Tuesday, June 6, 2017

More Than Pain

Story: More Than Pain
Ep: 01
Mtunzi: Abdulkarim
www.facebook@dee lovee
Ni juma pili moja tulivu iliyokuwa imeangukia tarehe 14 ya mwezi wa pili. ktk siku hiyo kulikuwa na sikukuu maalum ya wapendanao maarufu kama Valentine day
Rangi za upendo zilitawala kwa kila aliyekuwa akiithamini siku hiyo huku kila mmoja akiitumia kusherekea na ampendae jinsi anavyojua ... Kwa upande wa Alan alipanga kuisherekea siku hiyo kwa kufunga ndoa na mpenzi wake ambaye alizaliwa tarehe kama hiyo na kupewa jina la Valentina.
Ndoto zao siku nyingi ilikuwa ni kufunga ndoa siku hiyo ili wawe wanaazimisha sherehe mbili kwa mpigo kwa kila mwaka yani Siku ya kuzaliwa kwa Valentina lakini pia itakuwa ni siku yao ambayo waliafunga ndoa na itakuwa sherehe ya wapendano Duniani kote
Familia ya Valentina walikuwa na uwezo wa hali ya juu na walikuwa na wamepanga kumfanyia sherehe ya kufa mtu binti yao baada ya kutoka kufunga ndoa na Alan ... "Unanitia simanzi Shangazi kwa nini muda wote unalia wakati leo ni siku yako muhimu ktk maisha yako?" .. Shangazi yake Valentina alimwambia baada ya kumuona Valentina akiwa analia muda wote wakati anapambwa .. Valentina alionekana kama mtu ambaye alikuwa na kitu moyoni lakini aliogopa kusema kwa sababu alikuwa akiogopa ... "Sawa unaolewa lakini tambua kuwa ndoa yako itaondoka na roho yangu Nakupenda sana Valentina na sitoacha kukupenda naomba utambue hilo swala" .. Ni maneno ambayo yalikuwa yanapita kichwani kwa Valentina na alijua mwenyewe sijui ni nani aliyemwambia maneno hayo
Kwa jinsi Valentina alivyokuwa akipendana na Alan hakuna mtu ambaye aliyeisi labda Valentina hakutaka kolewa na Alan na uenda Valentina analia kwa sababu ya furaha na hakuamini kama kweli siku hiyo anafunga ndoa na mpenzi wake tena yeye akiwa mtu ambaye aliependekeza harusi yake hiwe siku hiyo.
*****
Kwa upande wa Alan siku hiyo alipendeza na kumfanya awe na mvuto zaidi muda wote alikuwa akitabasam na kutaniana na watu wake wa karibu .. "Unajiskiaje leo kufunga ndoa na Valentina?" .. Kaka ya Alan anayeitwa Franco alimuuliza na kumfanya Alan acheke kidodo na kumwambia .. "Najisikia poa, japokuwa kuna kajiuwoga fulani kamenishika ila nafurahi sana kufunga ndoa na Valentina mwanamke wa maisha yangu. Siku zote nampenda Valentina naye ananipenda mimi na nafurahi kuona tunapendana naami kwa kitendo cha mimi kuishi na yeye kitakuwa cha mafanikio kwangu na kwake pia' ... Alan aliongea kwa kujiamini na Kaka yake alizidi kumtania na kumtisha kuwa ndoa ni ngumu
*****
Vaentina aliendelea kulia mfululizo na sasa kuanza kuwaogopesha ndugu zake na kumuuliza kipi ambacho analilia ... Aliogopa kuwaambia ukweli na kuwaficha kuwa haamini kama kweli yeye na Alan wanaingia katika kitu ambacho kilikuwa ndotoni mwake siku zote .. ndugu walijitaidi kumbeleza na kumsihii anyamaze na afurahie jambo ilo na siyo kulia kumbe hawakujua mwenzao analia ana yake yanayomsibu
Atimaye kile kitu ambacho kilikuwa kinasubiliwa na wengi ktk siku hiyo ya wapendanayo kilitimia ...Bibi na bwana harusi walipendeza na kuwafanya watu wapige vigelegele na kuwashangilia, tayari kufungishwa pingu za maisha ... Yale maneno yaliendelea kupita kichwani mwa Valentina na muda wote alikuwa akilia moyoni akijitaidi machozi yasimtoke .. alijiona mkosefu sana kumkatali mtu aliyemwambia yale maneno. lakini alikuwa akimfikilia sana Alan ingekuaje kama angemwambia kuwa hataki kuolewa na yeye wakati siku zote yeye ndiye aliyekuwa akipiga kelele kuhusu ndoa na diye aliyepanga wafunge ndoa siku hiyo ya wapendanao ili hiwe kumbukumbu nzuri katika maisha yake ... Valentina aliendelea kujiuliza maswali baila ya kupata majibu yake aliogopa sana kumuua mtu kwa sababu yake lakini pia aliogopa kama angemwambia Alan wasifunge ndoa kabla
Alan aliulizwa kama yupo tayari kumuoa Valentina na alijibu kukubali kwa moyo mkunjufu huku akitabasamu na baada ya kujibu mala tatu, ilikuwa ni zamu ya Valentina ... "Valentina Brown upo tayari kuolewa na ndugu Alan George awe mume wako wa ndoa mwende mkaishi kwa shida na raha?" ... Valentina hakujibu swali badala yake alitizama chini na kuzidi kulia mfululizo ... "Samahani sana Alan kwa hili nitakalo amua" ... Valentina aliongea mwenyewe kichwani mwake .. Aliulizwa tena swali kwa mala ya pili lakini hakujibu ... Alan na kila aliyekuwa pale aliapatwa na bumbuwazi na hakuna aliyejua kinachoendelea ..... Wakati anaulizwa kwa mala ya tatu akanyanyua sura yake na kuongea kwa jazba ... "Sitaki kuolewa na wewe Alan sikupendi, Nakuchukia sana Alan" ... Valentina aliongea kwa uchungu na kukimbia na kuwafanya watu wote wamshangae ...... Nini kitaendelea? ... Nani anayemchanganya Valentina na kwa nini? Tukutane katika Ep ya 02

Iblame my body

RIWAYA   : I'BLAME MY BODY ( NAULAUMU MWILI WANGU ) Imezaminiwa na   Simulizimahiri.blogspot.com Mahakama kubwa ya kesi za jina...