SIMULIZI : JERAHA LA MOYO
Utangulizi.
Mtunzi : iddi siraji
"Unajua kaka ABRAH jeraha kubwa huacha kovu na macho yanapo tazama kovu lile hufanya ukumbuke kisa kilicho kufanya upate kovu lile, ila jeraha la moyo ni la aina yake hukufanya ulie na uwe na simanzi wakati wote kamwe halisahauliki japo ukitazama hulioni , ni aheri kuumia mguu ama kiungo chochote mwilini kwani utakiuguza na kupona , kuliko kupata jeraha la moyo jeraha ambalo husababishwa na hisia za kuachwa ama kusalitiwa na umpendae " aliongea kijana yule ambae ni rafiki yangu Gerrald ambae alikuwa ni mlemavu wa miguu nami nikawa makini kumsikilizi alicho kuwa anaongea.
"Binadamu unaweza kupoteza vitu vingi sana ambavyo huku gharimu ghalama ghari ama pesa nyingi....lakini mimi kuna kitu nilikipoteza na kushindwa kabisa kukirudisha , ,nilitamani ni uze chochote cha thamani ili nipate pesa ya kuirudisha kitu hicho lakini imeshindikana.....hivi kaka Abrah katika maisha umeshawahi kupoteza kitu cha thamani na chenye umuhimu wa kuku fanya ukose furaha??" aliniuliza kijana gerrald na kunifanya nishindwe kujibu nikatikisa kichwa kukataa kisha nae akaendelea kuongea.
"Basi mimi nimepoteza vitu muhimu katika maisha yangu ....nimepoteza miguu kama unavyoniona nimlemavu nimepoteza furaha mbaya zaidi nimebaki na jeraha moyoni mwangu linalo niumiza kila kukicha" aliongea kwa unyonge sana nikahisi machozi yakinilenga na muda huo aliendelea kuongea.
"Siku nilio ipoteza miguu yangu na kubaki kilema ndio siku niliopata jeraha la moyo ambalo huniumiza zaidi ya maumivu ya kuikosa miguu yangu" safari hii aliongea kwa sauti ya chini yenye hisia za maumivu.... sikujua ni kitu gani rafiki yangu alitaka kunifahamisha siku hiyo , nikiwa kwenye hali ya sinta fahamu rafiki yangu huyo niliemtambua kwa jina la gerradi alianza kunisimulia mkasa ulio mkuta kwenye maisha yake.
Hii sio simulizi ya kuikosa ambayo utaipata kwa ofa .
Njoo whatsaapp nikutumie utangulizi huu kwa njia ya sauti 0746206428.
Huu ni mkasa mfupi wa aina yake ambao uta kuburudisha na kukufunza mengi.