinilenga na muda huo aliendelea kuongea.

"Siku nilio ipoteza miguu yangu na kubaki kilema ndio siku niliopata jeraha la moyo ambalo huniumiza zaidi ya maumivu ya kuikosa miguu yangu" safari hii aliongea kwa sauti ya chini yenye hisia za maumivu....  sikujua ni kitu gani rafiki yangu alitaka kunifahamisha siku hiyo , nikiwa kwenye hali ya sinta fahamu rafiki yangu huyo niliemtambua kwa jina la gerradi alianza kunisimulia mkasa ulio mkuta kwenye maisha yake.

Hii sio simulizi ya kuikosa ambayo utaipata kwa ofa .

Njoo whatsaapp nikutumie utangulizi huu kwa njia ya sauti  0746206428.

Huu ni mkasa mfupi wa aina yake ambao uta kuburudisha na kukufunza mengi.

Tuesday, April 4, 2017

CHOZI LA MILELE

SIMULIZI: CHOZI LA MILELE.

Binadamu unapozaliwa tu uhai wako na amani yako huishi kwenye mikono ya mama alie kuzaa japo mungu anakuwa ndio mlizi mkuu wa maisha yako.

Mama anapo amua kukufupishia uhai wako anaweza kutimiza kwa dakika chache haijalishi kwa kukupa sumu au kuziba pumzi kwa muda mrefu hii itategemea ni jinsi gani amekusudia kukufupishia uhai .

Wasichana wengi huchukua jukumu la kuharibu na kuzitoa mimba zao zinapokuwa changa kwa msukumo wa mazingira yaliyo mpelekea kupata mimba ile ama kwa sababu ya ugumu wa maisha na mazingira magumu anayo ishi,.
Wasichana wengine huenda mbali na kufanya maamuzi magumu pale anapo ilea mimba miezi tisa na kujifungua salama baada ya hapo humtupa mtoto na kumuacha katika mazingira hatarishi nae anaondoka na kutokomea, hufumba macho na kuyasahau mateso ya kutunza mimba ndani ya miezi tisa na yale machungu ya kujifungua .

Sijui ni ujasiri gani wanao utumia akina mama au ni roho mbaya kiasi gani wanayo kuwa nayo wakati ule wanapo watupa watoto walio wazaa wenyewe tena kwa uchungu....na sikitika sana kwani hata mama yangu alinitupa nikiwa mtoto mdogo mchanga akiniacha mazingira hatarishi .

Mungu msamehe mama yangu na wanawake wote wanao toa mimba na kuwatupa watoto....
Mimi ni Baraka matata. mwandishi na mtunzi wa simulizi hii ni ndugu Iddi Siraji  na imehaririwa na Lizbertha Maseke.

sasa isome na ujifunze.

Jina la baraka nilipewa na yule mama mgumba baada ya kuniokota nikiwa mtoto mchanga na kunifanya kuwa mwanawe mpendwa wa pekee na kwa hakika alinipa upendo ambao ulipindukia na alinipa malezi ambayo yalistahiki kwa kila mtoto japo alikuwa na maisha duni akijishughulisha na kilimo akiwa na mumewe mzee matata.

Yalikuwa ni maisha duni ya kutegemea kilimo cha mkono lakini baba na mama yule walijitahidi kunisomesha kwa kidogo kilicho patikana huku nami nikifanya bidii kwenye masoma na kuwasaidia kilimo kila nilipo rudi kutoka shule,.

Siku zote mama alinihimiza nisome kwa bidii kwani elimu ni urithi wa milele.

"Mwanangu nipo tayari kuuza hata mashamba ili mradi tu usome na ufike mbali...unadhani nisipo kupa elimu utapata urithi gani wa thamani pindi nikifumba macho" aliongea kwa kunisisitizia na kunifanya niwe makini sana ninapo kuwa darasani.

Mbali na kuwa saidia kulima wazazi wangu nilikuwa nina bustani zangu za mboga ambazo kila jumapili nilienda kuuza sokoni na kujipatia pesa ndogo zilizo niwezesha kununua vifaa vya shule na mafuta ya taa ya kibatali changu cha  kusomea usiku.

Hatimae juhudi zangu zilizaa matunda ni pale tu nilipo faulu kwa kishindo kutoka la saba kwenda kidato nilikuwa mwanafunzi wa  pili kati ya wanafunzi sita wa kwanza akiwa ni mtoto wa kike wa mwalimu mkuu wa shule ile ilio kuwa chini ki elimu na uhaba wa walimu.

Mama na baba mzee matata walifurahi kupita kiasi nina uhakika furaha yao ilizidi ya kwangu, waliuza mazao yaliyo patikana msimu ule kisha pesa iliyo patikana walininunulia vifaa vya shule na kunilipia ada ya shule kwani kipindi hicho cha mwaka 2005 elimu haikuwa bure kama sasa.

Hatimae siku zilifika nikajiunga na wenzangu katika shule ile ya sekondary....Bado mama alinisisitizia kuhusu swala la kujituma katika elimu huku safari hii akinisihi sana nijiepushe na makundi ya vijana wasio na maadili , nami nilizingatia hayo, siku zika songa nikijituma kwenye masomo pamoja na kazi za nyumbani.

***--**

Kama ilivyotokea mwaka 2005 basi ndivyo ilivyo jirudia mnamo 2009 kwani kwa mara nyingine nilifanikiwa kuziweka ndoto zangu mahala pazuri kwa kufaulu kutoka kidato cha nne kwenda cha tano.

Safari hii furaha yangu haikudumu sana kwani iliyayuka baada ya kujua kwamba kulikuwa na uwezekano wa kutoendelea na masomo kwa sababu ya ada kubwa na shule niliyopangiwa ilikuwa mbali sana.
Wazazi wangu wapendwa hawakuwa na uwezo wa kumudu gharama zile, nilijikuta nikikata tamaa machozi yakinitoka kila siku zilivyo karibia za kujiunga na kidato cha tano.

Siku moja baba aliniletea karatasi kadhaa na kuniambia ni chukue kalamu kisha nijaze ma swali ya form ile kisha niambatanishe na cheti changu cha kidato cha nne,
nami nilifanya vile nikajaza karatasi ile ilio sheheni maswali yalio nihusu mimi na elimu yangu , baada ya kufanya hivyo baba aliichukua barua ile na cheti changu na kuuondoka navyo bila kuniambia anapeleka wapi hii ni kawaida yake mzee matata huwa haweki mipango yake wazi hivyo sikutaka kujisumbua kumuuliza.

Baada ya siku sita tangu nijaze barua ile tulipokea ugeni wa watu ambao hakika walitoka serekalini tukawakaribisha,
"naona mmekuja mabwana...kijana mwenyewe ndio huyu" mzee matata aliongea baada ya kusalimiana na watu wale huku akinielekezea kidole mimi.
watu wale waliniuliza maswali kadhaa yenye misingi ya elimu wakijenga maada ya juu ya masomo ambayo huwa naya fanya vyema .

Nami niliwajibu kadri nilivyo weza.
walipo ridhishwa  walitazamana na kuafiki
"Ok mzee matata mwanao atajiunga  kwenye hiyo shule kwa msaada wa kitengo chetu hivyo aanze maandalizi" aliongea mmoja wa watu hao na hapo nilishindwa kuivumilia ile furaha iliyo ripuka ghafla kwenye moyo wangu.

Mzee matata alikuwa amefanya jitahada kubwa sana kwa kwenda kuomba msaada wa mimi kusomeshwa na alifanikiwa watu wale niliohisi wa serekalini walimkubalia nami nilitakiwa nikajiunge na wenzangu kwenye ile high school tena nilitakiwa nikaishi bweni.

Huo ndio ulikuwa msaada mwisho wa mzee matata!! msaada katika mafanikio yangu kwani nikiwa nipo shule miezi tisa tangu niondoke nyumbani nililetewa taarifa mbaya yenye kuumiza moyo wangu mzee matata alikuwa kapata ajali ya kugongwa na gari ! maskini mzee matata aliaga dunia na kumuacha mama mjane huku akiniachia kilio cha aina yake.

Nililia sana baada ya kupokea habari ile  na uongozi wa shule ukanifanyia msaada wa usafiri wa haraka ili niwahi mazishi.

Hayati mzee matata tulimzika katika hali ya udhuni iliopindukia huku akimuachia mama kilio kisicho bembelezeka.

Baada ya kumzika baba yangu mpendwa sasa macho yangu yalimuangalia mama yangu mpendwa ambaye nae hali yake kiafya haikuwa nzuri alikuwa kanyongea sana tena alidhohofika, hali ile ilinifanya nisitamami kurudi shule nikae kumuuguza mama yangu mpendwa, lakini mama alilipinga hilo na kuniamuru nirudi shule niendelee na masomo huku akidai udhoofu ule alionao ni sehemu ya ukiwa wa kufiwa na sio ugonjwa

Maskini mama kipenzi alipenda sana nisome kuliko kitu kingine , sikuwa na pingamizi kwani mitihani ilikuwa imekaribia ikanilazimu nirudi shule na kumuacha mama akilelewa na wanakijiji.

Wakati nikiendelea na mitihani shuleni nililetewa taarifa kuwa hali ya mama sio nzuri amelazwa hosptal hii ikanilazimu kumalizia mitihani haraka kisha nikarudi kijijini kwenye hospital aliyo lazwa mama.

Hali ya mama haikuwa nzuri hata kidogo alikuwa taabani akisumbuliwa na maradhi ya moyo bila shaka  ni kutokana na kifo cha baba.

Nikiwa na muuguza mama hospitalini pale siku moja alfajiri iliniita jina langu nami haraka nikaitika.

"Mwanangu baraka kunakitu nataka ni kujuuze leo hii" aliongea ni kauliza ni kitugani mama ?

"Unajua nilimpenda sana baba yako mzee matata na nilimkabidhi moyo wangu wote kwani ni wazi yeye pia alinipenda sana pengine kupita mimi kwani alikubali kuhama na mimi na kuondoka mkoa alio zaliwa akiepuka maneno ya ndugu zake walio mshawishi aniache na aoe mwanamke mwingine kwani mimi nilikuwa ni mgumba nisie weza kushika mimba" mama aliongea na kunyamaza kidogo kisha akaendelea"

"mzee matata hakukubaliana nao kabisa akahama nami kutoka mkoa aliozaliwa, ndugu zake wasijue tume hamia wapi .baba yako alinipenda sana kufikia hatua ya kukubali kuishi nami bila kupata mtoto lah! mzee matata alikuwa na upendo wa kweli kwangu.
siku moja usiku nilitoka nje kukojoa  kukiwa na hali ya mvua, na wakati narudi ndani nilisikia sauti ya mbwa akiunguruma huku akiburaza kitu nilipuuzia na kutaka kurudi ndani lakini hapo nikasikia chafya ya mtoto mchanga haraka nikawasha kurunzi yangu yenye mwanga hafifu  nikasogea upande huo ! masikini nilikuta kuna mtoto mchaga akisukwa sukwa na mbwa akiwa katupwa nilimfukuza mbwa huyo kisha nikamuita mzee matata tukamchukua huyo mtoto na kuingia nae ndani kwani mvua ilikuwa imeanza kunyesha bila ya mimi mvua ile ingechukua uhai wa mtoto au mbwa ange mdhuru mtoto huyo tukampa jina la BARAKA na kukufanya kuwa mwanetu mpendwa ukiwa ni baraka kutoka kwa mungu" Moyo wangu ulipata mshtuko mkubwa sana na kukumbwa na simanzi mara dufu baada ya kusikia maneno yale kutoka kwa mama na muda huo mama aliendelea kunisimulia
"mama yako alikuzaa akakutupa akiwa anaona hufai ila sisi ulitufaa japo hatuku kuzaa ila tulikufanya kuwa mwanetu ....baraka mimi sio mama yako ila nakupenda sana"

kufikia hapo nilikuwa na lia tu huku nikiwa siamini kuwa yule sio mama yangu  kilio kile kilichukua takribani dakika ishirini
"HAPANA MAMA WEWE NA MZEE MATATA NDIO MLIO NIZAA HAYO MANENO SIYAAMINI NAKUPENDA MAMA" niliongea huku nikilia lakini mama alikuwa kimya... naaam kimya cha milele!! alikuwa amesha iaga dunia akiniacha na chozi la milele.

Tayari mama alikuwa amefariki.

Mama yangu alitangulia mbele za haki akiniacha kwenye kilio kikubwa nililia sana zaidi ya unavyo fikiri msomaji, mbaya zaidi mama alikuwa amefichuwa siri nzito kuwa mimi waliniokota , swala lile liliniumiza sana ni bora asingeniambia kwani mimi nawajua wao ndio wazazi wangu na mpaka leo hii naandika haya moyo wangu una kiri kuwa wale ni wazazi wema japo hawakunizaa.

Ulikuwa ni msiba mkubwa sana kijijini pale , nae mama tulimzika karibu na kaburi la mumewe mpendwa mzee matata.
Baada ya mazishi yaliyo hudhuliwa na watu wengi huku waalimu kadhaa walio nipenda wakishiliki mazishi yale kisha nikarudishwa shuleni ili nika pumzike bwenini kwani pale kijijini sikuwa na ndugu mwingine  tofauti na wazazi wangu walio tangulia.

Hapo shuleni nilipewa wiki tatu za kupumzika kabla ya kurudi kwenye masomo...sikuwahi kuwaza kumtafuta mama yangu alie nizaa na kunitupa ila mara nyingi nilijiuliza ni kwanini alinitupa na kuniacha mazingira hatarishi .

Nilirudi tena kwenye masomo huku hali yangu kiafya ikiwa sio nzuri lakini nilijikaza kuushinda wakati ule wa majonzi

nilifanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha tano na sita na nilifaulu kwa matokeo mazuri kwenda chuo kikuu cha dar es salaam.

Jiji la dar nilikuwa nalisikia tu kwenye  vyombo vya habari lakini sasa nilipata nafasi ya kwenda kimasomo huku gharama zote zikisimamiwa na watu wale walio tafutwa na hayati mzee matata .

Miaka mitatu ya chuo ilinitosha kuhitimu vyema masomo yangu na kufikia hatuwa ya kuajiriwa kwenye kampuni ya wale wadhamini walio ni somesha huku asilimia ishirini na tano ya mshahara wangu wakichukuwa wao kama fidia .
Yalikuwa ni mafanikio ya haraka sana kwani watu wengi huhitimu chuo kisha hupata tabu kwenye swala la kuajiriwa , nilishukuru sana kwa mungu huku nikiukumbuka msaada wa mzee matata , nilisikitika sana kwani wazazi wale walio nilea vyema walikufa bila kuyaona mafanikio yale.
mshahara wangu wa kwanza niliuchukua na kwenda kijijini kujenga makaburi ya wazazi wangu wa pendwa na kuyaacha katika hali nzuri kisha pesa ilio bakia nikawagawia majirani ambao walikuwa bega kwa bega kwa mama yangu hadi umauti ulipo mfika, baada ya hapo nilirudi mjini ili kundelea na kazi.


Tayari nilikuwa nimesha fanikiwa kujenga nyumba kubwa na kuna msichana nilikuwa nime muoa, msichana huyo nilimkuta katika maisha ya kifukara akiishi na mama yake kwenye nyumba waliopanga baba yake akiwa alisha kufa. yeye na mama yake walikuwa kwenye maisha magumu lakini moyo wangu ulipendezwa na binti yule nika muoa na kufanga nae pingu za maisha.
kama wasemavyo wahenga ukipenda boga penda na ua lake, basi nilipo muoa binti yule nilimchukua na mama yake nikaishi nao nyumbani kwangu .

Msichana yule aliyeitwa joyce alikuwa mke mwema kwangu aliniheshimu na alinipenda sana .tulifanikiwa  kupata mtoto wa kiume nae nikamuita MATATA ,

Siku moja tukiwa wote mama mkwe na mimi na mke wangu niliamua kuwasimulia juu ya maisha yangu kwani walijua mimi ni yatima lakini hawakujua mengi ya maisha yangu.
Siku hiyo niliwasimulia tangu nilipo tupwa na mama alie nizaa nyuma ya ua wa mzee matata kisha nikaokotwa na wazee wale wakanilea.
stori ile ili wahudhunisha sana wakanipa pole, lakini nilikuwa nimefanya kosa kubwa kuwasimulia!!!!

Ilikuwa ni siku ya pili tangu familia yangu niisimulie kuhusu maisha yangu , siku hiyo niliwahi sana kutoka kazini nikanunua zawadi za mwanangu na mahitaji ya mama watoto.  lakini nilipo fika nyumbani furaha yangu ili yayuka na kuzitupa chini zawadi zile , kwanza nyumba ilikuwa kimya kabisa tofauti na siku zote na nilipoingia ndani nikakutana na balaa.

Kwanza nili muona mke wangu akiwa kalala sakafuni na mama mkwe alikuwa kalala kwenye kochi mwanangu matata akiwa kalala pembeni yake.

Loh! hii sijawahi kuona usingizi namna ile itawezekana vipi wasinzie fofofo muda ule wa saa kumi za jioni!

Haraka nikamsogelea mke wangu na nikamgusa kujaribu kumuamsha lakini hakuamka kabisa na mwili wake ulikuwa wa baridi!! , hata mama mkwe nae ile vile vile hadi mtoto wangu na wote wale hawakuwa wao ila ilikuwa ni miili yao tayari wamesha fariki.!!!!
Nilichanganyikiwa sikujua nini kimetokea ila niliona karatasi ikiwa mkonomi mwa mama mkwe nikaichukua ilikuwa ni barua  haraka nikaifungua na kuisoma.
   
Ndani ya barua ile nilikutana na jambo zito tena ilikuwa ngumu kuliamini na kulikubali kwani aliye iandika barua ile alikuwa ni mama wa mke wangu, aliandika kwamba yeye ndie yule msichana alie mtupa mtoto nje ya ua wa mzee matata !!!!!!, " Mwanangu kweli malipo ni hapa hapa duniani naona hata aibu kukutazama mwana nilie kutupa kisa ulikanwa na baba yako, jana ulipo simulia stori ya maisha yako nimejihakikishia kuwa wewe ndiwe nilie kutupa kisha nikakimbilia dar es salaam kuishi na mwanaume ambae na tulizaa huyu joyce ulie muoa naweza sema umemuoa dada yako ila wakulaaniwa ni mimi ...nisamehe kwa maamuzi nilio yachukua ya kuondoka na familia yako lakini nimefanya haya kwa kujiepushia aibu kwani wewe na mke wako ni mtu na dada yake japo baba tofauti ...nisamehe sana mwanangu ama hakika aibu kubwa imenikuta"

LA haullah! yule ndie alikuwa mama yangu. kwa mara nyingine niliangusha kilio kizito cha kuipoteza familia yangu machozi yalinitililika naam MACHOZI YA MILELE ama hakika hili ni CHOZI LA MILELE.

MWISHO.... 0746206428 Whatsup kwa maoni zaidi.

Kumbuka simulizi hii imeandikwa na ndugu Iddi Siraji na imehaririwa na dada Lizbertha Maseke.

® haki zote zimehifadhiwa.

Thursday, March 30, 2017

MUATHIRIKA

SIMULIZI : MUATHIRIKA

Mtunzi : Iddi Siraji
.................

Nilisahau kuwa hakuna furaha inayodumu milele hapa duniani niliona na bahati kubwa ilioje kupendwa na mtu nilie mpenda sana na niliona sasa ulikuwa wakati wangu wa mimi kuyaanza maisha mapya ya mume na mke kumbe mungu nae alikuwa amepanga la kwake, nilicho kiwaza mbele yangu ili kuwa ni kuishi maisha ya furaha na upendo kutoka kwa mpenzi ISSABELLA ....sikufikiria hata mara moja kama ndoa ile isinge fungika kwani nilijiamini sana mbele ya upendo mkubwa ulijengeka baina yangu na  issabela.... nilisahau kabisa kila unacho upanga mungu nae ana panga na kupangua ulicho panga.......

Nasikitika sana mpenzi msomaji kwani katika mkasa huu nimepoteza kila kitu furaha na watu wangu wa karibu.....mungu azilaze mahali pema roho za marehemu wote waliopoteza uhai katika mkasa huu wa MUATHIRIKA.
°°°°°°°°°°

ISABELLA alikuwa mwanamkee pekee alienipenda sana katika hii dunia licha yakuwa mimi ndo nilikuwa mwanaume wa kwanza kuujua usichana wake mimi nilikuwa mwanaume pekee kwenye swala mahusiano kwake , mara nyingi Isabella aliwahi kuniambia tangu aingie kwenye ulimwengu wa mahusiano mimi nimekuwa mwanaume wa kwanza kwake na hakuwahi kujaribu na mwanaume mwingine.

Maneno ya isabella yalinifanya nifurahi sana na kujiona wapekee kwa kukabidhiwa moyo na msichana mrembo isabella tangu nilipo kuwa nae shule ya sekondali mpaka anafika chuo hakuwahi kunisaliti, ila mimi nakiri kwamba mara kadhaa nilimsaliti na kuchepuka na wasichana fulani hii ni kutokana na wanaume tumeumbwa kutamani.

Isabella alipo kuwa chuo mwaka wa pili aliniletea habari kuwa yeye ni mjauzito amenasa ujauzito kutoka kwangu ile ilikuwa habari njema kwangu na kwake pia kwani issabella alithibitisha wazi furaha yake ya kubeba ujauzito niliompa na hakuwa tayari kuitoa hata kwa kulazimishwa.

Kwakuwa yeye alikuwa yupo chuo na mimi nilikuwa ni muajiliwa wa kampuni moja kubwa ya biashara hapa nchini mimi na Isabella tulipanga kufanya mikakati ya ndoa ili tukaishi maisha ya mume na mke na mtoto azaliwe ndani ya ndoa...
"Ila inabidi mpenzi wangu dotto tukapime afya zetu kwa ajili ya kiumbe kilichomo tumboni mwangu " mpenzi wangu isabella aliongea kwa sauti ya upendo.
"Kweli mpenzi wangu ila subiri zipite wiki mbili zipite nimalizie majukumu ya kiofisi sawa mama kijacho" nilimjibu kwa furaha
"sawa dotto...ila naomba hiyo siku tukapime kwenye ile hosptal anayo fanya kazi kaka yako kulwa" isabella aliongea na kuitaja hispatal ambayo pacha wangu kulwa alikuwa doctor pale....kwani sisi katika familia yetu tulizaliwa mapacha wawili naamu mapacha wa kufanana sana tulikuwa tuna fanana sana usinge weza kututofautisha kiurahisi yeye aliitwa kulwa nami niliitwa dotto, .

Basi bwana hatimae ile siku tuliyopanga tukapime kujua afya yetu ilifika , mida ya saa tano asubuhi tulifika kwenye hosptal ambayo kaka yangu kulwa alikuwa doctor mkubwa kwenye hiyo hosptal ilio sifika kutibu vizuri japo kwa gharama za juu.

Tuliingia kwenye ofisi ya kulwa ambae tulimkuta akipulizwa na kiyoyozi . baada ya salamu na maongezi mawili matatu basi ndugu yangu akaweka sawa vifaa vyake ili zoezi lililo tuleta lianze...

Kwanza alianza kupima Issabella ambae hakuonekana kuwa na wasiwasi hata kidogo...
"Ah shemeji yangu Isabella wewe huna tatizo damu yako ni safi kabisa" aliongea na kumpa mkono wa hongera mpaka hapo sikuwa na wasi wasi hata kidogo kama Issabella hana mimi naupataje nilijipa moyo kisha kaka yangu kulwa alienizidi saa moja kuliona jua katika kuzaliwa kwetu, akanipima na kabla hajatoa majibu alionekana kushtuka na kuwa kama haamini anacho kiona....
"vipi kaka"  nilihamaki
"No i think some mistake" alijibu kisha akarudia tena kunipima na kuangalia vipimo vyake ghafla sura yake iliingiwa na simanzi na mfadhaiko mkubwa huku safari hii machozi yakimlenga.

LAHAURA! vipimo vilisema mimi ni MUATHIRIKA....

Hakuna alie weza kuikabili simanzi ile ilio letwa na vipimo vilivyo thibitisha kuwa mimi nimuathirika ...Isabella alichanganyikiwa na muda huo pacha wangu alikuwa kainamia meza yake ya ofisi....sasa niliona dunia inazunguka kwa kasi kiasi cha kufanya ni hisi kizungu zungu..(inamaana kati ya jeska na mariamu mmoja wapo kaniambukiza virusi) nilijiuliza na kuwakumbuka wasichana wawili nilio chepuka nao kwa wakati tufauti mwezi mmoja nyuma.

Nikahisi kitu kizito kimenikaa kooni, nikajikuta nikisimama na kupiga hatua

"Dotto why .....nani kakuambukiza....." Issabella aliuliza huku akilia....

Nilishindwa kuvumilia nikafungua mlango na kutoka nje ya ofisi kulwa akajiribu kuniita lakini sikugeuka nyuma nikashusha ngazi za hospatal ile na kuelekea nilipo egesha gari haraka nikatoeka eneo lile.

Naam nilikuwa nina maambukizi ya virusi vya ukimwi na hili halikuwa pigo kwangu tu ilikuwa hadi kwa baba na mama niliwahudhunisha sana japo walijitahidi kunipa moyo na kuniambia ni ule ni ugonjwa kama magonjwa mengine lakini pamoja na kunipa moyo hudhuni yao ilionekana wazi.

Nilikata tamaa kwakila kitu lakini kila nilipo mfikiria issabella moyo wangu uliuma sana na alinipigia simu mara nyingi ila sikupokea kwani sikujua nimueleze nini.

Mara nyingine kaka yangu kulwa aliniletea simu akiniambia kuwa issabella anataka kuongea na mimi lakini nilikataa kabisa.

Hatimae nilifanya maamuzi nayo yalikuwa nikumtumia ujumbe wa maandishi mpenzi wangu mpendwa issabella....ujumbe ulikuwa ni wa kumuomba msamaha issabella nikimwambia ajitahidi kusahau kuhusu mimi mwanaume ni siye kuwa na bahati ,na nikamsihi atafute mume mwingine ambaye ataishinae pamoja na mwanangu atakae zaliwa hapo baadae "ila iwapo kama itatokea mume wako akawa hampendi mwanangu haraka sana mrudishe nyumbani....ni hayo tu mpenzi Issabella najua jinsi gani umeumia ila hata mimi naumia sana huwenda zaidi yako kwaheri mpenzi please usitoe hiyo mimba maana mtoto atakae zaliwa ndie atakuwa kumbu kumbu yetu sote wawili."

Baada ya kumtumia ujumbe huo nilizima tena simu na kuitoa laini na nikaweka line nyingine mpya , nikaendelea kufanya maandalizi ya safari yangu safari ya arusha! ndio nilikuwa nimechukua maamuzi ya kwenda kwa bibi yangu arusha ,kutoka.a na hali iliyo nikuta niliona bora nikapumzishe akiri kwa bibi .

Saa kumi ya alfajri ya siku iliyofuata nilitoka nje ya geti letu nikiwa ndani ya gari la kulwa mama na baba waliniaga huku wakini sihi nisichukue maamuzi yoyote mabaya kwani wao wananipenda sana na kuathirika sio mwisho wa uhai ila nikifuata mashariti nitaishi vizuri sana....ndugu yangu kulwa alinipatia vidonge vingi sana vya ARV "mdogo wangu ukifuatisha mashariti ya vidonge hivi utaisha maisha marefu pengine kutupita sisi" kulwa alinisihi, wakanipeleka stendi na kuniacha ndani ya basi nikielekea arusha wao wakarudi nyumbani.

************-ARUSHA********
Niliona ndoto zangu zote za maisha ya badae zilikuwa zimefikia tamati kwani siku zote nilisoma kwa bidii na nilipo ajiliwa nilijituma sana kwani malengo yangu ilikuwa ni siku moja niwe mfanya biashara mkubwa ,Lakini sasa ndoto zote nilizizika maana niliona haina maana kufanya hayo yote wakati wakati natembea na kifo.
Jijini arusha niliishi maisha ya upweke sana nikiwa kwenye nyumba ya bibi iliokuwa na ndugu wengi..usoni niliwaonesha furaha na tabasamu kubwa lakini moyoni nilikuwa na majonzi tele.

Mara nyingi bibi alinipa moyo nakunisitizia nisiache kunywa vidonge nami nilimkubalia lakini nilikuwa si mkweli kwake kwani tangu nifike arusha sikuwahi kunywa kidonge hata kimoja ila nilikuwa navitupa kwenye sinki la choo na kuwaongopea nimekunywa, niliona haina maana ya kunywa vidonge na kuishi maisha ya kutumaini  vidonge vya ARV ambavyo nilitakiwa ninywe kila siku ...mimi niliona bora nisinywe ili nife haraka na kuiacha hii dunia iliyo sheheni visa maatatizo ya kila aina.

Ilipita miezi mitatu tangu nipate maambukizi ya virusi na nilikuwa sina mawasiliano ya aina yoyote kwa mpenzi wangu issabella , siku moja  nilipokea ujumbe wa Issabella alionitumia kwa njia ya email yangu ujumbe ulikuwa wa kuuchoma moyo wangu....."Kwako mpenzi wangu doto nimimi wako nikupendae kwa dhati  naakuandikia haya nikiwa nipo na pacha wako kulwa napenda kukujulisha kwamba familia yangu na familia yako imekaa na kuamua kwamba niolewe na kaka yako kulwa ili kuficha aibu yako kwa watu waliojua kua utanioa hivi karibuni ....hivyo siku ya harusi wengi watajua wewe ndio unanioa kwa  kuwa umefanana vyema na kaka yako kulwa ....kwa upande wangu mimi sina pingamizi la swala hili nakupenda sana mpenzi wangu dotto nakutakia maisha mema." ...

Jasho lilikuwa linanitoka baada ya kuisoma barua ile ilioumiza moyo wangu nikiwa bado nafikiria mara bibi aliniletea simu akisema mama kampigia anataka kuongea na mimi amepiga simu yangu haipatikani, nilichukua simu ile na kuiweka sikioni na kukutana na sauti ya mama ilio nisalimu kwa kunijali na baada ya salamu alinipatia taarifa ambayo nilisha isoma muda mchache uliopita ...mama yangu alinisihi na kunibembeleza kuwa nikaze moyo kuyashinda maumivu ya moyo
"Ahhh am usijali mama mimi hii mitahani nilisha ishinda" niliongea kwa kujikaza huku sauti yangu ikitetemeka
"Lakini mwanangu kama hujapendezwa na swalala kulwa kumuoa issabella niweke wazi ili swala hili lisifanyike" mama aliongea kwa kunibembeleza.
"Ah mama moyo wangu ni mkunjufu acha kulwa amuoe ili hata mwanangu akizaliwa asiteseke kwa baba asie nijua " niliumaliza mjadala huku moyo wangu ukiniuma sana...
"Haya kila la heri mwanangu mpendwa" mama aliongea na kukata simu.

Baada ya mama kukata simu niliwasha simu yangu kisha nikaziblack list namba ya kaka yangu kulwa na issabella kisha nikiblack list namba za marafiki wangu wa dar esalaam kisha nikablock akaunt zangu za mitandao ya kijamii ili siku ya harusi yao nisizione picha zao..

nikaendelea kuishi arusha huko moyo wangu ukiendelea kuwa kwenye maumivu makali na majeraha ya sio pona nikawa na isubiri kwa hamu siku yangu ya kufa kwani sikunywa dawa za dawa za kupunguza makaoi ya ukimwi makusudi ili nife mapema .

************************************

Ulipita mwaka mmoja na miezi minne tangu harusi ya Issabela na ndugu yangu ifanyike na nilishapata taarifa kuwa issabella alijifungua salama mtoto wakike alie mpatia jina la MARIA...nilimshukuru mungu kwa mwanangu kuzaliwa salama japo sikutaka kwenda kumuona ....nilikuwa sina mawasiliano na issabela wala kulwa hata taarifa ya kujifunguwa kwake nilipewa na mama kupitia simu ya bibi.

Afya yangu haikuwa nzuri nilikuwa nimedhohofika sana nilikonda sana mpenzi msomaji wa mkasa huu .

**"""TAHARUKI********

Katika hali yakutotegemea nililetewa taarifa kwamba kaka yangu amefariki dunia baada ya kuwawa na alie mua alikuwa ni mke wake ISSABELLA alie muoa mwaka mmoja uliopita..!!!! jeshi la polisi linamshikilia issabella kwa mauaji aliofanya.

Nikitu kigumu sana kuamini eti issabella amemua kulwa nilihisi kuchanganyikiwa sana siku iamini taarifa ile .
haraka nilifanya maandalizi ya safari ya kurudi jijini dar esalaam.

Niliwasili jijini dar es salaam na kukodi tax ilionifikisha nyumbani ambapo palikuwa na umati mkubwa watu , kufikia hapo moyo wangu ukathibitisha ni kweli kulwa amekufa nilishindwa kuyazuia machozi.

Msiba ulikuwa ni pigo la kushtukiza liliyo piga mioyo ya kila mwanafamilia, niliambiwa kuwa mtoto wa issabella ambae ni damu yangu yupo kwa shangazi kwani mama yake yupo rockup.

Nikiwa kwenye udhuni ile ya kumpoteza pacha wangu mara ilikuja taarifa nyingine ya kushutua  nayo ni kujinyonga mtuhumiwa alieshikiliwa na polisi kwa kufanya mauaji ya kaka yangu......Eti issabella alikuwa,
matukio haya  yalinifanye nihisi nipo ksenye ndotona muda wowote ningeshtuka kutoka usingizini.

"Issabella kajinyoga akisa rockup na katika kujinyonga kwake aliacha barua alioiandika kabla ya kujininginiza kwa kitambaa cha gauni lake." aljongea I.S.P aluoleta taarifa .

Nililetewa barua ile ilio achwa na issabella kwani marehemu aliandika ili ni fikie mimi ...

Nikaanza kuisoma huku nikitetemeka.....

"Habari mpenzi wangu nikupendae kwa dhati ni matumaini yangu ni mzima wa afya..nakuandikia haya ili upate kujua ukweli ambao umefichwa kwa muda mrefu...
mpenzi dotto ndoa ya mimi na kaka yako sio kwamba familia zetu zilikaa na kupanga ile ndoa, hapana ni kaka yako alianza kunitongoza baada ya wewe kuondoka na kwenda arusha , kaka yako alinishawishi sana akisisitiza anahitaji kuziba pengo lako na kunifuta maumivu ulioniachia alinisihi nimuone yeye kama wewe kwani mmefanana sana .
kila siku alinipigia na kunisihi sana na hatimae nikakubali kwani mioyo yetu bina damu imeumbwa kurubunika...mikakati yote ya ndoa aliifanya yeye huku familia yangu na yako ikimuunga mkono kwani walijua kwa ndoa ile wangeficha fedheha yako kuwa umeshindwa kunioa sababu una ukimwi.

Hatimae ndoa ilifungwa na watu wngi walijua kuwa wewe ndio umenioa...kaka yako alionesha kunipenda sana na aliijali mimba ulionipa kana kwamba yake hata mtoto alipozaliwa alimpenda sana.

Lakini tatizo limeibuka kuanzia wiiki tatu zilizo pita baada ya mimi kugundua kuwa kaka yako kuna vidonge anatumia kila siku anakunywa na nilipo fuatilia kimya kimya juzi nili fanikiwa kuviona vidoge vile kwenye begi lake la kazi nikagundua vile ni vidonge vya A R V vya kuzuia makali ya H I V , mpenzi niliogopa sana na sikutaka kuamini kwamba mume wangu ambae ni kaka yako ni MUATHIRIKA ikanilazimu kukaa na kumsubiri atoke kazini, nikaenda kumlaza mtoto wangu maria kwenye kitanda chake, kisha nikarudi sebuleni   nika kaa kumsubiri kaka yako huku nikiwa na vidonge vile mkononi... nili msubiri sana kwani alirudi saa tano usiku akiwa kalewa kidogo kwani ni kawaida yake kunywa siku moja moja....alipo niona nimeshika vidoge vile alishtuka sana na nilipo muuliza kwa hasira aliniomba msamaha na kukiri kuwa ni kweli yeye ni muathirika!!!!!!!!!!! nusu nipoteze fahamu kwa mshtuko.

Alikiri kuwa alipata maambukizi tangu akiwa chuo ila alifanya siri kiasi kwamba wazazi wako na wewe hamkujua swala lile na hakutaka mjue , .....na alifanikiwa.
Kaka yako aliongea huku machozi yakimtoka akiniomba nimsamehe kwani hata wakati wa ndoa alinidanganya na kuniletea vyeti bandia vilivyo thibitisha hana virusi hii ni kutokana alinipenda sana asinge weza kukubali kunikosa Kwani alikuwa ananipenda tangu nilipokuwa na wewe kwenye mahusiano yetu ya awali tulivyokuwa seondary....

Kaka yako alifichua siri nyingine nzito na kusema kuwa wewe huna virusi vya ukimwi ila siku ile tulipo enda kupima alikuzushia kwamba unaukimwi ile ndoto zako za kunioa zife kisha anioe yeye !!!!! na alifanikisha mpango wake...Mpenzi wangu wewe huna virusi vya ukimwi ...
Baada ya ndugu yako mshezi kuniambia hayo nililia sana kwani hata mtoto nilie mzaa nae ni muathirika baada ya mimi kuambukizwa na kaka yako kabla sijamzaa , roho iliniuma sana lakini alini bembeleza na nikamwambia nimemsamehe!! tukaenda kulala .

Hivi kwa ubaya ho alio ufanya marehemu kaka yako  ni mwana damu gani anaweza kumsamehe kaka yako?? ok acha nikumalizie mkasa.
usiku wa manane kaka yako akiwa kalala fofofo niliamka na kwenda jikoni ni kachukua kisu na kumsogelea marehemu kaka yako kisha kwa nguvu kubwa na kwakishindo nilizamisha kisukile kwenye kifua chak....."  ....***********

Ndugu msomaji nilishindwa kumalizia barua ile nguvu ziliniisha na nikahisi pumzi zikiniishia....

Issabela alikuwa amemua kulwa kumchoma kisu kwenye kifua chake upande wa kushoto na na kurudia mara kadhaa kitendo kile cha ukatili ..
. Mungu azilaze mahali pema roho za marehemu walio poteza uhai wao katika mkasa huu wa MUATHIRIKA, malaika wa faraja awafute machozi na kuwapa furaha watu wote wanaoishi na maambukizi ya ukimwi.

Mpenzi msomaji kupata ukimwi sio mwisho wa maisha yako lakini jihadhari ukimwi unaua....

0746206428 whatsup kwa maoni zaidi juu ya mkasa huu wa MUATHIRIKA.

MWISHO.

Huu ni mwisho wa simulizi hii ya muathirika ila jiandae kusoma kipande kingine kitakacho husu maisha ya mtoto maria ambae ni MUATHIRIKA.  simulizi hii imeandikwa na ndugu IDDI SIRAJI.

Thursday, February 23, 2017

SIMULIZI ZA PICHA http://simulizimahiri.blogspot.com/2017/02/simulizi-za-picha.html

Monday, January 9, 2017

SEHEMU YA TATU

RIWAYA ;ROAD 2017
MTUNZI ;IDDI SIRAJI
WHATS'AAP-0746206428

  Usiku wa kafara..

ilipoishia.....

Gola akamuinua diana ambae hakuwa na fahamu kabisa akamuweka begani kisha akamtazama mama diana kwa macho ya chuki.
gola akageuka na kutikomea akiwa na diana begani...

"Haya mliobakia anzenu ibada ya kukaribisha sadaka ya usiku huu wa kafara"..

endelea..

31December.
Baraka alishuka na kwenda mbele ya gari na kufunua lile bati linayo ifunika injini na hapo macho yake yaka kutana na moshi kutokea kwenye injini.

"Dah gari imechemsha tukisema tuisubiri ipoe inabidi tukae saa zima ....ila kutoka hapa hadi kwenye mashine ya wind walter ni kama dakika kumi na tano hivyo napendelea tukachukue maji huko ili tusichelewe sana"  baraka aliongea huku akiliangalia gari lake lilio fuka moshi...
baraka alikuwa mzoefu wa barabara  hii mara nyingi alishawahi kuitumia na kutembea sana eneo la wind walter

"dah hii ilishakuwa mbaya na mama nilimuahidi nitampigia jioni mpaka sasa hivi saa mbili usiku sijampigia na hapa naona mtandao haukamati" sarah alilaani maana alijua muda ule wazazi wake wanamtafuta kwenye simu...
"Ah usijal chukua tablet yangu  uwa pigie kwa namba yangu ya zantel maana zantel hapa ina kata kwa njia ya satelite" baraka alio ngea kisha akawageukia gadyson na john
"oya wazee wa kazi tufanye maamuzi ya haraka" baraka aliwasihi
"ok kama vipi hawa bibie tuwaache sisi tukachukue hayo maji haraka" john aliongea na muda huo baraka akafungua mlango wa mizigo na kuchukua dumu lisilo na kitu ndani kisha akamsogelea neema.
"sasa jamani tunawaacha humu kwenye  gari sisi tunakuja haraka" baraka aliongea na kumbusu neema kwenye paji la uso(neema na baraka walikuwa na mahusiano ya kimapenzi"

John nae alimsogelea msichana dolla na kumbusu kwenye midomo yake..."kuwa na amani sawa mpenzi" john aliongea baada ya kumpiga busu na dolla alitikisa kichwa kuafiki. ..pia john na dolla walikuwa ni wapenzi

Ni sarah pekee ndie alikuwa msichana asie kuwa na mpenzi kwenye safiri ile yeye mpenzi wake alikuwa akimsubiri kwenye ile hotel walio panga kwenda kushrehekea mwaka mpya pale bagamoyo.

Gadyson nae hakuwa na mpenzi kwenye safari ile ila kuna wakati alijaribu kumchombeza sarah walipo kuwa mbugani mikumi, lakini sarah alionesha msimamo na gadyson akawa kalifutilia mbali lile swala.

Baraka akachomoa ufunguo wa gari yake na kuutia mfukoni akiwa na kidumu aliwasha touch yake yenye mwanga mkali akaaanza kuongoza njia akiwaongoza john na gady kuelekea kwenye maji wakiwaacha wasichana watatu ndani ya gari.

Tayari ilikuwa ni saa mbili usiku na upande wa magharibi mwezi mkubwa wa kuvutia ulikuwa una chomoza.

Kile kikosi cha vijana mbweha kikiongozwa na mzee juma kilikuwa kime wasili eneo lile kwa usiri na  ukimya wa hali ya juu  na wao walikuwa upande wa pili wa barabara na waliwashuhudia akina baraka wakiwaacha wasichana ndani ya gari na wao wakitokomea ndani ya msitu.

"sasa watu watatu wafuateni hao wa kiume sisi tunaenda kuwakamata hao wasichana wao tuna wapeleke kwa goroza" mzee juma aliongea na muda huo vijana watatu wakainuka na kuwafuata kina baraka ...vijana watatu hao walifuata kwa kuwazunguka na kwa mwendo wa ukimya mkubwa.

"dalu wanyatie kimya kimya na wasikuone ukifika jaribu kuufungua mlango wa gari" mzee juma aliongea na kijana dalu akiwa na panga aliondoka akiwa kajikunja kuanzia kiunoni huku aki hama mti hadi mti akihofia ule mwanga wa mbala mwezi usije kumfanya aonekane.

Ilimchukua dakika kumi na mbili  kufika pale kwenye gari ali kokota kokota akiwa anatembele magoti aliufikia mlango na kujaribu kuvuta kile kitasa lakini haukufunguka  akauwacha na kutambaa tena ili akajaribu kufungua mlango wa upande mwingine..

Ndani ya gari wasichana hawakutambua lolote dolla na neema walikuwa wakisikiliza mziki kwenye ear phone na sarah alikuwa busy na tableti akihamisha namba za wazazi wake ili awapigie.....

Baraka na wenzake walitembea kama dakika kumi  kisha akasita kichwani kwake akiwa kuna kitu amekumbuka
"ah nime fanya ujinga ujue humu ni mstuni na kuna wadudu wa na wanyama siku paswa kuiacha bunduki"  baraka aliongea huku akisimama
"ilo nalo neno" gadyson alijibu
"ok ikimbilie sisi tuna kusubiri hapa" john aliongea na baraka akaweka dumu chini akaanza kukimbia kuirudia bunduki yake huku touch yake ikimulika msituni mule  ipasavyo .

Dalu wakati ule ana zunguka ghafla aliona mwanga wa touch kwa mbali ukija kueleke kwenye gari akahamaki na haraka akajua kina baraka wana kuja... haraka dalu akaingi uvunguni mwa gari...

Sarah alijaribu kumpigia  mama yake lakini mama yake alipo pokea simu sarah aliisikia sauti  ya mama yake lakini mama yake hakumsikia sarah..
"dah mtandao una sumbua kweli" sarah alisema na hapo akaona mwanga wa touch ukija upande wao  "oh mara hii wamesha pata maji... ngoja nishuke nimpigie mama huenda nje ya gari nitaongea nae vizuri" sarah aliongea na kutoa lock ya mlango na kushuka akakifuata kisiki cha mti wa mbuyu akakipanda mara moja na kuanza zoezila kumpigia mama yake..

na muda huo baraka nae alikuwa ameisha ifikia gari...

nini kita tokea hapo ?
vipi gadyson na john ? iwapo watatokewa na wale vijana watatu waliotumwa na mzee juma.

like share iendeleee

Iblame my body

RIWAYA   : I'BLAME MY BODY ( NAULAUMU MWILI WANGU ) Imezaminiwa na   Simulizimahiri.blogspot.com Mahakama kubwa ya kesi za jina...