Friday, December 9, 2016

NAKUPENDA EPSODE 2

KIPANDE CHA PILI

Moyo wa ALEX mjomba ake GODNAND uliuzunika sana

.mtoto wa dada yake alimpanda kichwani, akukubali kirahisi akaamua kufanya jambo!

Jambo ambalo alijua ndo la muhimu kulifanya kabla ajachukua hatua mbaya zaidi kwa mtoto yule alomkosea heshima.

."ni lazima niwaitee wazee wa koo wamkanye la sivyo nita onekana natesa toto la mtu!"

Akajiwazia na kukubaliana na jibu lake la kuandaa mbuzi kwa wana ukoo kuweka kikao cha kuwajuza.

siku ya siku ikawadia...akiwa mbele ya wazee wa ukoo akaanza kueleza

"Wazee wangu!,nyinyi ndo mmeniteua kuongoza mali za dada yangu!,
nikakubali kwa moyo mweupeee!,
ila sasa huyu mjomb angu mtoto mkubwa wa dada GOD alipofikia ni pabaya,

ajali kama mimi ni mjomba ake...

.(miguno ya wazee wale ika shamiri ila ilo alikufanya kijana yule aache kueleza!"

ananijibu atakavyo,na mbaya zaidi anaitaji nimkabidhi hati za mashamba na nyumba pia!"

"haaa!"

miguno ikarejea

"ilo aliwezekani!" mzee mmoja akatamka

"ni mtoto mdogo huyo awezi sema haya!"

babu mwingine alimtetea GOD,

wengine wote wakamuunga mkono!

"embu aitwe haraka huyo GOD tutajua mkwel ni yupi!"

mzee mwingine alokuwa kimya muda wote naye akatoa dukuduku lake lililoungwa mkono na wazee wote,

alex akanyanyuka na kwenda kumuita god alokuwa ndani muda wote

"sikia wazee wangu bora hata mmekuja!,.....mimi nishakuwa na najua zuri na baya,ivyo uwezo wa kuziongoza mali za marehemu mama yangu nnao hvyo nshamwambia huyu siku nyingi hataki kunisikia naombeni mali zangu

lasivyo!,..

Lasivyo kwenye hii kaya patawaka moto"

Aliongea GOD kwa hasira! wazee wote walibaki na butwaa,pasina kuamini kuwa maneno yale  yalitoka kwa mtoto yule
GOD akaondoka na alipoufikia mlango wa kuingilia ndani akageuka

" na msipofanya ivyo sitosita kumwaga damu ya mtu nimemaliza."

alivyomaliza akaingia ndani.hasira za wazee wa ukoo zikawapanda,waliona ni jambo la ajabu kwa mtoto kama GOD kuwadharau,na kukiuka mila na desturi.
wakampa idhini mjomba amfanye chochote mtoto yule wakimtoa rasmi katika ukoo wao.ni jambo ambalo ALEX alilisubiria!...


Sent from my Vodacom Smart

No comments:

Post a Comment

Iblame my body

RIWAYA   : I'BLAME MY BODY ( NAULAUMU MWILI WANGU ) Imezaminiwa na   Simulizimahiri.blogspot.com Mahakama kubwa ya kesi za jina...